Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Winga wa Ivory Coast Diomande kutua Real Madrid

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid imefikia makubaliano na klabu ya RB Leipzig kumsajili winga wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19, Yan Diomande kwa hadi euro milioni 140 (£120m), kufuatia mazungumzo ya muda mrefu. (Athletic - usajili unahitajika)
Liverpool inatathmini uwezekano wa kumsajili winga wa Paris St-Germain na Senegal mwenye umri wa miaka 18, Ibrahim Mbaye. (Times - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool inahusishwa na tetesi za kumsajili beki wa Real Madrid, Raul Asencio, aliye na umri wa miaka 23, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kufahamishwa kuwa huenda akaondoka katika klabu hiyo ya La Liga msimu huu wa kiangazi. (Teamtalk)
Aston Villa imefikia makubaliano na Atletico Madrid kumsajili beki wa kushoto wa Italia, Matteo Ruggeri, mwenye umri wa miaka 24. (Marca - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wapo kwenye hatua za mwisho kumsajili kiungo wa Southampton na Ireland Kaskazini, Shea Charles (22), katika dili linalokadiriwa kufikia pauni milioni 30. Klabu hiyo ya London inaonekana tayari kumaliza mchakato wa kumnasa nyota huyo mwenye kipaji. (Talksport)
Trabzonspor inafanya juhudi za kumrejesha pamoja mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Núñez (27), na aliyekuwa mwenzake wa Liverpool, mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah (34), katika klabu hiyo ya Uturuki. Núñez kwa sasa anachezea Al-Hilal. (Spor Depor - in Turkish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wako tayari kupokea ofa mpya kutoka kwa Arsenal kwa ajili ya beki wa England, Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 28, huku wakijaribu kufikia makubaliano ya mkataba mpya ili kuhakikisha anaendelea kubaki Villa Park. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid huenda ikawaruhusu viungo wawili wa Ufaransa, Aurélien Tchouaméni (26) na Eduardo Camavinga (23), ambao pia wanawaniwa na Manchester United, kuondoka ili kupata fedha za kumsajili kiungo nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri (30 (El Nacional - in Spanish)
Hamburg wameonyesha nia ya kumsajili beki wa Leeds United na timu ya taifa ya Ubelgiji, Sebastiaan Bornauw (27). Klabu hiyo ya Ujerumani inapanga kumrudisha beki huyo wa Leeds United kwenye Bundesliga. (Hamburger Abendblatt - in German)














