Sikuweza kumtambua mtoto niliyejifungua

Chanzo cha picha, Samina Ali
"Mwonekano wangu wa nje ulikuwa sawa. Nilikuwa bado mdogo, nilikuwa mzima kiafya, ila nilikuwa na hisia fulani hivi isiyo ya kawaida, kuwa kuna jambo ambalo haliko sawa. Kuna kitu kilikuwa kinanisumbua"
Wazo hili kuwa kuna jambo ambalo haliko sahihi lilimfuata Samina Ali maisha yake yote.
Samina Ali, amezaliwa katika familia ya kiislamu, na amekulia nchini India pamoja na Marekani
Wazazi wake wanaamini kuwa alizaliwa siku yenye bahati nzuri, na walifanya kila wawezalo kumkinga, na hirizi za fedha wakihofia kuwa maisha yake huenda yakakumbwa na maumivu na bahati mbaya.
Lakini wakati wa ujauzito wake wa kwanza mwaka 1999, madaktari wake hawakuwa na wasiwasi wowote wa aina hiyo. Walipofanya uchunguzi wa picha (scan) wa kijusi kilichokuwa bado kidogo, waliridhishwa na kile walichokiona na kukisikia.
"Hakukuwa na chochote isipokuwa mapigo ya moyo yenye nguvu sana, kama farasi anayekimbia kwa kasi,"
Samina aliiambia kipindi cha Outlook cha BBC News World Service kuwa "Sauti ya mpigo wa moyo ulijaza chumba kizima, na nilifikiri labda nilikuwa nawaza kupita kiasi. Lakini nilipofika mwezi wa saba wa ujauzito, dalili zilianza. Nilikuwa nimevimba sana kiasi kwamba nilihisi vidole vyangu vinagusana nilipokuwa nikiandika kwenye kompyuta, nilikuwa natapika, na pia nilianza kuwa na mabadiliko katika uwezo wangu wa kuona."
Hata hivyo, madaktari waliendelea kumwambia kwamba alikuwa "bado mchanga, mwenye afya njema, na kwamba hakuwa na tatizo lolote."
Changamoto za ujauzito
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Enzi hizo, haikuwa rahisi kufanya utafutaji wa haraka kwenye mitandao.
"Tuligeukia vitabu, hasa kitabu cha What to Expect When You're Expecting," "Mwishoni mwa kitabu hicho kulikuwa na takriban ukurasa mmoja kuhusu pre-eclampsia, uliotaja baadhi ya dalili nilizokuwa nazo."
'Pre-eclampsia' ni tatizo la ujauzito linaloanza kutokana na matatizo ya kondo la nyuma au placenta. Madaktari bado hawaelewi kikamilifu kwa nini hutokea, lakini linaweza kuwa hatari sana na kuathiri viungo mbalimbali vya mwili, hata ubongo.
Wanawake wenye asili ya Kiafrika au Asia ya Kusini wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata hali hii. Dalili zake ni pamoja na shinikizo la juu la damu, maumivu makali ya kichwa, kuwepo kwa protini kwenye mkojo, na ukungu.
Wasiwasi wao ulipoongezeka, Samina na mume wake waliamua kumwona daktari tena.
"Mtoto wangu alikuwa anatarajiwa kuzaliwa ndani ya wiki moja, kwa hiyo nilimchukua mume wangu twende pamoja kwa sababu yeye ni mwanaume, hivyo huenda madaktari wangemsikiliza zaidi,lakini daktari wangu wa uzazi alisema kila kitu kiko sawa, nirudi nyumbani nipumzike."

Chanzo cha picha, Samina Ali
Matatizo ya Samina yalianza rasmi alipojifungua.
"Nilikuwa katika maumivu makali sana, sio maumivu ya uchungu wa kujifungua, nazungumzia maumivu ya kifua na kichwa changu, ambacho kilihisi kana kwamba kingepasuka," aliiambia kipindi cha outlook. "Nilihisi mwili wangu ukizidi kudhoofika na kushindwa kufanya kazi."
"Daktari aliyekuwa akimzalisha mwanangu alikuwa akisimama nyuma ya wauguzi wengine ili asilazimike kujibu maswali yangu. Shinikizo langu la damu lilikuwa linapanda kwa kasi sana. Nilikuwa napoteza fahamu na kurejea katika hali ya fahamu mara kwa mara, hivyo kila uchungu wa kusukuma ulipokuja, muuguzi alilazimika kuniamsha ili nisukume mtoto. Nilikuwa nimechanganyikiwa, na ubongo wangu ulikuwa tayari unaanza kupata viharusi. Maumivu ya kifua baadaye yaligundulika kuwa yalitokana na mshtuko wa moyo."
Samina hakumbuki mengi yaliyofuata anakumbuka zaidi maumivu, pamoja na taswira chache za mtoto wake mchanga.
"Nakumbuka mwanangu alipozaliwa na wauguzi wakamchukua na kumwogesha,Lakini pia nakumbuka nilivyokuwa nimelala kitandani nikiwa nimefumba jicho moja, nikijaribu kumwona vizuri. Dakika ishirini baada ya kujifungua mwanangu, nilipatwa na kifafa kikali . Kilienea mwilini mwangu kana kwamba nilikuwa nimepewa dawa ya usingizi. Sikuhisi tena maumivu. Hicho ndicho kitu cha mwisho ninachokikumbuka."
Samina na mwanawe Ishmael walihamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Ishmael alikuwa katika wodi ya wazazi akiwa na utapiamlo, huku Samina akiwa katika kitengo cha magonjwa ya mfumo wa neva, akiwa amepoteza fahamu, akiwa na uharibifu mkubwa wa ubongo, na akiendelea kuishi kwa msaada wa mashine.

Chanzo cha picha, Marissa Leshnov for The Washington Post via Getty Images
Baada ya siku tano, Samina ambaye daktari wake wa neva alimwita "msichana wa muujiza" alizinduka kutoka kwenye koma.
Hata hivyo, ingawa aliweza kuwatambua wazazi wake na ndugu zake kutokana na kumbukumbu za zamani, na aliweza kuzungumza lugha yake ya kwanza, Kiurdu, alipata ugumu wa kuzungumza Kiingereza na hakuweza kumkumbuka mume wakewala kukumbuka kwamba alikuwa amejifungua.
"Daktari wangu wa neva alidhani kwamba kukutana na mwanangu kungeweza kunisaidia kuanza kurejesha kumbukumbu zangu,"

Chanzo cha picha, Samina Ali












