Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege 10 bora za kivita duniani mwaka 2026
Nchi zenye silaha bora Duniani, ndio kwa sehemu kuwa humiliki au kuzalisha ndege zenye ubora katika mapambano ya kivita. Ndege hizi zipo ambazo huuzwa kwa nchi nyingine, na zile ambazo haziwezi kabisa kuuzwa.
Ndege bora zaidi za kivita duniani mwaka 2026, zimeoorodheshwa kutokana na uwezo wa mapigano. Pia uzito wake na uwezo wa kukwepa makombora, utambuzi wa adui na ushiriki wa data, uwezo wa kulenga silaha, na rekodi ya mapigano.
Toleo la ndege hizi ndio ishara moja ya nguvu ya ndege, kwa hivyo ndege za kivita za toleo la tano ndio zinaongoza kwa ubora, huku toleo la 4.5 zikifuata nyuma. Orodha hii ni kwa mujibu wa mtandao unaofuatilia vyombo vya anga, Aero Corner.
Lockheed Martin F-22 Raptor
Ndege ya kivita aina ya F-22 ndiyo ndege bora zaidi ya kivita kuwahi kutokea. Ina vipengele vyote muhimu vya ndege na hutembea kwa kasi ya kilomita 2,410 kwa saa.
Injini mbili za F119 ndio zinazoifanya iwe ya hatari katika mapigano, na ina uwezo wa kulenga shabaha kutoka mbali. Mchanganyiko wa kasi, uwezo wa kujificha kutokana na rada, na ujanja wa angani ndio maana inashika nafasi ya kwanza.
Raptor ndiyo ndege pekee ya kivita ya kiwango cha juu ambayo Marekani imekataa kuuza nje. Sheria ya mwaka 1998 ilipiga marufuku mauzo ya nje ili kulinda siri zake za kujificha na rada na vifaa vyake, kwa hivyo ndege zote 186 zinatumika tu na Jeshi la Anga la Marekani.
Uzalishaji uliisha mwaka 2011, ndiyo maana ndege hizo sasa ndizo ndege adimu zaidi.
Lockheed Martin F-35 Lightning II
F-35 inatembea kilomita 1,930 kwa saa. Ndege aina ya F-35 huunganisha taarifa ya rada, picha, na vita vya kielektroniki katika picha moja, na hivyo kumruhusu rubani kuona na kupiga shahaba.
Inapatikana katika matoleo matatu, na imetumika katika misheni za mashambulizi za vikosi vya anga. Inashikilia orodha ya ndege bora za kivita za Marekani pamoja na Raptor.
Kuna zaidi ya ndege 1,100 za aina hii zilizotolewa kufikia mwaka 2026 na nyingine zinazalishwa kwa ajili ya mataifa zaidi ya kumi na mbili, F-35 imekuwa uti wa mgongo wa nguvu ya anga ya Magharibi.
Chengdu J-20 Mighty Dragon
Ndege ya kivita ya J-20 ya China ndiyo inatoa changamoto kwa ndege za kivita za Marekani, imeundwa ili kushambulia maeneo muhimu kama ndege au meli za mafuta na ndege za rada za angani.
Inabeba kombora la PL-15 lenye kasi ya kilomita 2,469.6 kwa saa. Uzalishaji wake unaongezeka kwa kasi zaidi kuliko ndege nyingine yoyote ya kizazi cha 5, mbali na F-35.
Makombora yake hushambulia ili kuharibu meli za mafuta na ndege za rada za adui. Ndiyo maana J-20 inawatia wasiwasi wa-Magharibi kutokana na uwezo wake katika mapigano.
Sukhoi Su-57 Felon
Su-57 ya Urusi ni ndege ya kivita ya kizazi cha 5, lakini ni ya nne kwa sababu ya uchache wa ndege zilizopo na idadi kubwa ya taarifa zake hazijathibitishwa. Inaweza kuendeshwa kwa urahisi, na injini yake ni ya kasi sana.
Udhaifu wake ni kuweza kuonekana katika rada na ukubwa.
Eurofighter Typhoon
Ndio ndege bora zaidi miongoni mwa ndege zinazoweza kuonekana na rada duniani, na ndio ndege bora zaidi katika safu ya vizazi 4.5. Inaendeshwa na Uingereza, Ujerumani, Italia, Uhispania na wateja wa nje.
Ina kasi ya takriban kilomita 1,320 kwa saa. Inatumia kombora la Meteor. Ndege hii hutumia rada ya AESA ambayo huifanya Typhoon kushindana dhidi ya vitisho visivyoonekana.
Dassault Rafale
Rafale ya Ufaransa ndiyo ndege ya kivita ya kizazi 4.5 yenye uwezo mkubwa zaidi. Ni bora katika mashambulizi, na upelelezi. Hutembea karibu kilomita 1,320 kwa saa saa na hubeba kombora la Meteor.
Kinachoitofautisha na Typhoon ni seti yake ya vifaa vya kielektroniki vya SPECTRA, mojawapo ya mifumo bora ya kujilinda, na ina rekodi nzuri ya mapigano Libya, Mali, Iraq, na Syria.
Usafirishaji wake nje kwenda India, Misri, UAE, Qatar, na Ugiriki umeifanya kuwa ndege ya kisasa bora ya Ufaransa nje ya nchi, na kuwa maarufu miongoni mwa ndege bora za kivita za Ufaransa.
Boeing F-15EX Eagle II
F-15EX ni uthibitisho kwamba muundo wa miaka 50 bado unaweza kuwa moja ya ndege bora zaidi duniani. Ina kasi ya takriban kilomita 2,655 kwa saa, na inaweza kubeba makombora mengi zaidi ya angani kuliko ndege nyingine yeyote.
Sio ya siri, kwa hivyo inafanya kazi kama lori la makombora ya masafa marefu nyuma ya F-22 na F-35, ni moja ya ndege kubwa zaidi za kivita zinazohudumu.
Saab JAS 39 Gripen E
Gripen E ndio ndege nyepesi zaidi duniani. Ni ndege ya injini moja yenye kasi, rada ya kisasa ya AESA, vifaa vya kielektroniki vya hali ya juu, na kombora la Meteor.
Imejengwa ili kutua kwenye barabara na kusukumwa na watu wachache, falsafa ya usanifu inayolenga kupunguza gharama za utengenezaji na marekebisho.
Boeing F/A-18E/F Super Hornet
Super Hornet ni ndege ya Marekani yenye injini mbili, yenye kasi na rada ya AESA.
Uwezo wake wa nyumbulifu, na uwezo wa kubeba silaha za aina mbalimmbali, ndio huiweka katika kumi bora.
Sukhoi Su-35 Flanker-E
Su-35 ni ndege ya kivita ya Urusi na moja ya ndege yenye kasi na masafa marefu ya mapigano.
Rada yake ina na sahihi.
Ndege hii inahitimisha orodha ya ndege kumi bora zaidi duniani 2026.