Mnyika: Haya ni mashtaka ya uongo na kubambikizwa

Lissu: Sasa shahidi umeeleza mahakama yote yaliyofanyika mpaka Msajili alipokutana na ujumbe wako, waeleze utekelezaji hayo maazimio ya No Reform No election kwa upande wa Umma ulikuaje.
Mnyika:Tarehe 23 Machi 2025, tulianza Operesheni katika ukanda wa Nyasa wenye mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Rukwa na mkutano mkubwa wa uzinduzi ulifanyika Mbeya ambapo Mwenyekiti Tundu Lissu ndiye mgeni Rasmi.
Lissu: Hiyo ziara ya Kanda ya Nyasa iliwahusisha kina nani?
Mnyika:Ukiondoa Mwenyekiti Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama
Lissu:Ziara hiyo ilimalizika lini kwa ukanda wa Nyasa?
Mnyika: Sina kumbukumbu vizuri lakini ilidumu kuanzia tarehe 23 Machi mpaka tarehe za mwanzo za mwezi Aprili ambapo ilipanga baada ya kumaliza ukanda wa Nyasa Operesheni iende Kusini.
Lissu: Baada ya mkutano wa tarehe 3 Aprili nini kilitokea?
Mnyika: Tulipanga kuanza Operesheni ukanda wa kusini katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma
Lissu: Ilianza tarehe ngapi?
Mnyika:Ilianza mara baada ya tu ya kumalizika kwa mkutano wa Aprili 3,2025.
Lissu: Ziara ilihusisha kina nani?
Mnyika: Ziara ilihusisha mwenyekiti Tundu Lissu na viongozi wakuu wa Chama, Katibu Mkuu sikuwepo
Lissu: Sasa turudi kwenye hoja za mkutano wa tarehe 3 Aprili, eleza tofauti ya hoja za mkutano tarehe 3 Aprili na katika mikutano hiyo ya Kanda.
Mnyika: Hakuna tofauti isipokuwa kabla ya hapo. Nilipokea barua au waraka wa watia nia wakiwa na maoni yao wakitaka Chama kubadili msimamo wa No Reforms No Election.
Lissu: Sasa Shahidi nikurudishe kwenye maneno haya(Msimamo huu uanaashiria uasi………….) wewe unafahamu vipi haya maneno?
Mnyika: Ufahamu wangu nami naona ni maneno ya kisiasa, umma uweze kuona uchaguzi una uozo mkubwa, unanuka.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji kama baada ya huo mkutano wa tarehe 3 Aprili mwaka jana mlichukua hatua yoyote ya kujulisha Jeshi la Polisi juu ya maneno haya?
Mnyika:Hapana sijachukua hatua yoyote
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji maelekezo yote uliyotoa kwa wanachama wako kuhusu kutoa taarifa ya mkutano huu.
Mnyika:Sikutoa maelekezo yoyote juu ya maneno yaliyozungumzwa kwenye mkutano.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hatua zilizochukuliwa na jeshi la Polisi juu ya kutokuoa taarifa juu ya maneno yaliyozungumzwa kwenye mkutano.
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la polisi kwa waandishi kutokupeleka taarifa za Jeshi la Polisi kuhusu huo mkutano.
Mnyika: Sina taarifa zozote kwa waandishi kutokupeleka taarifa hiyo Jeshi Polisi
Lissu: Kuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waandishi waliochapisha na kusambaza mkutano huo?
Mnyika: Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhusiana na madai ya kuchapisha na kusambaza mkutano huo
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako uwepo wa mtu mwingine yoyote aliyeshtakiwa kuhusiana na ushiriki wake au kupanga kwake au kueneza taarifa zilizotokana na mkutano huo.
Mnyika: Hakuna mtu yeyote aliyeshtakiwa kuhusu kushiriki kwake au kupanga kwake au kuchapisha taarifa zilizotokana na mkutano huo
Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya mimi kukamatwa.
Mnyika: Siku ileile ya tarehe 9 Aprili 2025 uliyokamatwa kulisainiwa nyaraka za kufunguliwa kwa kesi ya madai dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama na Bodi ya Wadhamini wa Chama ambapo Mahkama iliombwa kutoa amri ya zuio juu ya shughuli za chama na matumizi ya mali za chama mazuio ambayo yalikuja kutolewa na Mahakma tarehe 10 Juni 2025 kupitia kesi namba 8323 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa Said Issa Mohamed na wenzake.
Lissu: Kitu gani kilitokea?
Mnyika: Wakati huohuo msajili wa Vyama vya siasa alituandikia barua ya kutakiwa kujieleza Juu ya Uhalali wa Katibu Mkuu na wajumbe wa kuteuliwa walioidhinishwa tarehe 22, Januari 2025 na baada ya majibizano ya barua tarehe 15 Mei ameandika barua kwa umma wa kutengua nafasi ya katibu Mkuu na wajumbe wa kuteuliwa na Baraza Kuu.
Tarehe 27 Mei 2025 akatuandikia barua nyingine na kutoa taarifa kwa umma ya kuzuia ruzuku ya Chama kwa kile alichokieleza kuwa Chama hakina Katibu Mkuu ki halali
Lissu: Kitu gani kingine kilitokea?
Mnyika:Tarehe 12 Aprili 2025 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakatoa kauli kwamba Chadema haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 na uchaguzi wa marudio mpaka uchaguzi wa 2030 kwa kile walichodai kuwa Katibu Mkuu hajasaini fomu za maadili ya uchaguzi.
Lissu: Sasa shahidi waeleze waheshimiwa majaji hatua nyingine zozote zilizochukuliwa dhidi ya chama na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa kuhusiana na mkutano huu wa Aprili 3.
Mnyika: Ofisi ya Msajili ilituandikia barua
Lissu: Barua iliandikwa na nani?
Mnyika: Barua iliandikwa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama kwenye barua iliandikwa kwamba kauli ya Mwenyekiti ni ya kihaini.
Mnyika: Hakukua na kauli yoyote iliyoandikwa kwamba kauli ya Mwenyekiti ni ya Kihaini
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji hatua mlizochukua baada ya kupokea barua hiyo.
Mnyika: Kwa sababu wakati tunapokea barua hiyo Mwenyekiti alishakamatwa tuliwaandikia kuwa jambo hilo tayari linashugjulikiwa na mamlaka nyingine.
Lissu: Sasa shahidi nimekuuliza mara mbili mara tatu na mara zote umesema haya mashtaka ya uongo na kubambikizwa hii una maana gani?
Mnyika: Kwa sababu unatuhumiwa kuandaa mkutano ambao hujauandaa, unatuhumiwa kupanga njama peke yako wakati yalikua maamuzi halali ya chama, unatuhumiwa kuchapisha maneno ambayo hujayachapisha, unatuhumiwa kufanya siasa halali, unatuhumiwa kwa kuhamasisha watanzania kutumia mamlaka yao kudai uchaguzi huru na haki na halali dhidi ya wanaoasi na kuhaini na kuchagua viongozi wanaowataka.
Lissu: Tarehe 16 Aprili 2018 aliuawa Mwanachuo Akwelina Akwilini Kwa risasi katika tukio hilo ambalo polisi walishambulia kwa risasi na wengine kujeruhiwa na kubambikiwa kesi mimi na viongozi wengine wa Chdema kwamba tulifanya mkusanyiko usio halali, tulifanya ghasia na tumesababisha kifo cha Akwelina Akwilini.
Tarehe 10 Machi 2020, tulishtakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali na tukahukumiwa kifungo cha miezi mitano jela au faini shilingi milioni 350, tukaenda gerezani kuanza kutumikia kifungo, siku chache baadaye Watanzania wakatutoa kupitia michango, tulilipa faini na tukakata rufaa, mwezi Juni mwaka 2021 Mahakama Kuu chini ya Jaji Mgeta ikatukuta kuwa hatukuwa na hatia, ikatufutia hukumu hiyo kati ya mambo ambayo Jaji aliyasema kwa uzito mkubwa sana ni juu ya uhuru wa kisiasa na mpaka leo hatujawahi kurudishiwa hizo pesa.
Lissu:Ulisema mlishtakiwa wewe na Viongozi wenzako 8 hao wenzako ni kina nani?
Mnyika: Mshtakiwa namba moja alikua, Freeman Mbowe, aliyekuwa Katibu Mkuu Vicent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, aliyekuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti Ester Matiku, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Peter Msigwa, na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu John Heche.
Lissu: Kwa matukio yote haya ambayo umeyaeleza, waeleze Waheshimiwa majaji kama yana uhusiano na kesi hii.
Mnyika: Yana uhusiano kwa sababu hii kesi ni mwendelezo wa kuwabambikia viongozi wa chadema kesi za uongo na mbinu za kukwamisha mabadiliko, ni matumizi yasiyo ya haki ya njia za kimahakama na kisheria dhidi ya wapinzani na CCM dhidi ya Chadema na Viongozi wake.
Lissu: Shahidi kuna kitu sijakuuliza, naomba uwaeleze waheshimiwa majaji umenifahmu kwa miaka mingapi?
Mnyika: Nimekufahamu kwa miaka 23 kabla ya kukusoma.
Lissu: Huyu mtu unayesema umemfahamu kwa miaka 23 ni mtu wa aina gani?
Mnyika:Ni mtetezi wa Haki, mtaka mabadiliko, mwenye msimamo wa kusimamia ukweli kwa hiyo haya mashtaka ni ya uongo na hayakuelezei ulivyo na ninaamini ni gharama unazolipia.
Mnyika amemaliza kutoa ushahidi, ni muda wa mapumziko.





















