Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Real inamfukuzia Olise Bayern Munich
Real Madrid inaandaa ofa kubwa ya thamani ya euro milioni 220 (pauni milioni 188) kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa, Michael Olise. (Fichajes - kwa Kihispania)
Tottenham inafikiria kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Ureno, Rafael Leao (27), ambaye yuko tayari kuhamia London. (Teamtalk)
Hatima ya Bradley Barcola katika klabu ya Paris St-Germain bado haijulikani, huku Arsenal na Liverpool zikiwa katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa (23). (Talksport)
Newcastle imemlenga kiungo wa Stuttgart na Ujerumani, Angelo Stiller (25), kama chaguo bora la kuimarisha safu yao ya kiungo. (Bild - kwa Kijerumani)
Manchester United inamfuatilia kwa karibu kipa wa San Lorenzo na Paraguay, Orlando Gill (26). (Fichajes - kwa Kihispania)
Mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi, Cody Gakpo (27), na winga wa Manchester City na Brazil, Savinho (22), wamo kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Tottenham katika dirisha la usajili la majira ya joto. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Trabzonspor na Ivory Coast, Christ Inao Oulai, mwenye umri wa miaka 20, ananyatiwa na klabu za Juventus, Fiorentina, Brentford, Brighton na RB Leipzig. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Beki wa Tottenham, Radu Dragusin, anatarajiwa kujiunga na Fiorentina kwa mkopo wa awali, huku kukiwa na sharti la kumnunua mchezaji huyo raia wa Romania kwa ada inayoweza kufikia pauni milioni 21.4 vigezo fulani vikitimizwa. (Sky Sports)
Hull City inataka kumsajili kipa wa Napoli na Serbia, Vanja Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 29, huku ikijiandaa kurejea katika Ligi Kuu ya England. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Beki wa Sporting na Ureno, Gonçalo Inacio, mwenye umri wa miaka 24, amekuwa mmoja wa wachezaji wanaolengwa zaidi na AC Milan ili kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa msimu ujao. (Fichajes - kwa Kihispania)
Beki wa Chelsea na Uingereza, Trevoh Chalobah, mwenye umri wa miaka 26, angependelea kuhamia Inter Milan msimu huu wa joto. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)