Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iskander: Kombora hatari zaidi Afrika kwa sasa?
Jeshi la Algeria kwa mara ya kwanza limethibitisha kuwa na makombora ya Iskander yenye nguvu ya hypasoniki, huku likitoa picha za ufyatuaji wa makombora hayo wakati wa mazoezi.
Kombora hilo linadhaniwa kuwa limetumika katika jeshi la nchi hiyo kwa miaka mingi, ingawa ukosefu wa uthibitisho hapo awali unawakilisha mwelekeo wa jeshi la Algeria wa kutotangaza ununuzi wa silaha mpya.
Iskander linachukuliwa kuwa kombora lenye uwezo mkubwa duniani la balestiki na inajulikana kuwa limesafirishwa kwenda Armenia na Algeria pekee kutoka Urusi, huku Korea Kaskazini na Kusini zikirusha makombora yanayofanana ambayo yanadhaniwa ni manufaa ya teknolojia ya Urusi.
Kombora hilo lina kwenda umbali wa kilomita 500 na linalenga shabaha kwa usahihi wa hali ya juu na uwezo wa kubadii mwendo, na uwezo wake wa kusafiri kwa kasi kubwa na hufanya iwe vigumu kulizuia.
Kufichuliwa kwa Iskander kumefuatia kuzuka kwa uhasama wa kiwango cha chini kati ya Jeshi la Morocco na makundi mbalimbali ya waasi.
Kombora la Iskander
Iskander inawakilisha aina ya kisasa zaidi ya kombora la balestiki barani Afrika au ulimwengu wa Kiarabu, na ni mojawapo ya silaha za hadhi ya juu katika miaka ya hivi karibuni kutoka Urusi.
Silaha nyingine za Algeria zinajumuisha mifumo ya makombora ya S-400 ya masafa marefu, mamia ya vifaru vya T-90, magari ya ulinzi wa anga ya Patnsir-SM, nyambizi za mashambulizi za Kilo Class na makombora ya China ya CX-1 - miongoni mwa mengine.
Algeria pia inadhaniwa kusaini mkataba wa ununuzi wa ndege za kivita za Su-57 kutoka Urusi, ingawa kama kawaida kwa nchi kubwa zaidi barani Afrika ununuzi mkubwa wa silaha hautathibitishwa rasmi.
Mkusanyiko wa silaha za Algeria uliongezeka sana baada ya mashambulizi yasiyotarajiwa ya NATO dhidi ya nchi jirani ya Libya mwaka 2011, ambayo ilikuwa imepuuza uboreshaji wa jeshi lake la anga au ulinzi wa anga na ililipa gharama kubwa kwa kufanya hivyo wakati udhaifu huu ulipotumiwa vibaya.
Hii ilisababisha Algeria na Misri kuwekeza sana katika uwezo wao zaidi wa silaha ili kuzuia mashambulizi yoyote ya Magharibi.
Asili ya Kombora la Iskander
Mfumo wa makombora wa 9K720 Iskander unatoka Urusi, ni maendeleo ya kombora lililoanzishwa wakati wa enzi ya mwisho ya Usovieti. Limechukua nafasi ya kombora la zamani la balistiki la Oka na limeingia rasmi katika jeshi la Urusi 2006
Maendeleo rasmi ya kombora hilo, yalianza chini ya amri ya Baraza la Mawaziri la Usovieti Desemba 1988.
Limejengwa kama mfumo wa makombora ya masafa mafupi ya kimkakati yanayoweza kuhamishika ili kukwepa ulinzi wa anga na kushambulia maeneo ya kawaida au ya nyuklia yenye thamani kubwa.