Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Arsenal wamtaka Bruno Guimaraes wa Newcastle

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 28, kutoka Newcastle msimu huu. (Mail)
Tottenham wamekataliwa ofa ya pili kwa kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali, huku Magpies wakitaka takriban pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Mail),
Ombi la hivi punde la Liverpool la pauni milioni 100 kwa winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, limekataliwa na RB Leipzig. (TeamTalks)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wanataka pauni milioni 50 kumnunua beki wa Ufaransa Maxence Lacroix, 26, ambaye anasakwa na Chelsea kote London. (Football Insider
Bournemouth wamejiunga na orodha ya klabu zinazomtaka kiungo wa kati wa Benfica na Colombia Richard Rios, 26. (Sportwitnessi)
Inter Milan wanaweza kumnunua mlinzi wa Chelsea na Muingereza Trevoh Chalobah, 26, ikiwa hawataweza kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Oumar Solet, 26, kutoka Udinese. (Gazzetta dello Sport - In Itali}

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund haitamuuza kiungo wa kati wa Ujerumani anayehitajika Felix Nmecha, 25, kwa chini ya £86m (euro 100m). (Kicker - In Germany)
Wolves wameweka bei ya pauni milioni 15 kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Huge Bueno, 23, huku kukiwa na hamu kutoka Fiorentina. (Football Insider)












