Kijiji kinacholala kwa hofu: Wapalestina wanaoshambuliwa na walowezi

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Lango kuu la chuma la nyumba ya familia ya Abu Alia katika kijiji cha al Mughayyir katika eneo la Ukingo wa Magharibi limestahimili mashambulizi ya walowezi, wengi wao wakiwa vijana; Vyuma vyake vyemba vililia kwa kila pigo huku wakiigonga tena na tena kwa fimbo zao.

Lakini matusi yaliyotolewa na pande zote mbili siku hiyoyalipita lango hilo.

Tusi la kuudhi hasa—ambalo karibu liendane na lugha zote mbili za Kiebrania na Kiarabu—lilitamkwa kwa dharau na vijana wa kiyahudi waliokuwa wakigonga mlango kwa hasira huku Mpalestina aliyesimama upande wa pili wa lango akirekodi tukio hilo kwa simu yake.

Lango hili, lililo nje kidogo ya al Mughayyir, limekuwa mstari wa mbele kila wiki katika kupigania Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Na aina hii ya mashambulizi ya walowezi dhidi ya makaazi ya Wapalestina ni utaratibu wa kila wiki unaofanywa katika eneo hili.

Tulipofika al Mughayyir siku hiyo, makabiliano katika boma ya Abu Alia tayari ilikuwa imeanza.

Jeshi la Israel na polisi wa mpakani walikuwa tayari wanashika doria mitaani, na wakaazi walikuwa wakikimbia kutoka makwao; hapa, askari, kama walowezi, wanachukuliwa kuwa maadui.

Kutoka kwenye kilima kilicho mkabala na eneo hilo, msikiti wa hapo ulitoa wito kwa watu kuisaidia familia iliyokuwa imezingirwa na walowezi.

Hata hivyo, kujaribu kuwakwepa askari wa Israel kumekuwa hatari kubwa.

Wakazi, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wamepigwa risasi wakati wa operesheni za kijeshi za Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Hali hii inachukuliwa kuwa ya kawaida wakati wa wikendi huko al-Mughayyir na vijiji vingine vya Ukingo wa Magharibi, ingawa ni nadra sana kuangaziwa kwenye vyombo vya habari vya ndani.

Tulitumia wiki moja katika eneo linalozunguka al-Mughayyir na kijiji jirani cha Khirbet Abu Falah ili kushuhudia jinsi maisha yalivyo kwa jamii, au hata kwa familia moja tu.

Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonyesha jinsi udhibiti wa eneo hili unavyobadilika kwa kasi, na jinsi mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa eneo hilo yalivyo sehemuya mpango mpana wa kitaifa unaolenga kuweka ardhi ya Ukingo wa Magharibi chini ya udhibiti wa Israel.

Tangu iliponyakua eneo la Ukingo wa Magharibi mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya Kati, Israel imejenga zaidi ya makazi 100 yanayohifadhi zaidi ya Wayahudi laki tano kwenye ardhi ambayo Wapalestina wanaitaka iwe taifa lao la baadaye.

Baadhi ya walowezi wa Kiyahudi pia wameanzisha mamia ya vituo visivyo rasmi—mara nyingi vikianza na hema moja au gari la kukaa (caravan) juu ya kilima, na mara nyingi karibu sana na nyumba za Wapalestina. Makazi rasmi ya Israel na vituo hivyo visivyo rasmi vyote ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amewataja wale wanaofanya mashambulizi hayo ya walowezi kuwa ni kundi dogo la vijana waliopotoka: "wahalifu 150 wenye umri mdogo," aliwaita hivyo, au "vijana 70 kutoka katika familia zilizosambaratika."

Walowezi waliovunja lango la nyumba ya Abu Alia siku hiyo ya Jumamosi huko al-Mughayyir walionekana kuwa vijana wadogo, lakini mapema siku hiyo, kundi la walowezi lilikuwa limetoa wito kwenye mitandao ya kijamii wa "kumfukuza adui," likijumuisha maandiko kutoka kwenye Torati.

"Msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo mbele yenu, wale mtakaowaacha watakuwa kama miiba machoni mwenu na michongoma ubavuni mwenu," inasema sehemu hiyo ya maandiko.

Na nyuma ya nyuso hizo changa kwenye lango huko al-Mughayyir kulikuwa na walowezi wenye umri mkubwa zaidi—ambapo angalau mmoja wao alikuwa na silaha—wakisimama pamoja na askari wa Israel si mbali na nyumba hiyo.

Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wanaamini kwamba askari wa Israel wa awaunga mkono walowezi wanaovamia makaazi yao.

Kanda ya video iliyorekodiwa na familia ya Abu Alia inayoonyesha jinsi askari wanavyotembea ndoa kwa upole. Haifai: vijana hao hurudi tena na tena kufanya ghasia katika lango hilo, huku mwanamke aliye ndani akiwafokea kuwataka waondoke.

Wanajeshi waliosimama nao langoni hawajaribu kuhoji au kuwaweka kizuizini washambuliaji, au hata kuwanyang'anya marungu yao.

Kanda za video, zilizorekodiwa kutoka kwa boma la Abu Alia, zinaonekana kuwaonyesha walowezi vijana wakivunja uzio unaozunguka mali hiyo, huku wanajeshi wakiwa wamesimama karibu na eneo la tukio bila kuchukua hatua yoyote.

Tuliuliza Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kuhusu matukio haya. Haikutoa maelezo ya matukio hayo, lakini ilisema katika majibu ya jumla kuwa inachunguza madai ya uharibifu wa mali.

Rafeeq Abu Alia, ambaye alikuwa mmoja wa wanafamilia katika nyumba hiyo siku hiyo, aliiambia BBC kuwa shambulio hilo lilikuwa limefuata mtindo uliozoeleka.

"Jambo la kwanza asubuhi ya leo, walikuja ... Kulikuwa na walowezi wanne na walikuwa na silaha. Kisha walowezi zaidi wakaja na kuizingira nyumba hiyo, wakitukana na kutuchokoza," alisema. "Walikuja na jeshi. Wanajeshi waliingia, wakifuatiwa na walowezi. Jeshi liliwapiga watu ndani ya nyumba."

Tuliwarekodi wanajeshi wakijaribu kuvunja lango la Abu Alias ​​siku hiyo, huku walowezi wakisimama kando yao. Na baadaye kuona wafanyikazi wakirekebisha mlango uliovunjika.

Madaktari waliiambia BBC kwamba wamewatibu Wapalestina kadhaa kwa gesi ya machozi na majeraha ya kupigwa, na kwamba mtu mwingine alikuwa amepelekwa hospitalini akiwa na jeraha la risasi.

IDF isema vikosi vyake vilikuwa al-Mughayyir siku hiyo, kujibu ripoti za makabiliano kati ya Wapalestina na raia wa Israel.

Ilisema kuwa askari waliingia katika nyumba moja kijijini hapo kuwasaka washukiwa waliokuwa wakirusha mawe, na kwamba wanamshikilia mtu mmoja kwa kujihusisha na kile ilichokiita "machafuko makali".

Ilisema inachunguza madai ya ghasia za wanajeshi.

Pia ilisema Wapalestina waliojifunika nyuso zao waliwapura mawe wanajeshi katika hali ambayo ililazimu vikosi vyake kufyatua risasi kuondoa tishio hilo, na kwamba "tishio lilitambuliwa", ikimaanisha kuwa mtu alipigwa risasi.

Sheria za kujihusisha kwa wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi zililegezwa ili kuruhusu wanajeshi kuchukua hatua kali dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakirusha mawe, baada ya mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023 ambayo yalisababisha vita vya Gaza.