Moja kwa moja, Mnyika Mahakamani: Lissu hakuhusika kuchapisha kauli zilizoko kwenye shtaka

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Muhtasari

Moja kwa moja

Elizabeth Kazibure, Rashid Abdallah & Asha Juma & Ambia Hirsi

  1. Mnyika: Haya ni mashtaka ya uongo na kubambikizwa

    Mnyika: Haya ni mashtaka ya uongo na kubambikizwa

    Lissu: Sasa shahidi umeeleza mahakama yote yaliyofanyika mpaka Msajili alipokutana na ujumbe wako, waeleze utekelezaji hayo maazimio ya No Reform No election kwa upande wa Umma ulikuaje.

    Mnyika:Tarehe 23 Machi 2025, tulianza Operesheni katika ukanda wa Nyasa wenye mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Rukwa na mkutano mkubwa wa uzinduzi ulifanyika Mbeya ambapo Mwenyekiti Tundu Lissu ndiye mgeni Rasmi.

    Lissu: Hiyo ziara ya Kanda ya Nyasa iliwahusisha kina nani?

    Mnyika:Ukiondoa Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama

    Lissu:Ziara hiyo ilimalizika lini kwa ukanda wa Nyasa?

    Mnyika: Sina kumbukumbu vizuri lakini ilidumu kuanzia tarehe 23 Machi mpaka tarehe za mwanzo za mwezi Aprili ambapo ilipanga baada ya kumaliza ukanda wa Nyasa Operesheni iende Kusini.

    Lissu: Baada ya mkutano wa tarehe 3 Aprili nini kilitokea?

    Mnyika: Tulipanga kuanza Operesheni ukanda wa kusini katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma

    Lissu: Ilianza tarehe ngapi?

    Mnyika:Ilianza mara baada ya tu ya kumalizika kwa mkutano wa Aprili 3,2025.

    Lissu: Ziara ilihusisha kina nani?

    Mnyika: Ziara ilihusisha mwenyekiti Tundu Lissu na viongozi wakuu wa Chama, Katibu Mkuu sikuwepo

    Lissu: Sasa turudi kwenye hoja za mkutano wa tarehe 3 Aprili, eleza tofauti ya hoja za mkutano tarehe 3 Aprili na katika mikutano hiyo ya Kanda.

    Mnyika: Hakuna tofauti isipokuwa kabla ya hapo. Nilipokea barua au waraka wa watia nia wakiwa na maoni yao wakitaka Chama kubadili msimamo wa No Reforms No Election.

    Lissu: Sasa Shahidi nikurudishe kwenye maneno haya(Msimamo huu uanaashiria uasi………….) wewe unafahamu vipi haya maneno?

    Mnyika: Ufahamu wangu nami naona ni maneno ya kisiasa, umma uweze kuona uchaguzi una uozo mkubwa, unanuka.

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji kama baada ya huo mkutano wa tarehe 3 Aprili mwaka jana mlichukua hatua yoyote ya kujulisha Jeshi la Polisi juu ya maneno haya?

    Mnyika:Hapana sijachukua hatua yoyote

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji maelekezo yote uliyotoa kwa wanachama wako kuhusu kutoa taarifa ya mkutano huu.

    Mnyika:Sikutoa maelekezo yoyote juu ya maneno yaliyozungumzwa kwenye mkutano.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hatua zilizochukuliwa na jeshi la Polisi juu ya kutokuoa taarifa juu ya maneno yaliyozungumzwa kwenye mkutano.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la polisi kwa waandishi kutokupeleka taarifa za Jeshi la Polisi kuhusu huo mkutano.

    Mnyika: Sina taarifa zozote kwa waandishi kutokupeleka taarifa hiyo Jeshi Polisi

    Lissu: Kuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waandishi waliochapisha na kusambaza mkutano huo?

    Mnyika: Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhusiana na madai ya kuchapisha na kusambaza mkutano huo

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako uwepo wa mtu mwingine yoyote aliyeshtakiwa kuhusiana na ushiriki wake au kupanga kwake au kueneza taarifa zilizotokana na mkutano huo.

    Mnyika: Hakuna mtu yeyote aliyeshtakiwa kuhusu kushiriki kwake au kupanga kwake au kuchapisha taarifa zilizotokana na mkutano huo

    Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya mimi kukamatwa.

    Mnyika: Siku ileile ya tarehe 9 Aprili 2025 uliyokamatwa kulisainiwa nyaraka za kufunguliwa kwa kesi ya madai dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama na Bodi ya Wadhamini wa Chama ambapo Mahkama iliombwa kutoa amri ya zuio juu ya shughuli za chama na matumizi ya mali za chama mazuio ambayo yalikuja kutolewa na Mahakma tarehe 10 Juni 2025 kupitia kesi namba 8323 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa Said Issa Mohamed na wenzake.

    Lissu: Kitu gani kilitokea?

    Mnyika: Wakati huohuo msajili wa Vyama vya siasa alituandikia barua ya kutakiwa kujieleza Juu ya Uhalali wa Katibu Mkuu na wajumbe wa kuteuliwa walioidhinishwa tarehe 22, Januari 2025 na baada ya majibizano ya barua tarehe 15 Mei ameandika barua kwa umma wa kutengua nafasi ya katibu Mkuu na wajumbe wa kuteuliwa na Baraza Kuu.

    Tarehe 27 Mei 2025 akatuandikia barua nyingine na kutoa taarifa kwa umma ya kuzuia ruzuku ya Chama kwa kile alichokieleza kuwa Chama hakina Katibu Mkuu ki halali

    Lissu: Kitu gani kingine kilitokea?

    Mnyika:Tarehe 12 Aprili 2025 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakatoa kauli kwamba Chadema haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 na uchaguzi wa marudio mpaka uchaguzi wa 2030 kwa kile walichodai kuwa Katibu Mkuu hajasaini fomu za maadili ya uchaguzi.

    Lissu: Sasa shahidi waeleze waheshimiwa majaji hatua nyingine zozote zilizochukuliwa dhidi ya chama na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa kuhusiana na mkutano huu wa Aprili 3.

    Mnyika: Ofisi ya Msajili ilituandikia barua

    Lissu: Barua iliandikwa na nani?

    Mnyika: Barua iliandikwa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama kwenye barua iliandikwa kwamba kauli ya Mwenyekiti ni ya kihaini.

    Mnyika: Hakukua na kauli yoyote iliyoandikwa kwamba kauli ya Mwenyekiti ni ya Kihaini

    Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji hatua mlizochukua baada ya kupokea barua hiyo.

    Mnyika: Kwa sababu wakati tunapokea barua hiyo Mwenyekiti alishakamatwa tuliwaandikia kuwa jambo hilo tayari linashugjulikiwa na mamlaka nyingine.

    Lissu: Sasa shahidi nimekuuliza mara mbili mara tatu na mara zote umesema haya mashtaka ya uongo na kubambikizwa hii una maana gani?

    Mnyika: Kwa sababu unatuhumiwa kuandaa mkutano ambao hujauandaa, unatuhumiwa kupanga njama peke yako wakati yalikua maamuzi halali ya chama, unatuhumiwa kuchapisha maneno ambayo hujayachapisha, unatuhumiwa kufanya siasa halali, unatuhumiwa kwa kuhamasisha watanzania kutumia mamlaka yao kudai uchaguzi huru na haki na halali dhidi ya wanaoasi na kuhaini na kuchagua viongozi wanaowataka.

    Lissu: Tarehe 16 Aprili 2018 aliuawa Mwanachuo Akwelina Akwilini Kwa risasi katika tukio hilo ambalo polisi walishambulia kwa risasi na wengine kujeruhiwa na kubambikiwa kesi mimi na viongozi wengine wa Chdema kwamba tulifanya mkusanyiko usio halali, tulifanya ghasia na tumesababisha kifo cha Akwelina Akwilini.

    Tarehe 10 Machi 2020, tulishtakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali na tukahukumiwa kifungo cha miezi mitano jela au faini shilingi milioni 350, tukaenda gerezani kuanza kutumikia kifungo, siku chache baadaye Watanzania wakatutoa kupitia michango, tulilipa faini na tukakata rufaa, mwezi Juni mwaka 2021 Mahakama Kuu chini ya Jaji Mgeta ikatukuta kuwa hatukuwa na hatia, ikatufutia hukumu hiyo kati ya mambo ambayo Jaji aliyasema kwa uzito mkubwa sana ni juu ya uhuru wa kisiasa na mpaka leo hatujawahi kurudishiwa hizo pesa.

    Lissu:Ulisema mlishtakiwa wewe na Viongozi wenzako 8 hao wenzako ni kina nani?

    Mnyika: Mshtakiwa namba moja alikua, Freeman Mbowe, aliyekuwa Katibu Mkuu Vicent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, aliyekuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti Ester Matiku, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Peter Msigwa, na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu John Heche.

    Lissu: Kwa matukio yote haya ambayo umeyaeleza, waeleze Waheshimiwa majaji kama yana uhusiano na kesi hii.

    Mnyika: Yana uhusiano kwa sababu hii kesi ni mwendelezo wa kuwabambikia viongozi wa chadema kesi za uongo na mbinu za kukwamisha mabadiliko, ni matumizi yasiyo ya haki ya njia za kimahakama na kisheria dhidi ya wapinzani na CCM dhidi ya Chadema na Viongozi wake.

    Lissu: Shahidi kuna kitu sijakuuliza, naomba uwaeleze waheshimiwa majaji umenifahmu kwa miaka mingapi?

    Mnyika: Nimekufahamu kwa miaka 23 kabla ya kukusoma.

    Lissu: Huyu mtu unayesema umemfahamu kwa miaka 23 ni mtu wa aina gani?

    Mnyika:Ni mtetezi wa Haki, mtaka mabadiliko, mwenye msimamo wa kusimamia ukweli kwa hiyo haya mashtaka ni ya uongo na hayakuelezei ulivyo na ninaamini ni gharama unazolipia.

    Mnyika amemaliza kutoa ushahidi, ni muda wa mapumziko.

  2. Mnyika aelezea CHADEMA ilivyonadi kauli ya ''No Reforms No Election''

    Lissu: Nini kikafuata

    Mnyika: Mwenyekiti Mpya Lissu alianza ziara na viongozi wengine nakumbuka tulikuna na sheikh Ponda Issa Ponda, kwa asasi za kiraia tulikutana na kituo cha demokrasia, TLS pia alikutana mzee Jaji Warioba.

    Kwa upande wa waandishi wa habari mwenyekiti alifanya mkutano na waandishi wa habari kuwajuza msimamo wa chama kuhusu ''No Reforms No Election''. Mnamo Machi moja alifanya mkutano na wahariri ofisi kuu za chama

    Lissu: Na kuhusu Jumuiya ya kimataifa ilikuwaje?

    Mnyika: Alitembelea balozi mbalimbali ukiwemo ubalozi wa Marekani Na kwa upande wa wadau wengine tulipokea wito wa Jaji mutungi kwenda kueleza msimamo ulitolewa na chama kupitia kwa mwenyekiti kuhusu ''No Reforms No Election.''

    Lissu: Ofisi zake ziko wapi

    Mnyika: Ziko Dar es Salaam karibu na shule ya msingi Bunge ambayo pia ni karibu na Ikulu.

    Lissu: Nini kikatokea

    Mnyika: Alituuliza juu ya kampeni hiyo na kama inaendana na sheria na baada ya kumueleza juu ya mkutano wetu na maazimio yetu ya Bagamoyo akasema haoni shida kisheria na baadaye akaja kutoa kauli akiwa Dodoma kwamba No Reforms No Election ni kauli ya kisiasa na haikiuki sheria na hij ilikuwa ni aprili 10 2025.

    Lissu: Tubakie kwenye hicho kikao cha msajili na chama. Tarehe 17 Machi nani mwingine alihudhuria hicho kikao

    Mnyika: Msajili alikuwa na maafisa wa ofisi yake Sisti Nyahoza

    Lissu: Sio Shosti Nyahoza nimesikia vibaya

    Mnyika: Hapana ni Sisti Nyahoza

    Lissu: Umeeleza Mahakama mpaka msajili alivyokutana na delegation yako. Utekelezaji kwa upande wa umma ulikuwaje

    Mnyika: Tulipanga mikutako ya hadhara na kanda ya nyasa ndio ilikuwa ya kwanza Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Rukwa na mkutano mkubwa ulifanyika mbeya tarehe 23 mwezi Machi 2025 na huo ndio ulikuwa mkutano wa uzinduzi operesheni na Mwenyekiti Lissu ndio alifungua mkutano huu

    Lissu: waeleze Majaji hiyo ziara ya Nyasa iliwahusisha akina nani.

    Mnyika: Huo mkutano ulikuwa na viongozi wengine waandamizi wa chama na ilidumu mpaka wiki ya kwanza ya mwezi Aprili Sekretarieti ilipopanga kikao cha watia nia Dar es salaam na kwamba baada ya kumaliza Nyasa tutaelekea kusini

    Lissu: Ulishaileza mahakama juu ya ushiriki wako kwenye maandalizi ya mkutano wea tarehe tatu aprili sasa nini kilitokea

    Mnyika: Tulipanga kuendelea na operesheni kanda ya kusuni na misafara ikaanza kuondoka ya maandalizi na mikutano.

    Soma zaidi:

  3. Mnyika kwa Lissu: Vikao vya chama viliongozwa na Mbowe

    John Mnyika ameiambia Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam kwamba vikao vyote vya kamati kuu viliongozwa na mwenyekiti wa wakati huo wa CHADEMA Freeman Mbowe.

    Lissu: baada ya hapo nini kilifiata

    Mnyika: Ulifanyika uchaguzi ndani ya chama na ulikwenda hadi tarehe 22 na uliwezesha kukupatikana kwa viuongozi wapya kwa nafasi mbali mbali

    Lissu: nini kimaendelea

    Mnyika: Mkutano mkuu ulikubaliana utekelezaji wake ufanyike haraka

    Lissu: Baada ya vikao vyote hivyo vya chama kukamilika kitu gani kilitoka kufuatis azimio la no reforms no election

    Mnyika: Katibu Mkuu aliitisha vikao mfululizo vilivyifanyika Bagamoyo kuanzia tarehe 31 Januari hadi tarehe nne mwezi wa pili ili kupanga utekelezaji wa azimio hilo la No Reforms No Election.

    Lissu: waeleze Majaji mpango mliozungumziakwenye vikao hivyo

    Mnyika: Kutoa elimu kwa umma na kuwaunganisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

    Pili tulipitisha mpango wa kukutana na wadau wengine nchini kama asasi za kiraia viongozi wa dini sekta binafsi na wadau wengine muhimu.

    Pia tuliweka mpango wa kuzunguka kwenye vyombo vya habari na kukutana na wahariri. Pia tulipitisha mpango wa kushawishi jumuiya za kimataifa na kikanda nje ya nchi na ndani ya nchi.

    Pia tulipanga kukutana na viongozi wetu wote ndani ya chama na watu mashuhuru kwa jamiii na sekretarieti ikapewa jukumu la kutafakari njia nyingine za amani na kidemokrasia za kukamilisha azma hiyo ya No Reforms No Election.

  4. Lissu kwa Mnyika: "Nani aliitisha Kikao cha Kamati Kuu?"

    Lissu: Nini kikafuatia?

    Mnyika: Tuliita kikao cha Kamati Kuu mwezi wa 12, tarehe mbili na tatu, kikao cha dharura cha Kamati Kuu kwa ajili ya kupokea taarifa na kutathmini juu ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi Novemba.

    Lissu: Hiki kikao cha Kamati Kuu aliitisha nani?

    Mnyika: Hiki kikao niliitisha mimi kwa kushauriana na mwenyekiti wa chama wakati huo, Freeman Mbowe.

    Lissu: Kwenye kikao cha Kamati Kuu nini kilitokea?

    Mnyika: Tulipokea taarifa na kujadili kisha kikao kilitoa maazimio kumi. Kwa uchache ni kwanza, kikao kiliazimia kwamba kwa yaliyotokea Novemba 27 hakukuwa na uchaguzi huru wala halali wala wa haki wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji.

    Pili, hakuna tena uwezekano kwa mazingira yaliyopo ya kikatiba na kisheria wa kuwa na uchaguzi huru na wa haki Tanzania.

    Tatu, chama kiwaunganishe Watanzania kutaka mabadiliko na marekebisho ya kikatiba na kisheria kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025, na kwamba bila mabadiliko hakuna uchaguzi, "No Reforms No Election."

    Lissu: Sasa nini kitafuata baada ya azimio hilo?

    Mnyika: Tarehe 10/12/2024 tuliitisha mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama, Mikocheni, ambapo mwenyekiti wa wakati huo, Mbowe, alitangaza maazimio hayo kwa umma.

    Lissu: Baada ya Mwenyekiti Mbowe kutangaza hayo maazimio, kitu gani kilitokea?

    Mnyika: Chama kiliingia kwenye mkutano mkuu wa chama kupokea taarifa na kufanya uchaguzi mkuu ndani ya chama, ambapo tarehe 20/1/2025 tulipeleka taarifa ya Kamati Kuu kwa Baraza Kuu la chama iliyopendekeza, pamoja na mambo mengine, maazimio yale kumi ikiwemo la "No Reforms No Election."

    Lissu: Kwanini mlipeleka hayo maazimio?

    Mnyika: Ili yawe maazimio ya Baraza Kuu na sio Kamati Kuu tena.

    Mnyika: Ili yawe maazimio ya Baraza Kuu, na Baraza Kuu la tarehe 20 liliridhia mapendekezo na maombi hayo.

    Lissu: Sasa nini kikafuata baada ya aizimio hilo

    Mnyika: 10/12/2024 tuliitisha mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama Mikocheni ambapo mwenye kiti wa wakati huo Mbowe aliyatangaza maazimio hayo kwa umma

    Lissu: Baada ya mwenyekiti mbowe kutangaza hayo maazimio kitu gani kilitokea

    Mnyika: Chama kiliingia kwenye mktano mkuu wa chama kupokea taarifa na kufanya uchaguzi mkuu ndani ya chama ambapo tarehe 20/1/2025 tulipelekea taarifa ya kammati kuu kwa baraza kuu la chama iliyopendekeza. Pamoja na mambo mengine maazimio yale kumi ikiwemo la No Reforms No Election.

    Lissu: Kwani mlipeleka hayo maazimio

    Mnyika: ili yawe maazimio ya baraza kuu na sio kamati kuu tena Myika lili yawe maazimio ya baraza kuu na baraza kuu la tarehe 20 liliridhia mapendekezo na maombi hayo.

    Maelezo zaidi:

  5. Mnyika Mahakamani: Lissu hakuhusika kuchapisha kauli zilizoko kwenye shtaka

    Mnyika

    Chanzo cha picha, CHADEMA

    Jaji: Tuendelee.

    Shahidi anakumbushwa alipoishia juma lililopita na kukumbushwa kuwa kiapo chake kinaendelea.

    Lissu: Shahidi, kwema?

    Mnyika: Salama kabisa, kaka.

    Lissu: Haya, tuendelee.

    Mnyika: Ninachokumbuka ni pamoja na utaratibu wa mfumo mzima wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na mgawanyo wa majimbo, population quota, Tume kuwa na watumishi wake huru badala ya wakurugenzi na watumishi wengine wa umma, na kuweza kupinga matokeo ya urais mahakamani. Baadaye mwenyekiti akaeleza namna ambavyo kutokuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki kulivyopelekea yote hayo.

    Lissu: Sasa shahidi, shtaka linalonikabili mimi linasema mimi ndiye niliyechapisha hiyo hotuba kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV. Wewe unasemaje?

    Mnyika: Hilo shtaka litakuwa la uongo kwangu mimi, kwa sababu mwenyekiti hakuhusika kwa namna yoyote na masuala yanayohusu waandishi wa habari wala taarifa zao.

    Lissu: Sasa shahidi, haya maneno ya "kukinukisha kweli kweli", waeleze majaji yalichapishwa na nani.

    Mnyika: Binafsi sielewi ni nani aliyechapisha hayo maneno. Binafsi sikuwa nimefahamu, ila kama mtendaji mkuu wa chama, baada ya kusikia kuna kesi mahakamani yenye madai kuwa kuna maneno yalichapishwa na Jambo TV, niliuliza kuhusu hayo maneno. Nikashangazwa kwa sababu mkutano ulikuwa wa zaidi ya saa tatu na si sentensi chache zinazodaiwa kuchapishwa tu.

    Soma pia:

  6. Katika Picha: Matukio ya kabla ya kuanza kwa kesi ya Tundu Lissu

    .
    .
    .
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chadema wamewasili mahakamani wanasubiri kesi
    .
    .
  7. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 31.08.2026.

    Tundu Lissu

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, Leo Mnyika anaendelea kutoa ushahidi wake.

  8. Kutoka Tume ya Nyalali hadi Samia: Mnyika asimulia hotuba ya Lissu

    Lissu

    Lissu: Lengo la kualika waandishi wa habari kwa sehemu hiyo lilikuwa nini?

    Mnyika: Lengo lilikuwa kuwapa nafasi ya kuchukua habari na kuzifikisha kwa umma kuhusu madai yetu ya mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili kuwezesha uchaguzi huru na wa haki chini ya kaulimbiu ya No Reforms, No Election; bila ya mabadiliko hakuna uchaguzi.

    Lissu: Unaposema hotuba ya mwenyekiti ndiyo ilikuwa ndefu, unamaanisha nini?

    Mnyika: Katika muda wa masaa matatu, masaa mawili na zaidi alizungumza mwenyekiti wa chama.

    Lissu: Waeleze majaji hotuba hiyo ndefu ilihusu nini.

    Mnyika: Mwenyekiti alieleza historia ndefu ya madai ya kutaka haki kuanzia kabla na baada ya Tume ya Rais maarufu kama Tume ya Nyalali kati ya mwaka 1991 na 1992. Aliendelea kuzungumzia mabadiliko ya kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na wa haki yaliyokataliwa na serikali ya chama kimoja wakati huo, CCM.

    Lissu: Suala lingine nililolizungumzia?

    Mnyika: Alieleza madhara ya kutofanyika kwa mabadiliko hayo kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995.

    Pia alieleza maoni ya tume nyingine zilizoundwa kushughulikia mambo ya kikatiba wakati wa uchaguzi. Alitaja Tume ya Kisanga, akataja Tume au Kamati ya Bomani, na akaeleza kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba kati ya mwaka 2011 hadi 2014, maarufu kama Tume ya Warioba, na jinsi CCM ilivyotumia wingi wake katika Bunge la Katiba kukwamisha mchakato huo.

    Pia alieleza madhara ya kukosekana kwa mabadiliko hayo kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, uchaguzi wa vijiji na vitongoji wa mwaka 2019, uamuzi wa Chadema kujitoa kwenye uchaguzi baada ya wagombea wengi wa Chadema kuondolewa kwenye uchaguzi, na yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo yeye alikuwa mgombea urais.

    Alieleza baadhi ya wagombea kuenguliwa kwa mapingamizi yasiyokuwa na msingi, na wale waliobaki kufungiwa kampeni. Pia alieleza kuwa siku ya kura mawakala wa Chadema waliondolewa vituoni katika maeneo mengi na kwamba kura ziliingizwa kwenye vituo vya kupigia kura zikiwa zimeshapigwa.

    Pia alieleza kuhusu hatua ambazo chama kilichukua baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 wakati huo mwenyekiti wa chama akiwa Freeman Mbowe, akidai mabadiliko ya kikatiba na tume huru ya uchaguzi. Alisema matokeo yake ni Mbowe kubambikizwa kesi ya ugaidi na kukaa rumande gerezani kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2022.

    Alieleza kuwa baada ya kesi hiyo kufutwa na Mbowe kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu mwaka 2022, ndipo mazungumzo kati ya Chadema na CCM pamoja na serikali yalipoanza.

    Akaeleza kuwa katika mazungumzo hayo upande wa Chadema uliwasilisha kwa mdomo na kwa maandishi mapendekezo ya maeneo ya marekebisho ya kikatiba ili kuwezesha uchaguzi huru na wa haki. Alisema baada ya mwaka mmoja wa mazungumzo, upande wa CCM na serikali ulijibu kwa mdomo kukataa mapendekezo yote ya marekebisho ya Katiba yaliyolenga kuwezesha uchaguzi huru na wa haki, na hatimaye mazungumzo yakavunjika.

    Lissu: Subiri, waeleze waheshimiwa majaji hayo mazungumzo na mapendekezo yalikuwa yanahusu uchaguzi gani?

    Mnyika: Yalikuwa yanahusu uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

    Lissu: Waeleze majaji ushiriki wako katika mazungumzo hayo.

    Mnyika: Mimi nilikuwa miongoni mwa timu iliyokutana na Rais tarehe 22 Mei 2022. Katika kikao hicho, mapendekezo ya namna ya kukwamua na kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya yaliwasilishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe.

    Lissu: Waeleze majaji kulikuwa na nini baadaye?

    Mnyika: Mapendekezo ya hoja nyingine kumi za mazungumzo, mojawapo ikiwa ni marekebisho ya kikatiba na kisheria ya kuwezesha uchaguzi huru na wa haki, yaliwasilishwa na mimi.

    Lissu: Uchaguzi huru wa mwaka gani?

    Mnyika: Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2024. Mapendekezo hayo yalihusu kufanyika kwa marekebisho ya kuwezesha uchaguzi huru na wa haki tuliyoyaita Minimum Reforms.

    Lissu: Baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo, nini kiliendelea?

    Mnyika: Rais aliahidi kwamba mchakato wa mazungumzo utaendelea, na akaahidi kuunda timu ya watu watano ikiongozwa na Abdulrahman Kinana ambaye wakati huo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM. Sisi kwa upande wetu, aliyekuwa mwenyekiti wetu pia aliahidi kuunda timu ya watu watano, na aliunda.

    Lissu: Mazungumzo hayo yaliendelea hadi lini?

    Mnyika: Mazungumzo yaliendelea hadi tulipojibiwa na upande wa pili kwamba marekebisho hayo yasubiri hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Hata yale tuliyoyaita Minimum Reforms, kama kuwa na tume huru ya uchaguzi, matokeo ya urais kupingwa mahakamani, maamuzi ya tume kufanyiwa mapitio, na tume kuwa na watumishi wake huru. Walieleza kuwa mradi yanagusa marekebisho ya Katiba, yasubiri mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

    Nzengeli: Waheshimiwa majaji, muda si rafiki na tumepokea maombi kutoka kwa watu wa usalama. Tunaomba tuishie hapo kutokana na muda.

    Jaji: Mshitakiwa, wewe umechoka?

    Lissu: Ombi linahusu masuala ya kiulinzi, sasa mimi siwezi kufahamu, lakini tukubali tu kwamba saa kumi na moja hii inatosha.

    Jaji: Tunaahirisha hadi siku ya Jumatatu saa tatu asubuhi.

  9. Mnyika Mahakamani: Hotuba ya Lissu ilijikita kwenye mabadiliko ya Katiba

    Lissu

    Lissu: Lengo la kualika waandishi wa habari hiyo sehemu ilikuwa ni nini?

    Mnyika: Lengo ni kuwapa nafasi ya kuchukua habari na kufikisha kwa umma, ambayo inahusu madai yetu ya mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuwezesha uchaguzi huru na wa haki chini ya kauli mbiu ya No Reforms, No Election; bila ya mabadiliko hakuna uchaguzi.

    Lissu: Unaposema hotuba ya mwenyekiti ndiyo ilikuwa ndefu unamaanisha nini?

    Mnyika: Katika muda wa saa tatu, saa mbili na zaidi alizungumza mwenyekiti wa chama.

    Lissu: Waeleze majaji hotuba hiyo ndefu ilihusu nini?

    Mnyika: Mwenyekiti alieleza historia ndefu ya madai ya kutaka haki kuanzia kabla na baada ya Tume ya Rais maarufu kama Tume ya Nyalali kati ya mwaka 1991-92.

    Aliendelea kuongea juu ya mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuwezesha uchaguzi huru na wa haki yaliyokataliwa na serikali ya chama kimoja wakati huo, CCM.

    Lissu: Swala jingine nililolizungumzia?

    Mnyika: Alieleza madhara ya kutofanyika kwa mabadiliko hayo kuanzia mwaka 1995 wakati wa uchaguzi.

    Pia akaeleza maoni ya tume nyingine zilizoundwa kushughulikia mambo ya kikatiba wakati wa uchaguzi. Akataja Tume ya Kisanga, akataja tume au kamati ya Bomani, akaeleza kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba kati ya mwaka 2011 mpaka 2014 maarufu kama Tume ya Warioba, na jinsi CCM ilivyokwamisha mchakato huo na kueleza madhara ya kukosekana kwa mabadiliko hayo kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, uchaguzi wa vijiji na vitongoji mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

  10. Mnyika Mahakamani: Si Lissu aliyesambaza video za mkutano wa watia nia

    Lissu

    Katuga: Mshtakiwa anamtilia maneno shahidi. Amuulize maswali in chief, waheshimiwa majaji. Inatakiwa itoke kwa shahidi.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, sasa hizi objection zinatupotezea muda. Ni leading question na si vinginevyo.

    Katuga: Waheshimiwa majaji, leading question imekuwa provided kwenye kifungu cha 159. Sasa shahidi yeye anatiliwa maneno na hizo ndiyo leading questions.

    Lissu: Sasa swali langu lina-lead namna gani? Mimi nilisoma LLB miaka 32 iliyopita. Mimi si mjuzi, waheshimiwa majaji. Swali langu ni sahihi, tunapotezana muda tu hapa.

    Jaji: Tuendelee.

    Lissu: Ahsante, Mheshimiwa.

    Lissu: Shahidi, inadaiwa kwamba mimi ndiye niliyesambaza video za mkutano huo.

    Mnyika: Hapana, hayo madai ni ya uongo. Tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari na mwanzo wa mkutano nilitangaza mkutano utakuwa na awamu mbili. Awamu ya kwanza waandishi wa habari watahusika, na baadaye vyombo vya habari vitaondoka kuendelea na watia nia wenyewe.

    Lissu: Waeleze majaji hiyo sehemu ya kwanza ambayo waandishi wa habari wangehusika nayo ni ipi.

    Mnyika: Kwa kadiri ya kumbukumbu zangu, zilitolewa hotuba fupi fupi na Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ally Ibrahim; Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika; Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Mzee Said; Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche; na Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu, aliyetoa hotuba ndefu.

    Lissu: Ahsante, waheshimiwa majaji. Ninaomba health break ya dakika tano.

  11. Mahakamani: Mnyika akanusha Lissu kuhusika na mialiko ya waandishi wa habari

    Lissu: Sasa wakati wewe na Sekretarieti yako mnafanya yote haya, mwenyekiti alikuwa wapi?

    Mnyika: Mwenyekiti alikuwa kwenye mikutano ya Kanda ya Nyasa kwenye operesheni ya No Reforms, No Election.

    Lissu: Wafafanulie majaji, Kanda ya Nyasa ndiyo sehemu gani ya nchi hii?

    Mnyika: Waheshimiwa majaji, Kanda ya Nyasa inajumuisha mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Rukwa.

    Lissu: Waeleze majaji hiyo ziara ya mwenyekiti ilitumia muda gani?

    Mnyika: Nakumbuka ilianza tarehe 23 Machi hadi kabla ya tarehe 3 Aprili.

    Lissu: Waeleze majaji, wakati mnafanya maandalizi ya mkutano huo, kama mwenyekiti alishiriki kwa namna yoyote kwenye mkutano huo.

    Wakili wa Serikali: Tuna concern kidogo jinsi shahidi huyu anavyoongozwa. Tunaomba muongozaji akumbushwe kufuata kanuni.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, hili pingamizi ni la kitu gani? Taratibu ipi ambayo nimekiuka? Na kwa sababu haijasemwa, naomba niendelee.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji ni namna gani mwenyekiti alivyoshiriki kwenye maandalizi ya mkutano huo wa tarehe 3 Aprili.

    Mnyika: Mwenyekiti wa chama hakushiriki kwa namna yoyote ile.

    Lissu: Waeleze majaji namna mwenyekiti alivyoshiriki kuwaalika watia nia au waandishi wa habari.

    Mnyika: Mwenyekiti hakushiriki kwa namna yoyote ile.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji waandishi wa habari na vyombo vyao ambavyo unakumbuka vilihudhuria mkutano huo.

    Mnyika: Nakumbuka The Chanzo, Mwanzo TV na Jambo TV.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, naomba nipatiwe Exhibit D16. Shahidi apatiwe Exhibit D16, maelezo ya PW17.

    Lissu: Shahidi, kwenye hicho kielelezo naomba wasomee waheshimiwa majaji huyo shahidi wa Jambo TV alipataje taarifa za mkutano.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, naomba nipatiwe Exhibit D16. Shahidi apatiwe Exhibit D16, maelezo ya PW17.

    Lissu: Shahidi, kwenye hicho kielelezo naomba wasomee waheshimiwa majaji huyo shahidi wa Jambo TV alipataje taarifa za mkutano.

    Mnyika: Anasoma sawa sawa na alivyoelekezwa juu ya PW17, alivyopata taarifa za mkutano huo kutoka kwa mkurugenzi wao, John Marwa.

    Lissu: Endelea.

    Mnyika: Anataja vyombo vingine vya habari.

    Lissu: Hivyo vyombo ulivyovisahau vilikuwepo?

    Katuga: Hii ni kinyume cha taratibu, waheshimiwa majaji. Shahidi anasomeshwa document ya mahakama halafu analazimishwa kusema kama anakumbuka.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, hiyo naiondoa.

    Lissu: Sasa shahidi, baada ya ushahidi huo ambao umeutoa mpaka hapo ulipofikia, hii tuhuma ya kwamba mimi ndiyo nilialika hao waliokuja kwenye huo mkutano, wewe unaionaje?

    Mnyika: Waheshimiwa majaji, hiyo ni tuhuma ya uongo. Ni tuhuma ya kubambikiza tu.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji, wakati mnatuma mwaliko kwa hawa waandishi wa habari, mlitoa maelekezo waje na nini?

    Mnyika: Hakukuwa na maelekezo yoyote waje na kitu gani.

    Lissu: Imetolewa ushahidi kwamba waandishi wa habari wa Jambo TV waliokuja waliagizwa waje na kamera na vitu vingine kama hivyo.

    Ubishani kidogo pande zote, Jaji anasema tuendelee.

    Lissu: Waeleze majaji iwapo kulikuwa na maelekezo juu ya namna ya kutumia vifaa vyao.

    Mnyika: Hakukuwa na maelekezo juu ya namna ya waandishi wa habari kutumia vifaa vyao katika tukio hilo.

    Lissu: Wafafanulie majaji utaratibu uliotumika kurusha matangazo ya huo mkutano.

    Mnyika: Ninachofahamu...

  12. Shahidi John Mnyika anatoa ushahidi wake

    Lissu

    Pande zote mbili ziko tayari kuendelea Lissu anamwita shahidi wake wa pili.

    Mnyika tayari amepanda kizimba cha shahidi anasubiri kiapo kwa mujibu wa imani yake.

    Jaji: Shahidi unaitwa nani

    Mnyika: John John Mnyika

    Jaji: Unafanya shughuli gani

    Mnyika: Katibu mkuu wa Chadema

    Jaji: Dini yako

    Mnyika: Mkristo

    Jaji: Utaapishwa kwa mujibu wa imani yako

    Myika anakula kiapo mbele ya mahakama tayari kutoa ushahidi

    Lissu: Shahidi naomba nikuongeze kwenye kutoa ushahidi wako naomba ujibu pole pole na kwa sauti

    Lissu: Umeshikilia nafasi hii ya katibu mkuu tangu lini?

    Mnyika: Tangu mwaka 2019 Lissu waeleze majaji kabla ya nafasi hiyo ulikuwa na nafasi nyingine ndani ya chama chako.

    Mnyika: Nilikua Mkurugenzi wa vijana taifa tangu mwaka 2003 Nafasi ambayo niliishikilia mpaka mwaka 2011 wakati nashikilia nafasi mwaka 2007 niliteuliwa kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi nilikua nashika nafasi zote mbili ambazo nilizitumikia mwaka 2014

    Na wakati huohuo kati ya mwaka 2009 mpaka mwaka 2011 nilishikilia pia nafasi ya ukurugenzi wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa Chadema Mwaka 2014 niliteuliwa kuwa naibu katibu mkuu chadema taifa hadi 2019 nilipochaguliwa kuwa katibu mkuu Nilikua pia mbunge.

    Lissu: Huko sijakupeleka bado nataka za chama kwanza

    Mnyika: Nilishakuwa mwenyekiti wa chama mkoa wa kinondoni kwa vipindi viwili.

    Lissu: Nafasi nyingine zaidi ya hizo..?

    Myika: Nilipokuwa Mbunge wa ubungo nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wabunge wa Chadema bungeni mwaka 2010 hadi 2015.

    Na nilikuwa Mbunge wa jimbo la kibamba kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2020.

    Lissu: Sasa shahidi nafasi ya katibu mkuu wa Chadema ni nafasi ya aina gani ndani ya chama.

    Mnyika: Chadema inaongozwa kwa misingi ya Chadema na nafasi ya katibu mkuu ni nafasi ya Mtendaji mkuu wa Chama ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretarieti ya chama ambacho ndio chombo kinacho simamia chama hivyo Katibu Mkuu ndiye msimamizi wa rasilimali zote za chama na shughuli zote za chama.

    Lissu: Ukisikia jaji amesema mh ndio unaendelea hahahaha.

    Jaji: Tuendelee.

    Mnyika: Vilevile ndio msimamizi mkuu wa watumishi wote wa makao makuu ya chama na watendaji wake.

    Lissu: Ahsante, sasa shahidi naomba uwaeleze majaji kama chama chako huwa kinafanya mikutano na taratibu za kuandaa hiyo mikutano.

    Mnyika: Chama huwa kinafanya mikutano ya ndani ikiwemo vikao vya kikatiba ikiwemo mikutano ya hadhara kwa upande wa mikutano ya ndani ngazi husika ya kiutendaji ambayo ni sekretarieti inakaa kikao ngazi ya taifa chini ya katibu mkuu, kinafanya maamuzi ya kufanya kikao husika na utaratibu wa maandalizi yake.

    Lissu: Kwa vikao vya ndani kama nimekuelewa kazi ya kuandaa vikao ni kazi ya sekretarieti taifa ya Chama naomba waeleze majaji nani ni wajumbe wa hiyo sekretarieti

    Mnyika: Ni Katibu Mkuu, manaibu katibu wakuu wawili mmoja wa bara mwingine wa Zanzibar wakurugenzi wa kKurugenzi za Chama taifa, wataalamu, makatibu wa sekretarieti na makatibu wa mabaraza ya chama wakiongozwa na baraza la wazee, Baraza la wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).

    Lissu: Hao ndio wajumbe wa sekretarieti ya chama taifa

    Mnyika: Ndio

    Lissu: Katika wajumbe wote uliowataja waeleze majaji kama mwenyekiti wa chama ni sehemu ya sekretarieti ya Chama taifa.

    Mnyika: Mwenyekiti sio sehemu ya sekretarieti taifa Lissu waeleze majaji kama mwenyekiti anashiriki kwenye hivyo vikao vya maandalizi.

    Mwenyekiti huwa hashiriki kwenye hivyo vikao

    Lissu: Leo tuko mahakamani sababu ya kesi ya uhaini inayonikabili mimi. Mimi niliitisha mkutano wa watia nia wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, waeleze majaji kama unaufahamu huo mkutano wa Aprili tatu mwezi wa nne mwaka jana.

    Mnyika: Ninaufahamu huo mkutano sababu uliandaliwa kwa maelekezo yangu na sekretarieti ambayo ninaisimamia na ilifanya maandalizi chini ya usimamizi wangu na nikishiriki mkutano wewe

    Lissu: Waeleze majaji huo mkutano ulikuwa wa hadhara.

    Mnyika:Ulikuwa mkutano wa ndani.

    Lissu: Mkutano ulikuwa na lengo gani?

    Mnyika: Ulikuwa ni mkutano wa ndani wa kutaka kufanyika kwa azimio la kimageuzi ya kikatiba na kisheria na kuwezesha kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki chini ya kauli mbiu ya No reforms no Election ikimaanisha bila mabadiliko hakuna uchaguzi

    Lissu: Huo mkutano uliwahusu wakina nani?

    Mnyika: Mkutano uliwahusu wote waliokuwa na nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 maarufu kama watia nia 2025.

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama kuna watu wengine nje ya hao watia nia mliowashirikisha kwenye mkutano huo

    Mnyika: Tulialika viongozi wakuu wa chama na waandishi wa habari

    Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kusema ulialika viongozi wakuu wa chama mnaaanisha akina nani?

    Mnyika: Mwenyekiti wa chama taifa.

    Tundu Antipas Lissu, Makamo mwenyekiti Bara John Wegesa Heche, Makamo mwenyekiti Zanzibar Siad Mzee Said na viongozi wengine wakuu ambao ni sehemu ya manaibu wake.

    Lissu: Ahsante Katibu mkuu , Shahidi huo mkutano wa ndani ulifanyikia wapi?

    Mnyika: Mkutano ulifanyikia makao makuu ya chama mikocheni mtaa wa daima nyumba namba 31 kwenye ukumbi wa chama wa mikutano

    Lissu: Shahidi umesema vilevile mlialika waandishi wa habari na ni wa vyombo vipi kwa kumbukumbu zako?

    Mnyika: Kazi ya kualika waandishi wa habari ilifanywa na mkurugenzi wa mawasiliano wa Chama Brenda Jonas Rupia na nilielekeza itolewe taarifa kwa umma (Tangazo) ambalo lilitolewa tarehe 27 mwezi Machi ambalo lilialika waandishi wa habari na kuutarifu umma juu ya kikao hiki na ilisainiwa na Brenda Rupia.

  13. Lissu akamilisha ufafanuzi wa ushahidi wake

    Lissu

    Kielelezo cha D14. Detective Amani Michael ndiye afisa wa polisi kati ya hawa wote pekee aliyejaza maelezo kwa usahihi. Kila sehemu kuna saini yake katika kila ukurasa, na mwisho kuna saini ya afisa wa polisi aliyemchukua maelezo na kuyaandika. Huyu tu.

    Lissu: Niliulizwa na wakili wa Serikali, Nzengeli, "Hawa mashahidi wa Jamhuri unawaita wahalifu kwani walishahukumiwa?"

    Waheshimiwa majaji, watu ambao wamepanga kufanya uhalifu wakakamatwa kwa kupanga kufanya uhalifu, wakakiri mbele ya polisi kuwa wanapanga kufanya uhalifu, wakaja mahakamani wakaiambia mahakama, walio panga kufanya uhalifu. Ni ushahidi wangu kwamba hawa ni wahalifu.

    Nzengeli: Kweli ni ushahidi wake, lakini mimi nilimuuliza kati ya wewe na mahakama nani anaweza kusema wale ni wahalifu?

    Lissu: Waheshimiwa majaji, nimetoa ufafanuzi.

    Jaji: Tuendelee.

    Lissu: Naelekea kumaliza, waheshimiwa majaji.

    Kulikuwa na maswali niliyoulizwa juu ya omission na contradiction, na kwenye jibu langu moja wapo ni kwamba hizi omission ndio contradiction zenyewe. Sijui kama kwenye rekodi ipo sahihi.

    Jaji: Kwa swali lipi?

    Lissu: Basi niondoke hapo, waheshimiwa majaji. Kwa karatasi ambazo ninazo, waheshimiwa majaji, nimemaliza.

    Jaji: Na ndio msingi wa re-examination. Huwezi kuuliza na kufafanua kila kitu.

    "Lissu amemaliza kutoa ushahidi"

    Wakati Lissu ameomba mapumziko kidogo kesi iendelee saa nane. Akiwa anarudi kizimba cha mshitakiwa alisema "Uhuruni kunaendaje? Waambie nimewamiss."

  14. Mahakama yamzuia Lissu kutoa ufafanuzi zaidi kwenye Re-examination

    Lissu

    Lissu: Naomba washauri wangu wanisomee swali la mwisho, sikuliandika.

    Nzengeli: Naona utaratibu unakiukwa. Hao anaowaita washauri hawatambuliki na mahakama. Kama hakuandika, aiombe mahakama.

    Jaji: Naomba tuendelee.

    Lissu: Nimeulizwa kwamba nia ya kutenda kosa inathibitishwa na matendo? Nikajibu si kweli. Ufafanuzi wangu ni huu kwenye kesi za uhaini.

    Nzengeli: Swali niliuliza mwenyewe na sikuacha nafasi ya maelezo. Swali lilifungwa, kama atatoa maelezo itabidi turudi kwenye cross-examination.

    Lissu: Hili pingamizi ni la bure. Sasa anayeamua nifafanue ni wakili wa serikali au ni mimi?

    Jaji: Wote tunajua re-examination inajikita kwenye swali lililoulizwa na si zaidi.

    Lissu: Sawa, waheshimiwa majaji. Ufafanuzi wangu ni kwamba si kweli makosa yote nia inathibitishwa kwa matendo. Makosa mengine nia inathibitishwa kwa uchapishaji.

    Jaji: Ndiyo.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, niliulizwa na wakili...

    Katuga: Kwamba hii kesi imeshachunguzwa vilevile na Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Ikauliza mahakama yetu iko huru? Nikajibu iko huru. Pamoja na kwamba mahakama yetu iko huru, hizo taasisi nyingine zina umuhimu wake.

    Katuga: Yaleyale, waheshimiwa majaji, sababu alijibu na wala sikuuliza habari ya umuhimu. Sasa kwa namna hii tutamaliza kesi? Ndiyo maana tukasema hii itakuwa na changamoto zake. Ufafanuzi huu anaoufanya ni kuleta ushahidi mpya na sisi tuko macho, unless aiombe mahakama alete ushahidi mpya.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, huu si ushahidi mpya. Ameniuliza mwenyewe kama mahakama yetu inapangiwa na kama iko huru. Nafafanua wala si ushahidi mpya, waheshimiwa majaji.

    Jaji: Hili suala litatuchukua muda mrefu sana kama hatutafuata taratibu, na hata kwenye re-examination si kila swali. Hebu lisome tena hilo swali vyema.

    Lissu: Ninachotaka kusema ni kwamba mahakama zetu, licha ya kwamba hazipangiwi, hazinyimwi kutazama maamuzi ya taasisi nyingine za kimataifa.

    Katuga: Waheshimiwa majaji, yeye alishajibu iko huru. Hayo ya instruments nyingine mimi sikuuliza. Sasa kuyaleta sasa hivi halikuwa sehemu ya swali langu, mimi sikuuliza kabisa.

    Lissu: Mzigo wa kuthibitisha mashtaka ni wa upande wa waleta mashtaka.

    Jaji: Tuendelee.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, niliulizwa vilevile kwamba kwenye ushahidi wangu nilisema kwamba niliwahi kuwa Rais wa Tanganyika Law Society. Nikasema ni kweli, na nikaulizwa uliposhtakiwa ulikuwa bado Rais wa TLS, na nikaulizwa ulikuwa na kinga. Naomba nifafanue.

    Jaji: Unafafanua nini hapo? Naomba tuendelee.

    Lissu: Niliulizwa njia ya kupinga sheria zinazokinzana na Katiba. Nimesema kuna njia za kimahakama na zisizo za kimahakama, na nikaulizwa hiyo iko kwenye kifungu gani cha Katiba. Nikasema iko kwenye kifungu cha 20, kifungu kidogo cha kwanza.

    Sasa, waheshimiwa majaji, naomba kueleza haya majibu yangu. Hizo njia za kutaka mabadiliko ya sheria, ufafanuzi wangu ni kwamba hizo njia za nje ya mahakama zinatambulika kikatiba na zimethibitishwa hivyo na mahakama.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, nikaulizwa kama namfahamu Ishengoma Ndyanabo. Nikaulizwa alifanya nini, nikasema ninamfahamu na alikwenda mahakamani kupinga uchaguzi. Nikaulizwa kama ninamfahamu Mchungaji Mtikila ambaye aliomba mahakama itambue mgombea binafsi, na alishinda kesi Mahakama ya Afrika na mpaka sasa haijatekelezwa.

    Jaji: Sasa hapo unafafanua nini?

    Lissu: Ni sawa, waheshimiwa majaji.

    Jaji: Tuendelee.

    Lissu: Niliulizwa sana kuhusu kifungu cha 39(2)(d) kuhusu maneno yale "or" na mimi nikasema maneno haya yanafana. Wakili wa serikali alikuwa anasema maneno haya hayafanani. Ninaomba nifafanue hili, waheshimiwa majaji. "An act" or "did" ni same thing, maana yake ni matendo, na nilivyosema yanafanana nilikuwa na maana hiyo.

    Katuga: Sikwenda kwenye tafsiri na hakuna sehemu nilimuuliza tafsiri. Na hii tafsiri ameipata wapi? Wakati kwenye cross-examination hakukuwa na hilo swali, na tukasomeshana kisheria.

    Lissu: Waheshimiwa majaji, naomba mahakama itusomee rekodi ya hiki wakili wa serikali anachokisema.

    Jaji: Anasoma kile mahakama ilichokiandika, anasoma kwa Kiingereza.

    Lissu: Naendelea, waheshimiwa majaji. Niliulizwa kama ninafahamu mihimili mitatu na nikamwambia niitaje, na nikaulizwa kazi zake nikazitaja. Niliulizwa juu ya kazi za Bunge, nikasema kutunga sheria. Nikaulizwa kwa habari ya serikali, nikasema kusimamia sheria.

    Niliposema kazi ya Bunge ni kutunga sheria, sikuwa na maana kwamba hiyo ndiyo kazi pekee ya Bunge. Nikasema kazi nyingine ni kuisimamia serikali.

    Waheshimiwa majaji, kulikuwa na ushahidi wa mashahidi wa serikali ambao hawakuja kutoa ushahidi juu ya namna nilivyokamatwa, na nikasema uhalali wa kukamatwa kwangu ni suala tofauti. Kwa sababu, waheshimiwa majaji, sheria zimeweka utaratibu wa namna ya kukamata. Kama sheria ilifuatwa au la ni suala linalobishaniwa na lilihitaji kujibiwa na upande wa mashtaka.

    Soma Zaidi Hapa:

  15. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba kuhojiwa tena

    G

    Wakili wa Serikali (Katuga): Tunaombi waheshimiwa Majaji, upande wa Jamhuri tunafahamu kuhojiwa tena ni njia moja wapo ya shahidi kutoa ushahidi na ipo kisheria na ila tunaomba kwa mujibu wa sheria shahidi ajikite kwenye yale maswali ya kuhojiwa tena na tunajua mshitakiwa ni wakili na anajiwakilisha mwenyewe ni jinsi gani atajihoji ili kufikia lengo la kutoa ufafanuzi wa majibu yake wakati wa kuhojiwa na upande wa pili, suala ambalo tunaomba Mahakama hii tuulize, shahidi ni mtu ambaye anajiwakilisha mwenyewe sasa kuhojiwa tena itafanyikaje?

    Wakili Katuga: Ajiulize maswali mwenyewe na ajijibu mwenyewe kuna hatari ya kuleta ushahidi mpya kabisa maana lengo la kuhojiwa tena ni kufafanua sasa kujiuliza mwenyewe atakuwa hakimu wa mwenendo wako mwenyewe, sasa zile kanuni zetu zinakinzana na hiki, kama angekuwa na wakili sawa ila wewe mwenyewe ujiulize na ufafanue ili kuepuka mkanganyiko Mahakama inaweza ikamuuliza kwa vile vipande ambavyo inaona vinahitaji ufafanuzi

    Jaji: Maombi yako ni nini?

    Katuga: Tunaomba Mahakama imuelekeze shahidi atoe maelezo kama itahitajika kufanya hivyo kwenye majibu yake yenye maana zaidi ya moja na sio kufungua sababu ya kutoa uwanda wa kutoka nje ya yale ambayo yanayohitaji ufafanuzi. Ni hayo tu waheshimiwa majaji

    Lissu: Waheshimiwa majaji kabla sijajibu naomba wakili mkuu wa serikali mkuu aimbie mahakama kama ameleta pingamizi ili muitolee uamuzi na kama ni ushauri tu naomba yawekeni pembeni ili nifanye kazi ya kuhojiwa tena, kwa hiyo naomba majibu hili ni pingamizi au ni nini?

    Katuga: Waheshimiwa majaji tumeiomba Mahakama irejeee kifungu na itoe mwongozo hakuna sehemu tumesema tunapinga, tumeomba mwongozo.

    Lissu: Kwa kuwa ni mwongozo naomba nijibu hayo maombi ya mwongozo, kuhojiwa tena ni haki ya shahidi aliyekuwa aliyehojiwa na upande wa pili, ndio maana kifungu alichokitaja cha 156 moja shahidi atakuwa wakwanza kutoa ushahidi na kama upande wa pili utamhoji na shahidi huyo akitaka kuhojiwa tena ni haki yake na kama ni haki alipaswa kunyamaza kimya.

    Lissu: Wakili wa serikali mkuu anasema atajiongozaje sababu hana wakili, the fact kwamba shahidi ndiye mshitakiwa na anajiwakilisha mwenyewe (ukweli kwamba shahidi ndiye mshitakiwa na anajiwakilisha mwenyewe) kitakachofanyika ni kurejea maswali yaliyoulizwa na majibu yake na kufafanua kwa hiyo hakuna chochote cha kutolea mwongozo sheria iko wapi, hii inaweza kuwa ni fursa ya kuingiza mambo mapya?

    Lissu; Utaratibu uko wazi kama kutakuwa na mambo mapya watafanya pingamizi kwa hiyo hawapaswi kuwa na hofu ya bure sasa waheshimiwa majaji hamna mwongozo wa kutoa.

    Lissu: Baada ya kusema hayo naomba niendelee.

    Jaji: Sasa hayo uliyosema si ndo muongozo wenyewe

    Lissu: Waheshimiwa majaji kama mtatoa mwongozo kwenye jambo dogo hivi tutafika tumechoka sana ila kama anahitaji kuambiwa awe macho waheshimiwa majaji.

  16. Upande wa Mashtaka wamaliza kumdodosa Lissu

    F

    Jaji Ndunguru: Shahidi unakumbushwa kiapo chako kinaendelea

    Lissu: Sawa sawa

    Wakili Nzengeli (Upande wa serikali): Shahidi unakumbuka jana tulipoishia naomba nikuulize swali moja la mwisho tuachane na wewe

    Lissu: Asante mmening'ang'ania sana

    Wakili wa Serikali- Nzengeli: Ni kweli au si kweli nia ya kutenda kosa inathibitishwa na matendo husika

    Lissu: Sio kweli

    Wakili Nzengeli: Waheshimiwa tulikuwa na hilo tu kwa shahidi huyu tunaomba kusema tumemaliza kwa shahidi huyu

    Upande wa Jamhuri umemaliza kumuuliza maswali Shahidi wa Kwanza wa utetezi, ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo.

    Baada ya kukamilika kwa dodoso hilo, Tundu Lissu anatarajiwa kupewa nafasi ya kufanya majumuisho ya utetezi wake.

    Baada ya majumuisho hayo, mahakama itaendelea na hatua inayofuata ya kusikiliza ushahidi wa shahidi mwingine.

  17. Katika Picha: Matukio ya kabla ya kuanza kwa kesi ya Tundu Lisuu

    d
    Maelezo ya picha, Baadhi ya wanachama wa ngazi ya juu wa Chadema wakisubiri kufuatilia kesi dhidi ya Lissu
    h
    Maelezo ya picha, Ibada ya maombi kabla kesi kuanza
    D
    Maelezo ya picha, Shahidi namba moja anasubiriwa
    h
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chadema wamewasili mahakamani wanasubiri kesi kuanza
  18. Kilichojiri jana Mahakamani

    h

    Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, iliendelea jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, huku upande wa serikali ukiendelea kumuhoji Lissu kuhusu ushahidi alioutoa katika utetezi wake.

    Mawakili wa serikali walimhoji Lissu kuhusu kampeni yake ya “No Reforms, No Election”, wakitaka kujua kama mkutano alioufanya ulihitaji taarifa kwa polisi na kama ulikuwa unahusiana na uchaguzi.

    Lissu alisisitiza kuwa huo ulikuwa mkutano wa ndani na kwamba mikutano ya aina hiyo haihitaji kibali.

    Sehemu nyingine ya maswali ilijikita katika kauli za Lissu kuhusu mahakama.

    Wakili wa serikali Job Mtemba alimuuliza kama kauli kwamba majaji ni CCM na kwamba “mahakamani hapaendeki” ilikuwa na lengo la kupandikiza chuki dhidi ya mfumo wa utoaji haki.

    Lissu alikataa kauli hiyo na akasema alikuwa akizungumzia masuala ya uchaguzi.

    Lissu pia alikiri mbele ya mahakama kwamba uanaharakati na uanasiasa vina mipaka ya kisheria, na kwamba hakuna kinga inayomruhusu mwanaharakati au mwanasiasa kuvunja sheria.

    Hata hivyo, alisisitiza kuwa wananchi wana haki ya kupinga uchaguzi ambao wanaona si huru wala wa haki.

    Maswali mengine yalihusu video inayodaiwa kuwa na maneno yaliyosababisha kufunguliwa kwa kesi hiyo.

    Lissu aliendelea kusisitiza kuwa video hiyo ilipaswa kuwasilishwa mahakamani, akisema mashahidi waliodai kuiona na kuisikia hawawezi kuthibitisha kikamilifu yaliyomo bila kuwepo kwa video yenyewe.

    Katika sehemu nyingine, Lissu alihoji uaminifu wa baadhi ya mashahidi wa polisi na akaeleza kuwa hakuridhishwa na namna alivyokamatwa.

    Alisema baadhi ya malalamiko yake kuhusu kukamatwa na madai ya kushambuliwa hayakushughulikiwa na polisi, huku upande wa serikali ukimhoji kwa nini hakuchukua hatua nyingine za kisheria.

    Maswali ya upande wa serikali yaliendelea hadi mahakama ilipoahirisha mwenendo wa kesi hiyo.

    Leo kesi inatarajiwa kuendelea, Lissu akiendelea kujibu maswali ya dodoso kutoka kwa upande wa Jamhuri.

  19. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu, tarehe 28/08/2026.

  20. Nzengeli ahoji uhalali wa kampeni ya ‘No Reforms, No Election’

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Nzengeli: Ni kweli kwamba wakati unafanya huo mkutano wa kuzuia uchaguzi hukuwa na kibali?

    Lissu: Mikutano ya ndani haihitaji kibali, inahitaji taarifa tu.

    Nzengeli: Hapo hukupi PGO?

    Lissu: Ndiyo.

    Nzengeli: Soma kifungu cha 40(3).

    Lissu: 40(3), aya gani?

    Nzengeli: Wakati natafuta, soma Sheria ya Vyama vya Siasa.

    Lissu: Nisaidie kusoma ili tusipoteze muda.

    Nzengeli: Soma kifungu cha 40(2), aya ya sita.

    Lissu:(Anasoma.)

    Nzengeli: Wewe umekielewaje?

    Lissu: Nilichoelewa ni kwamba wakati wa mikutano ya kampeni, wanasiasa watatoa taarifa kwa polisi.

    Nzengeli: Ni kweli au si kweli mkutano huo ulikuwa unazungumzia mambo ya uchaguzi?

    Lissu: Haukuwa mkutano wa kampeni, na uchaguzi ulikuwa bado miezi sita mbele.

    Nzengeli: Waheshimiwa majaji, ninaomba nimpe Sheria ya Vyama vya Siasa, kifungu cha 23.

    Lissu: Nisomee.

    Nzengeli:(Anasoma.)

    Lissu: Ahsante, uliza swali.

    Nzengeli: Je, kwa kifungu hiki ulipaswa kupeleka taarifa polisi?

    Lissu: Hapana, si kweli, kwa sababu ulikuwa mkutano wa wazi na ulikuwa mkutano wa ndani.

    Nzengeli: Shahidi, elewa swali.

    Lissu: Mikutano ya ndani, dada yangu, haihitaji notification.

    Lissu: Next.

    Nzengeli: Ni kweli au si kweli huo mkutano unaouita wa ndani ulikuwa na waandishi wa habari?

    Lissu: Ni kweli.

    Nzengeli: Ambao ulikuwa mubashara na kila mtu aliuona?

    Lissu: Ndiyo, ni mkutano wa ndani.

    Nzengeli: Una kifungu chochote kinachokupa ruhusa ya kufanya mkutano wa ndani?

    Lissu: Kifungu hicho hicho, kwa sababu hakuna mkutano unaohitaji ruhusa bali taarifa tu. Next.

    Nzengeli: Wewe usinipangie.

    Nzengeli: Je, maneno yaliyoko kwenye hati yako ya mashtaka unakiri uliyaongea?

    Lissu: Nimesema sijatangaza maneno ya uhaini mbele ya waandishi wa habari.

    Nzengeli: Uliyaongea au hukuyazungumza? Naomba uwaangalie majaji.

    Lissu: Nimeshitakiwa kwa kuchapisha maneno yanayodaiwa kuwa ya uhaini kwa zaidi ya saa tatu.

    Nzengeli: Uliyaongea au hukuyazungumza?

    Lissu: Nimeongea kwa zaidi ya saa tatu.

    Nzengeli: Je, ni kweli video ni kifaa tu kinachotumika kuchapisha?

    Lissu: Hiyo inahitaji wataalamu.

    Nzengeli: Kati yako na mahakama, nani anaweza kusema nani ni mhalifu?

    Lissu: Mahakama ndiyo inaweza kusema mtu huyu ni mhalifu.

    Nzengeli: Na ni kweli kwamba hujaleta namba za kesi za hao mashahidi wote ambao unasema ni wahalifu?

    Lissu: Mapolisi si walifuta?

    Nzengeli: Tuhuma ni shtaka au si shtaka?

    Lissu: Tuhuma si shtaka.

    Nzengeli: Shahidi, nimekusikia ukilalamika kuhusu mambo ya kukamatwa. Uliyapeleka hayo malalamiko mahakamani?

    Lissu: Niliyapeleka na hakimu wa mahakama niliyemkabidhi alikataa. Ulitaka nifanyaje wakati niko gerezani?

    Nzengeli: Unakubali kwamba sheria zote zilizotungwa na Bunge zinasimamiwa na Serikali?

    Lissu: Sheria ya uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi, si Serikali.

    Nzengeli: Kwa hiyo sheria ya uchaguzi ni sheria kama sheria nyingine?

    Lissu: Ni sheria.

    Nzengeli: Ni kweli kwamba kuna tofauti kati ya kupinga uchaguzi na kuzuia uchaguzi?

    Lissu: Waheshimiwa majaji, sisi tulitaka kupinga uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike. Shughuli zote za uchaguzi, majimbo yasitangazwe, wagombea wasitangazwe, kwa ujumla kila kitu kisimame.

    Lissu: Utaratibu wetu wa saa kumi na moja umekuwa suspended.

    Jaji: Ngoja tuulize, tulikuwa tunajua anamalizia.

    Nzengeli: Kwa maelezo ya mshtakiwa, ni kweli amechoka na kibinadamu. Tunaomba tuahirishe.

    Lissu: Kesho nayo ni siku.

    Jaji: Tunaahirisha shauri mpaka kesho saa tatu asubuhi.