Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Fenerbahce wamuwekea Rashford dau kubwa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Fenerbahce iko tayari kutoa ofa kubwa yenye thamani ya juu ili kumnasa Marcus Rashford, huku RB Leipzig ikikataa kulegeza msimamo wake katika mazungumzo na Real Madrid kuhusu usajili wa Yan Diomande, wakati Arsenal wameanza mazungumzo ya awali ya kumsajili Bruno Guimaraes.

Fenerbahce imejipanga kuvunja rekodi ya matumizi yake ili kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford (28), katika dirisha hili la usajili la majira ya joto. (The Sun)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyota chipukizi winga wa Ivory Coast, Yan Diomande (19), hatajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya ya RB Leipzig huku hatma yake ikipewa uzito mkubwa. Klabu hiyo inang'ang'ania ada ya euro milioni 130 (pauni milioni 111) katika mazungumzo ya kumuuza kwa Real Madrid. (The Athletic)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huohuo, Arsenal wamechukua hatua rasmi ya kumuwania kiungo wa kati nyota wa Brazil, Bruno Guimaraes, 28, kwa kuanza mazungumzo na Newcastle United. The Gunners wanatarajia kukamilisha dili hilo kwa ada inayokadiriwa kuwa kati ya pauni milioni 70 na 80. (Telegraph - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Paris Saint-Germain imeongeza kasi katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Ferran Torres, 26. (Fichajes - in Spanish)

Liverpool haina mpango wa kumuuza Cody Gakpo, 27, licha ya Tottenham kuonyesha wazi nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi. (Mail)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sunderland haina nia ya kumuuza mshambuliaji wa Haiti, Wilson Isidor, 25), katika dirisha hili la usajili licha ya kusakwa na klabu kadhaa, hasa West Ham. (Sky Sports)

Kipa wa Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen, 34, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Ajax ya Uholanzi kwa mkopo wa mwaka mmoja. (Sport - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Aston Villa yatengeneza dau la £30m kumng'oa kumng'oa kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Marc Bernal (19). (Sun)

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Endrick (20), ameanza kufuatiliwa na klabu ya Roma katika dirisha hili la usajili wa majira ya joto. (Fichajes - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Coventry City, iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ni miongoni mwa klabu tatu za Ligi ya Primia zinazomuwania winga wa Chelsea na Ukraine, Mykhailo Mudryk, 25. (Mail - subscription required)

Hull City, Ipswich Town and Coventry City wote wanamwania kiungo wa Everton na England, Tim Iroegbunam, 23, (Teamtalk).