Magari 7 yaliyovunja rekodi kwa kasi duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu gari la kwanza lilipozinduliwa na Karl Benz mwaka 1886, wanadamu wamekuwa wakishindana kuunda magari bora na imara zaidi.
Katika kipindi cha miaka 140 iliyopita, watu wengi wamehatarisha maisha yao wakiendesha magari kwa kasi kubwa wakitafuta kukumbukwa na vitabu vya historia.
Wabunifu wa magari wametumia injini za mvuke, umeme, petroli na ndege ili kuendesha magari yao kwa kasi zaidi.
Hapa kuna baadhi ya magari yenye kasi zaidi ambayo yamevunja rekodi duniani.
7. The Railton

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama magari mengine mengi kwenye orodha hii, 'Railton Special' ilikuwa na injini mbili za ndege zilizochukuliwa kutoka katika boti za mwendo kasi.
Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Septemba 1938, John Cobb aliweka rekodi kwa kufikisha kasi ya kilomita 634.39 kwa saa (394.19 mph) - rekodi ambayo ilidumu kwa miaka 16.
6. The Spirit of America

Chanzo cha picha, Getty Images
Dereva Craig Breedlove aliinuka kwa kiwango kikubwa mwaka 1963 wakati gari lake 'The Spirit of America' lilipovunja rekodi kwa kasi.
Lilikuwa la kwanza kati ya kizazi kipya cha magari yenye injini ya ndege, likichukua injini yake kutoka katika ndege ya zamani ya kivita ya F-86.
Lakini ilikuwa na magurudumu matatu tu, mithili ya bajaji na kutembea kwa kasi ya kilomita 655.84 kwa saa mwaka 1963.
Lakini FIA (Fédération Internationale de l'Automobile), chombo kinachoongoza michezo ya magari, kilisema gari linahitaji kuwa na magurudumu manne, na kwa hivyo halikutambua rekodi hiyo.
5. The Green Monster

Chanzo cha picha, Getty Images
Gari la Art Arfons kutoka Marekani, 'Green Monster' Injini yake ilichukuliwa kutoka ndege ya F-104 baada ya kutupwa kutokana na kuharibika wakati wa safari ya ndege.
Arfons aliijenga upya na kujaribu injini hiyo katika bustani yake, ingawa uendeshaji wake ulikuwa wa siri, lakini majirani zake walishuhudia.
1964 bidii yake ilizaa matunda, na aliweka rekodi ya kasi ya 698.34 kwa saa, kabla ya kupoteza rekodi yake kwa Craig Breedlove mwaka mmoja baadaye.
4. The Spirit of America (Sonic 1)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tofauti na 'Spirit of America' ya kwanza ya Breedlove, toleo lake la pili (pia linaitwa 'Sonic 1') lilikuwa na magurudumu manne na lilitambuliwa na FIA lilipofika kasi ya kilomita 966 kwa saa Novemba 1965.
Pia ilikuwa na injini sawa na ile ya Art Arfons, na magari yote mawili yalibadilishana rekodi kati ya Oktoba 1964 na Novemba 1965 hadi Sonic 1 iliposhinda vita.
3. The Blue Flame

Chanzo cha picha, Getty Images
'Blue Flame' la Marekani, kimsingi ilikuwa roketi yenye magurudumu, ikawa gari la ardhini lenye kasi zaidi duniani mwaka 1970 likiendeshwa na Gary Gabelich kwa kasi ya kilomita 1,014.511 kwa saa.
Kukimbia kwake kulikuwa tofauti na magari mengine yenye rekodi ya kasi, na ilikuwa na uwezo wa kupandisha mafuta hadi kasi ya juu kwa sekunde 20 tu.
2. Thrust2

Chanzo cha picha, Getty Images
Muundo wa 'Thrust 2' unakumbusha sana gari la Art Arfons la 'Green Monster' la mwaka 1964, huku turbine ya ndege ikiwa imewekwa katikati ya gari.
Richard Noble alichochewa na hamu yake ya kurejesha rekodi ya kasi nchini Uingereza, na 4 Oktoba 1983, alifanikisha hili kwa kasi ya kilomita 1,019 kwa saa katika mbio katika Jangwa la Black Rock, Marekani.
1. Thrust SSC

Chanzo cha picha, Getty Images
Thrust SSC ndiyo gari lenye kasi zaidi duniani, likifikia kasi ya kilomita 1,223.6 kwa saa (maili 760.3 kwa saa). Dereva aliyeweka rekodi hiyo ni Andy Green.
Karibu miaka 30 baadaye, rekodi hii ya ajabu bado ipo.
Jaribio la mwisho la kushinda mafanikio haya lilikuwa la Bloodhound LSR, kwa bahati mbaya, kampuni iliyo nyuma ya mradi huo ilifilisika mwaka 2018 na majaribio zaidi ya kuufufua yamekwama hadi sasa.















