Moja kwa moja, Axio: Iran, Oman na Marekani zakaribia kufikia makubaliano ya kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz
Axios iliripoti, ikinukuu vyanzo viwili vya kikanda na afisa wa Marekani, kwamba Marekani, Iran, na Oman ziko karibu kufikia makubaliano ya muda ya kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz
Muhtasari
Asilimia 87 ya wafanyakazi wa Kenya waripoti msongo wa mawazo - Utafiti
Axio: Iran, Oman na Marekani zakaribia kufikia makubaliano ya kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz
Infantino aitisha kikao cha FIFA huku ukosoaji ukiongezeka
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Gianni Infantino
Gianni
Infantino amewaita viongozi wakuu wa shirikisho la soka duniani (FIFA) kwenye
mkutano nchini Morocco siku ya Jumatano, kufuatia siku nyingine ambapo rais wa
shirikisho hilo amekabiliwa na ukosoaji mkali kuhusu mpango wake uliositishwa
wa kuuza kuuza hisa za mashindano ya FIFA kwa wawekezaji binafsi.
Mkuu wa
maendeleo ya soka duniani wa FIFA, Arsene Wenger, Katibu Mkuu Mattias
Grafstrom, na Mwana mfalme Ali, rais wa Shirikisho la Soka la Jordan, wote
walionyesha wazi kupinga mpango wa Infantino unaojulikana kama 'Fifa Forward
Enterprise'.
Infantino,
ambaye amekuwa nchini Morocco kwa wiki iliyopita, aliitisha mkutano wa maafisa
watendaji mjini Rabat katika juhudi za kutafuta suluhisho la utata huo.
Katika
taarifa iliyotolewa kupitia FIFA, Wenger alisema kuwa kusitisha mpango huo
kulikuwa "jambo la lazima kabisa na lisilo na shaka yoyote".
Grafstrom
alielezea wiki iliyopita kama "mfululizo wa matukio ya kusikitisha na ya
kulaumiwa" katika barua pepe ya ndani iliyotumwa kwa wafanyakazi wa FIFA.
Wakati huo
huo, Mwana mfalme Ali aliishutumu FIFA kwa kuunda hali ambayo "inaweza
kuchukuliwa kama shinikizo la kulazimisha mambo" kuhusiana na fedha za
zawadi ambazo hazijalipwa na uungaji mkono kwa ajili ya kuchaguliwa tena kwa
Infantino.
Tangu mwaka
2019, Wenger amekuwa akishikilia wadhifa unaohusisha uchambuzi wa takwimu za
mchezo huo, mafunzo ya mtandaoni ya FIFA, na mashindano ya vijana.
Aliyekuwa kocha mkuu wa Arsenal hapo awali
aliunga mkono pendekezo la Infantino la kuandaa Kombe la Dunia la wanaume kila
baada ya miaka miwili
Asilimia 87 ya wafanyakazi wa Kenya waripoti msongo wa mawazo - Utafiti
Chanzo cha picha, Getty Images
Sekta ya
biashara nchini Kenya inakabiliwa na mgogoro unaoongezeka wa ustawi kazini, huku utafiti mpya ukionyesha kuwa
takriban wafanyakazi tisa kati ya kumi (87%) wanaripoti kupata msongo wa
mawazo, na kuibua wasiwasi mpya kuhusu tija, ushiriki wa wafanyakazi na
utendaji.
Matokeo
hayo, yaliyotolewa na shirika la Niche Human Capital Advisory, yanajiri wakati
ambapo waajiri wanakabiliwa na kuongezeka kwa uchovu, mabadiliko ya matarajio
ya wafanyakazi na kuongezeka kwa ushindani wa vipaji.
Nchini humo,
asilimia 80.4% ya wafanyakazi wanaripoti msongo wa mawazo wa wastani hadi
uliokithiri kazini, huku 67.8% ya wafanyakazi katika Afrika ya Kusini mwa
Jangwa la Sahara wakiripoti uchovu wa kihisia na uchovu, wakisisitiza ukubwa wa
changamoto inayowakabili waajiri.
Wakati huo
huo, 82.5% ya wafanyakazi wanaamini mashirika yanahitaji kufanya zaidi ili
kusaidia kuimarisha afya ya akili.
Axio: Iran, Oman na Marekani zakaribia kufikia makubaliano ya kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz
Chanzo cha picha, Reuters
Axios
iliripoti, ikinukuu vyanzo viwili vya kikanda na afisa wa Marekani, kwamba
Marekani, Iran, na Oman ziko karibu kufikia makubaliano ya muda ya kufungua
tena Mlango-bahari wa Hormuz.
Kulingana na
vyanzo vya habari vya Axios, serikali ya Marekani inatarajia kutangaza
makubaliano hayo siku ya Jumatano.
Maelezo ya
makubaliano hayo yanayoweza kufikiwa bado hayajatolewa na hakuna hata upande
mmoja kati ya pande hizo tatu uliothibitisha rasmi ripoti hiyo; hata hivyo,
siku ya Jumanne, vyombo vya habari vya Marekani vikinukuu vyanzo
vyao vilijaribu kuripoti vipengele vikuu vya mazungumzo hayo na masharti
yanayotakiwa na pande husika. Kama ilivyoripotiwa na Axios, vipengele vya
mazungumzo hayo vilikuwa kama ifuatavyo:
Meli zote
zinazoingia Ghuba ya Uajemi zitasafiri kupitia njia ya kaskazini na kupita
katika maji ya Iran.
Meli zote
zinazotoka Ghuba ya Uajemi kuelekea Bahari ya Oman zitapita kupitia njia ya
kusini na katika maji ya Oman, kwa uratibu na Iran.
Katika
kipindi cha utekelezaji wa siku 60 cha makubaliano hayo ya muda, hakuna ushuru
au ada yoyote itakayotozwa kwa meli zinazopita.
Pande
zinazohusika na makubaliano hayo zitajitolea kutekeleza operesheni ya kuondoa
mabomu ya baharini katika njia ya katikati ya Mlango-bahari wa Hormuz ndani ya
siku 30.
Mara tu njia
ya katikati itakapokuwa imesafishwa, itatumika kwa ajili ya usafiri wa meli
zinazoingia na kutoka. Utaratibu wa matumizi ya njia hiyo utaamuliwa katika
makubaliano ya kudumu yatakayojadiliwa kati ya Iran na Oman.
Vifo vya ajabu vya tembo nchini Kenya vyaibua maswali kuhusu dawa za kuuwa wadudu
Chanzo cha picha, GETTY
Maelezo ya picha, Tembo aliyefariki
Habari
kwamba vifo vya hivi karibuni vya tembo 15 huenda vilisababishwa na dawa za kuuwa
wadudu zilizopulizwa kwenye mashamba ya nyanya yanayozunguka Hifadhi ya Taifa
ya Amboseli vimezua wasiwasi na maswali nchini Kenya.
Wiki
iliyopita, Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya (KWS) lilisema kuwa
baadhi ya tembo hao waliokufa kati ya tarehe 24 Juni na 24 Julai walionyesha
dalili za "kupooza kwa sehemu ya mwili," jambo lililoashiria sumu
inayotokana na kemikali ya 'cyanide' inayopatikana katika dawa hizo za kuuwa
wadudu.
Hata hivyo,
wanaharakati wa uhifadhi wameiambia BBC kwamba huenda hiyo isiwe ndiyo picha
kamili ya hali halisi.
Wakulima
tuliozungumza nao katika eneo hilo pia walionyesha kutokuwa na uhakika na madai
hayo.
"Tumeishi
na wanyamapori hawa kwa miongo kadhaa na hatujawahi kushuhudia jambo kama
hili," Daniel Nina, anayewakilisha baadhi ya wamiliki wa ardhi katika eneo
hilo, aliambia BBC.
"Ndiyo
maana tunajiuliza ni kwa nini jambo hili linatokea leo."
Mashamba
hayo ya nyanya yanapatikana katika eneo la Kimana, ambalo ni sehemu ya njia ya
wanyama inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Amboseli na Hifadhi ya Taifa ya
Tsavo kusini mwa Kenya.
Eneo hilo
kubwa, linalojulikana kama mfumo wa ikolojia wa Amboseli, linapakana na nchi
jirani ya Tanzania na ni njia inayotumiwa na zaidi ya tembo 2,000 kutafuta
chakula na maji.
Mashamba
hayo hustawi kutokana na maji yanayotiririka kutoka Mlima Kilimanjaro ulio
karibu, na hutoa mazao yanayouzwa katika masoko ya Nairobi, mji mkuu wa Kenya,
na maeneo mengine.
Daktari Mkuu
wa Mifugo katika Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya, Dkt. Isaac
Lekolool, alituambia kuwa waligundua chembechembe za sumu ya 'cyanide' katika
sampuli zilizochukuliwa kutoka kwenye matumbo ya tembo hao.
Anasema kuwa
hawajaacha uwezekano wa sumu kuwekwa makusudi, lakini kwa sasa haiwezekani
kubaini nini hasa kilichosababisha vifo vya tembo hao.
"Ni
vigumu kusema kwa sababu hatujawahi kushuhudia visa vya aina hii hapo awali. Ni
tukio la kipekee, na lilitokea ndani ya kipindi cha takriban mwezi mmoja,"
alisema Lekolool.
Dhana yao ya
awali ni kwamba tembo hao walikumbana na sumu hiyo kupitia dawa za kuuwa wadudu
zilizopulizwa katika mashamba ya nyanya yaliyo karibu.
"Huenda
ilitokea bila kukusudiwa. Labda watu walikuwa wakijaribu kudhibiti wadudu
kwenye mazao yao, na hilo linaweza kuwa ndilo chanzo."
Tatizo la
dawa za kuua wadudu.
Ripoti ya
mwaka 2024 kutoka kwa shirika la Kenya linaloshughulikia usalama wa chakula,
Route to Food, ilibaini mkulima mmoja katika eneo la Kimana akitumia dawa ya
kuuwa wadudu iliyokuwa na "kiambato amilifu" ambacho ni " kemikali ya sianidi".
Wangunyu
Njuguna, mwandishi wa ripoti hiyo, alisema kuwa licha ya kupigwa marufuku
nchini Kenya, baadhi ya kemikali hatari za kilimo huingizwa nchini kwa njia ya
magendo kupitia mpaka wa Tanzania.
"Tatizo
kubwa ni kwamba hatutekelezi viwango sawa katika eneo hili," alisema
Njuguna. "Hakuna anayekagua ninachoenda kununua ninapovuka mpaka, hivyo
naweza kwenda kununua chochote na kupita mpakani bila mtu yeyote
kunizuia."
Kemikali
hatari sana zinapatikana kwa wingi katika mashamba ya Kenya na baadhi yake
zimehusishwa na magonjwa hatari.
Ingawa kuna
kanuni zinazopiga marufuku kemikali haramu za kilimo, utekelezaji wake ni
dhaifu na hakuna umakini wa kutosha kuhusu jinsi kemikali hizo zinavyoweza
kuathiri wanyama.
Chanzo cha picha, Getty Images
Tazama Video ya droni ya Urusi ikimfukuza mchuuzi nchini Ukraine
Maelezo ya video, Ukrainian vegetable seller targeted in 'human safari' drone attack
Rais wa
Ukraine, Volodymyr Zelensky, amechapisha video kwenye mitandao ya kijamii
inayoonyesha droni ikimwinda mwanamume kusini mwa Ukraine, akisema kuwa tukio
hilo linaonyesha shambulio la Kirusi la aina ya "safari" (uwindaji wa
burudani) dhidi ya raia.
Video hiyo
inaonyesha droni ikimfuatilia mchuuzi katika barabara ya jiji katika eneo la
Kherson.
Mwanamume
huyo anajaribu kujiepusha na droni inayoning'inia juu yake, kabla ya droni hiyo
kuanza kumkimbiza huku akikimbia kuzunguka gari jeupe la aina ya van.
Hatimaye,
droni hiyo inashuka kwa kasi na kulipuka ilipomgonga.
Mwanamume
huyo alinusurika akiwa na majeraha mengi ya vipande vya chuma, mtikiso wa
ubongo na mshtuko wa kisaikolojia, daktari alisema.
Matumizi ya
droni zinazoendeshwa kwa mbali dhidi ya raia, jambo ambalo wakati mwingine
huitwa "uwindaji wa binadamu" (human safari) yamekuwa yakitumiwa mara
kwa mara na Warusi kuwatia hofu wakazi wa maeneo ya mstari wa mbele wa vita
nchini Ukraine.
"Lazima
dunia ione hili," Zelensky aliandika kwenye Telegram. "Lazima ione
kila ushahidi kwamba Urusi imepoteza akili, na kila ukweli kwamba askari wa
Urusi wanafurahia kuua na kuwatesa watu."
Video hiyo
ilionyesha "uhalifu wa kivita wa kikatili," alisema Waziri wa Mambo
ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha.
Vitendo
hivyo vya uwindaji vilikuwa "mkakati wa makusudi na wa kimfumo wa
Urusi," Sybiha alisema.
"Mtu huyo mwenye tabia ya kikatili na ya
kufurahia mateso anayeendesha droni hii anajua kwamba anamshambulia raia."
Aliongeza
kuwa shambulio hilo lilikuwa sehemu ya kampeni ya makusudi ya Urusi ya
kuwatisha raia na akataka kulaaniwa kimataifa.
Klabu ya Uturuki Trabzonspor yaanza mazungumzo ya kumsajili Mohamed Salah
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mohammed Salah
Klabu ya
Trabzonspor ya Uturuki imetangaza kuwa imeanza mazungumzo ya kumsajili Mohamed
Salah.
Mshambuliaji
huyo raia wa Misri, mwenye umri wa miaka 34, aliondoka Liverpool mwishoni mwa
msimu uliopita na kwa sasa yuko katika mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo kama
mchezaji huru, bila kufungwa na mkataba rasmi na klabu yoyote ya michezo.
Katika
taarifa yake, Trabzonspor imesema kuwa Salah atawasili Istanbul siku ya
Jumatano.
Taarifa hiyo
iliongeza: "Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Trabzon jioni hiyo
hiyo."
Iliongeza
pia: "Tarehe ya kuwasili kwa mchezaji huyo na maelezo mengine kuhusu
ratiba ya mapokezi yake huko Trabzon yatatangazwa kupitia njia rasmi za
mawasiliano za klabu hiyo katika kipindi cha siku hiyo."
Bei ya mafuta yashuka kufuatia matumaini ya kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mlango bahari wa Hormuz
Bei ya
mafuta ilishuka hadi kiwango cha chini cha wiki tatu Jumanne huku maafisa wakuu
wa Marekani wakiongeza matumaini ya makubaliano na Iran ya kufungua tena njia
kuu ya maji ya Hormuz.
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Waziri wa Hazina Scott Bessent wote
walitangaza kwamba mazungumzo yameendelea ili kuruhusu uwezekano wa usafirishaji kuanza tena haraka
iwezekanavyo wiki hii.
Gharama ya
pipa la mafuta ghafi ya Brent, kipimo cha kimataifa cha bei ya mafuta, ilishuka
kwa karibu 5% hadi chini ya $80 (£60) kutokana na habari za usumbufu wa
usambazaji unaoweza kupungua.
Lakini
kushindwa kwa mazungumzo ya awali katika miezi ya hivi karibuni ili kupunguza
mzozo kati ya Marekani na Iran kumesababisha soko la mafuta tete, huku madereva
hatimaye wakiathiriwa na bei kubwa za mafuta kwenye pampu.
Siku ya
Jumanne, pamoja na kushuka kwa mafuta ghafi ya Brent, bei za kati za Marekani
Magharibi mwa Texas zilishuka kwa zaidi ya 5%, hadi $76 kwa pipa.
Mikataba
yote miwili ilishuka hadi viwango vyao vya chini kabisa tangu Julai 13.
Rubio
alisema kumekuwa na maendeleo yaliyopatikana katika majadiliano kuhusu kupeleka
meli zaidi kupitia njia hiyo na Iran na Oman.
"Kumepatikana
maendeleo katika mazungumzo hayo, lakini bado hayajakamilika. Tunatumai hilo
litatokea hivi karibuni," aliwaambia waandishi wa habari katika Wizara ya
Mambo ya Nje.
Bessent
alisema makubaliano ya kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz yanaweza kuafikiwa
siku ya Jumanne au Jumatano.
Meli ya India yazama baada ya kupigwa kombora karibu na maji ya Yemen
Waziri wa
Usafirishaji wa India anasema meli ya India ilipigwa na kitu kilichorushwa, na
kusababisha ipinduke na kuzama karibu na maji ya Yemen.
Alisema:
"Wanamaji wote 14 waliokuwa kwenye meli hiyo waliokolewa salama na Kikosi
cha Walinzi wa Pwani cha Yemen."
Wizara ya
Mambo ya Nje ya India ililaani shambulio hilo "vikali" katika taarifa
yake.
"Tunalaani
shambulio dhidi ya meli ya kibiashara yenye bendera ya India, MSV Faiz Noor
Alia, ambayo ilizama katika Bahari ya Shamu karibu na pwani ya Yemen mnamo
Agosti 4, 2026. Raia wote 13 wa India wameokolewa," wizara hiyo ilisema
katika taarifa..
Bloomberg: Iran inazingatia kuruhusu Ulaya kushiriki katika kuondoa mabomu ya baharini yaliotegwa katika Mlango-bahari wa Hormuz
Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock
Shirika la
habari la Bloomberg liliripoti, likinukuu wanadiplomasia wenye taarifa za
ndani, kwamba Iran inafikiria kuonyesha utayari kwa nchi za Ulaya kushiriki
katika shughuli za kuondoa mabomu yaliotegwa baharini katika Mlango-bahari wa Hormuz; hatua
ambayo inaweza kuwa sehemu ya makubaliano ya kurejesha hali ya kawaida ya
usafirishaji katika njia hiyo ya maji na kurahisisha mazungumzo ya amani na
Marekani.
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo, Iran imesisitiza mara kwa mara katika misimamo yake ya
hadharani kwamba haitaruhusu nchi za kigeni kushiriki katika shughuli za
kuondoa mabomu hayo katika njia hiyo muhimu ya kimkakati kwa usafirishaji wa
mafuta na gesi asilia.
Hata hivyo,
kulingana na wanadiplomasia waliozungumza na Bloomberg kwa sharti la kutotajwa
majina kutokana na unyeti wa suala hilo, Tehran imelainisha msimamo wake kiasi
katika mikutano ya faragha katika wiki za hivi karibuni na inazingatia
uwezekano wa nchi za Ulaya kushiriki katika operesheni hiyo.
Bloomberg iliripoti siku ya Jumanne kwamba iwapo
mabadiliko hayo yatatekelezeka, hatua hiyo inaweza kuwa sehemu ya juhudi za
kidiplomasia za kurejesha usalama wa usafirishaji katika Mlango-bahari wa
Hormuz na kupunguza mivutano kati ya Iran na Marekani
CBS: Marekani imetumia karibu akiba yake yote ya makombora ya masafa marefu katika vita dhidi ya Iran
Chanzo cha picha, CENTCOM
Vyanzo
viwili vimeiambia CBS News - mshirika wa BBC nchini Marekani - kwamba Marekani
imetumia karibu akiba yake yote ya dunia nzima ya makombora ya masafa marefu
yenye usahihi wa hali ya juu wakati wa vita dhidi ya Iran.
Kulingana na
ripoti hii, Marekani imetumia karibu makombora yake yote ya aina ya *Army
Tactical Missile System* (ATACMS) na makombora ya kushambulia kwa usahihi
(*Precision Strike Missiles*) katika Operesheni Epic Fury.
Awali,
Reuters iliripoti kuwa Marekani ilikuwa imetumia "karibu makombora
yote" ya masafa marefu yenye usahihi wa hali ya juu katika operesheni hii.
CBS
iliripoti hapo awali kuwa akiba ya Marekani ya makombora ya kuzuia mashambulizi
(*interceptor missiles*) na makombora ya masafa marefu imepungua sana, na jambo
hili limekuwa changamoto ya ndani kwa serikali.
Kulingana na
ripoti hiyo, Marekani haiwezi kuendelea na mwenendo huu kwa kasi ileile
iliyotumika kumaliza akiba ya silaha hizo mwanzoni mwa vita dhidi ya Iran.
Maafisa wa
Marekani wamesema kuwa akiba ya makombora haya ni finyu, lakini suala la
dharura zaidi ni idadi ya makombora ya kuzuia mashambulizi ya aina ya Patriot
na THAAD, ambayo yanatumika kwa kasi kubwa kuliko uwezo wa viwanda vya ulinzi
vya Marekani wa kuyazalisha.
Sean
Parnell, msemaji mkuu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), alisema
katika taarifa kwa CBS:
"Jeshi
la Marekani ndilo jeshi lenye nguvu zaidi duniani na lina kila kitu
kinachohitajika kutekeleza majukumu yake wakati wowote na mahali popote ambapo
rais ataamua. Tumefanya operesheni kadhaa zilizofanikiwa katika maeneo
mbalimbali huku tukihakikisha kuwa jeshi la Marekani lina akiba kubwa ya uwezo
wa kulinda watu na maslahi ya taifa."
Waziri wa
Ulinzi wa Marekani, Pete Hegsett, hapo awali alitupilia mbali wasiwasi kuhusu
kupungua kwa akiba ya silaha za Marekani. Aliambia CBS mnamo Julai 14:
"Hii ni
habari ya kubuni ambayo vyombo vya habari vinataka kuisambaza. Hatimaye, akiba
yetu iko katika hali nzuri na inaendelea kuimarika zaidi."
Ripoti hii
inakuja wakati matumizi makubwa ya makombora ya kuzuia mashambulizi na silaha
zenye usahihi wa hali ya juu katika vita vya hivi karibuni yamechochea mijadala
mjini Washington kuhusu uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ulinzi vya Marekani
na utayari wake kwa mzozo wa muda mrefu.