Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Forest wafukuzia kumpata Reijnders
Nottingham Forest wameingia vitani kumsaka Tijjani Reijnders, huku Tottenham wakipanga kuwasajili Savinho na Nicolas Jackson. Wakati huohuo, Real Madrid wameanzisha upya mazungumzo ya kumbakisha Vinicius Jr kwa mkataba mpya, huku Chelsea wakiwa hatua chache tu kukamilisha usajili wa Pep Chavarría.
Nottingham Forest wameweka mezani dau la pauni milioni 55 kumng'oa Tijjani Reijnders kutoka Manchester City, huku kiungo huyo wa Uholanzi akiwa lengo lao kuu katika dirisha hili la usajili. (Mail)
Folarin Balogun afunguliwa mlango wa Tottenham! Mshambuliaji huyo wa Marekani amepelekwa kwa Spurs kupitia mawakala, huku hatma ya nyota huyo wa zamani wa Arsenal katika klabu ya Monaco ikiwa bado haijulikani. (Sun)
Tottenham wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajili wa winga wa Brazil, Savinho, 22. Mbali na hilo, Spurs pia wanawafuatilia mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi, Cody Gakpo, pamoja na kiungo mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Jean-Matteo Bahoya, wakitajwa kwenye orodha ya mastaa wanaotakiwa kutua kaskazini mwa London kuimarisha kikosi chao kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Athletic - subscription required)
Mpango B wa Man City uko tayari! Savinho akitua Tottenham, mabingwa hao wa England watamgeukia Pedro Neto, 26, winga wa Chelsea na timu ya taifa ya Ureno huku mazungumzo ya awali na kambi ya nyota huyo wa Chelsea tayari yakiwa yameanza. (Fabrizio Romano)
Real Madrid wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Vinicius Jr wiki hii, lakini wameweka msimamo mkali wa kutoongeza dau lao kwa winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia anahusishwa na uhamisho wa kwenda Arsenal. (ESPN)
Chelsea wako hatua za mwisho kukamilisha dili la kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania, Pep Chavarría, kutoka Rayo Vallecano. Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari amekubaliana masharti binafsi na klabu hiyo ya Ligi ya Primia. (Athletic - subscription required)
Tottenham wameingia kwenye rada za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Jackson, huku Spurs wakitathmini uwezekano wa kumnasa nyota huyo wa Senegal. Hata hivyo, bado hawajapeleka ofa rasmi mezani, wakati Chelsea wakimthamini mchezaji huyo, 25, kwa dau la pauni milioni 65. (Mail)
Chelsea wameweka macho kwa mlinda mlango wa Porto na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Costa, mwenye umri wa miaka 26, huku wakipanga kumsajili nyota huyo ambaye awali alikuwa akihusishwa na Manchester United. Mkataba wa Costa una kipengele maalum cha kuachiliwa kwa dau la euro milioni 60, (£51m). (Mirror)
Manchester City waanzisha harakati za kumnasa Rulli na wamewasilisha ofa ya kumsajili mlinda lango wa Marseille na timu ya taifa ya Argentina, Gerónimo Rulli, 34. Mazungumzo kati ya klabu hizo mbili tayari yameanza. (Fabrizio Romano)
Hull City waliopanda daraja hivi karibuni wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Tottenham na timu ya taifa ya Israel, Manor Solomon, 27. Hull wanakabiliana na West Ham walioshuka daraja, huku dau la nyota huyo likikadiriwa kuwa karibu pauni milioni 20. (The i Paper)
Manchester United wameanza kumtazama Morgan Gibbs-White kama mrithi anayefaa wa nahodha Bruno Fernandes endapo kiungo huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 31 ataondoka Old Trafford. Nyota huyo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, mwenye miaka 26, amewekwa kwenye orodha ya chaguo za Mashetani Wekundu. (Mail - subscription required)
Manchester United na Chelsea wameingia kwenye mbio za kumsajili beki wa kati wa Bologna na timu ya taifa ya Colombia, Jhon Lucumí, mwenye umri wa miaka 28. Hata hivyo, hawako peke yao kwenye harakati hizo, kwani Juventus na Como za Serie A tayari zimewasilisha ofa kwa ajili ya nyota huyo. (Quotidiano Sportivo - in Italian)
Jadon Sancho ameingia kwenye rada za klabu kadhaa! Winga huyo wa zamani wa Manchester United, mwenye umri wa miaka 26, tayari ana makubaliano ya awali na baadhi ya timu kutoka Ulaya, Saudi Arabia na Mashariki ya Kati, huku nyota huyo wa England akipima chaguo lake kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho. (Sky Sports)