Kombe la Dunia 2026: Afrika Kusini yafuzu raundi ya pili baada ya kuilaza Korea Kaskazini
Chanzo cha picha, Carl Recine/Getty Images
Bao la kipindi cha pili la Thapelo Maseko limeweka historia kwa Afrika Kusini baada ya kufuzu kwa awamu ya muondoano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa mara ya kwanza dhidi ya Korea Kusini dhidi ya Monterrey.
Alama tatu zinaifanya Afrika Kusini kupanda hadi nafasi ya pili kwenye jedwali, nyuma ya Mexico, na kuiacha Korea Kusini kwa matumaini kwamba itamaliza ikiwa moja ya timu zilizo nafasi ya tatu bora.
Afrika Kusini sasa itamenyana na Canada huko Los Angeles siku ya Jumapili .
Polisi wafunga barabara kuu Nairobi wakihofia maandamano
Maelezo ya picha, Polisi waweka vizuizi kuingia katikati ya jiji la Nairobi
Polisi wameweka vizuizi barabarani na katika sehemu nyingi muhimu za kuingia katikati ya jiji la Nairobi ili kudhibiti harakati kabla ya Maandamano ya ukumbusho wa Gen Z .
Matatu na magari ya uchukuzi wa umma yanazuiwa kuingia mjini hatua inayosababisha kukwama kwa wasafiri na usumbufu mkubwa wa trafiki.
Baadhi Wakenya, wakiwemo baadhi ya walionusurika, wanapanga kufanya maandamano nchi nzima na kuwasha mishumaa kuwaenzi mashujaa hao.
Maandamano ya Juni 25, 2024, ambayo yalishuhudia Bunge la Kenya kuvamiwa na waandamanaji, yameonyeshwa kama kiini cha mabadiliko yasiyoweza kufutika katika utetezi wa raia wa taifa hilo.
Vijana wa Kenya maarufu Gen Z, walipinga Mswada wa Fedha uliopendekeza nyongeza ya ushuru kupita kiasi, kushinikiza nidhamu miongoni mwa wanasiasa na hata kuondolewa kwa Rais William Ruto na viongozi wengine.
Miaka miwili baadaye, kumbukumbu za Juni 25 zinaendelea huku familia za takribani watu 19 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga ushuru zikisubiri haki.
Mnamo 2025, Wakenya waliadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa maandamano ya Gen Z, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu wengine 16 kutokana na majeraha ya risasi na majeraha ya yaliyotokana na hatua ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na maandamano hayo.
Kombe la Dunia 2026: Morocco yafuzu kwa hatua ya 32 kwa ushindi wa kusisimua dhidi ya Haiti
Chanzo cha picha, EPA
Achraf Hakimi na Ismail Saïbari walifunga mabao ya kipindi cha kwanza na Soufiane Rahimi na Yassine Jassim waliongeza mabao ya kipindi cha pili na Morocco kupata ushindi mnono wa 4-2 dhidi ya Haiti mapema Alhamisi na kufuzu kutoka Kundi C hadi hatua ya 32 kwenye Kombe la Dunia.
Brazil, ambao walipata nafasi ya kwanza katika kundi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Scotland pia wamefuzu hatua ya 32.
Morocco na Brazil tayari walikuwa karibu sana kufuzu baada ya kila mmoja wao kujisanyia alama nne wakati wa mechi mbili za kwanza, na kila mmoja wao alicheza mechi yake ya raundi ya tatu kwa lengo la kupata kufuzu na kunyakua uongozi.
Wakati huo huo Qatar iliaga Kombe la Dunia la 2026 siku ya Jumatano, kwa kufungwa 1-3 na Bosnia na Herzegovina mjini Seattle, huku Uswizi ikiifunga Canada, moja ya nchi mwenyeji, 2-1 mjini Vancouver, na timu zote mbili zilifuzu kwa hatua ya 32 kutoka Kundi B.
Qatar ilihitimisha ushiriki wake wa pili katika Kombe la Dunia—baada ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2022—ikiwa na pointi moja, nyuma ya Bosnia na Herzegovina (4), ambao nafasi yao ya kufuzu hatua ya timu 32 bora kama mojawapo ya timu nane bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu imeimarika; huku Uswisi (7) ikiongoza kundi hilo mbele ya Canada (4), ambayo ilishika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao dhidi ya Bosnia.
Italia yamkosoa Katibu Mkuu wa NATO baada ya Marekani kutumia kambi za Italia katika vita na Iran
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Bendera ya Muungano wa NATO
Italia ilikosoa matamshi ya Katibu Mkuu wa NATO kuhusiana na jeshi la Marekani kutumia kambi za kijeshi nchini Italia katika vita na Iran.
Akijibu ukosoaji wa Donald Trump kwamba washirika wa NATO hawakuunga mkono Marekani vya kutosha, Mark Rutte aliiambia Fox News kwamba Ulaya imekuwa "jukwaa kwa Marekani kuonyesha na kutumia nguvu."
"Ndege mia tano za Marekani ziliruka kutoka kambi za Marekani nchini Italia ili kusaidia Operesheni Epic Fury.
Kwa hiyo msaada wetu ulikuwa mpana sana," alisema. Bw. Rutte pia alisema wakati wa vita, kati ya wanajeshi 4,000 na 5,000 walisafirishwa na ndege za Kimarekani kutoka kambi za Ulaya.
Lakini Wizara ya Ulinzi ya Italia inasema katika taarifa kwamba matamshi hayo yaliwakilisha "picha ya kupotosha kabisa" kwa sababu hayatofautishi kati ya aina za ndege.
Wizara hiyo ilisisitiza kuwa Italia iliidhinisha tu safari za ndege za "kiufundi, vifaa, na zisizo za kijeshi" za Marekani ndani ya mfumo wa makubaliano yaliyopo na Marekani, na "katika hali ambapo maombi yalifanywa nje ya mfumo huu, kama inavyojulikana, Italia haikutoa idhini."
Serikali ya Italia imesisitiza kuwa haijaidhinisha matumizi ya maeneo yake na vituo vyake kwa misheni ya moja kwa moja ya kijeshi ya Marekani katika vita na Iran, na kwamba jukumu lake lilikuwa tu kwa msaada wa kiufundi na vifaa.
Trump: Iran inapaswa kukubaliana na kila kitu ninachotaka
Chanzo cha picha, Getty Images
Katika taarifa zake za hivi punde, Rais wa Marekani amesema kuwa, ameridhishwa na mchakato wa maelewano kati ya Iran na Marekani.
"Nani angefikiria hili lingetokea? Huu ni wakati wa vita na Iran ina tabia nzuri sana. Wanakubali kila kitu ninachouliza na wanapaswa kufanya. Vinginevyo, tutarudi tu na kufanya kile kinachohitajika," Bw. Trump aliwaambia waandishi wa habari, akizungumzia bei ya mafuta inayokaribia $ 70 kwa pipa.
Katika siku za hivi karibuni, kufuatia mkutano wa timu za mazungumzo za Marekani na Iran nchini Uswizi, ambao ulisuluhishwa na Pakistan, maafisa kutoka nchi zote mbili wametoa kauli kali na zinazokinzana.
Marekani kuiuzia Uturuki injini za ndege za kivita zenye thamani ya mamilioni ya dola
Chanzo cha picha, Lockheed Martin
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, utawala wa Rais wa Marekani Donald
Trump unanuia kusonga mbele na mpango wa kuiuzia Türkiye makumi ya injini za ndege zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dola.
Hatua hiyo, ambayo inafanywa licha ya upinzani kutoka kwa Congress, ni maendeleo makubwa kwa Ankara kabla ya mkutano wa kilele wa NATO mwezi ujao, vyanzo vinne vinavyofahamu suala hilo viliiambia Reuters.
Injini hizi, zinazotengenezwa na General Electric, zitatumia Qa'an, ndege ya kwanza ya kivita ya Türkiye.
Türkiye, kama mwanachama wa NATO, alianza mradi huu mkubwa mwaka wa 2016 ili kujitegemea zaidi ulinzi.
Chanzo kimojawapo kilisema dili hilo litakuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 700 na linatarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.
Kwa picha: Hofu na wasiwasi katika mitaa ya Caracas
Picha zilizopigwa saa chache tbaada ya kutokea kwa tetemeko hilo zinaonyesha wakaazi wakiwa wamekusanyika kwenye mitaa ya mji mkuu wa Venezuela, baada ya nyumba zao kuporomoka na umeme kukatika.
Wengine wanaonekana wakiwakumbatia ndugu na jamaa zao, huku maafisa wa waokoaji wakipekua vifusi kuwatafuta walionaswa.
Mamlaka zinahofia tetemeko hilo limesababisha uharibifu mkubwa, lakini kiwango kamili cha uharibifu bado hakijajulikana.
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, EPA
Chanzo cha picha, Getty Images
Matetemeko makubwa ya ardhi yakumba Venezuela na kuangusha majengo Caracas
Chanzo cha picha, Getty Images
Mji mkuu
wa Venezuela Caracas, umekumbwa na matetemeko mawili makubwa yaliyoachana kwa sekunde
chache.
Tetemeko la kwanza
lilikuwa la ukubwa wa 7.2 lililotokea katika eneo la Montalbán, magharibi
kidogo mwa Caracas, kulingana na shirika la ufuatiliaji wa Utafiti wa Jiolojia
wa Marekani (USGC).
Sekunde
39 baadaye, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.5 lilipiga takriban kilomita 10
ndani ya eneo hilo.
Matetemeko
hayo yametajwa kuwa moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo
ya Amerika Kusini katika karne moja.
Majengo
yaliporomoka na wakaazi kukimbilia barabarani kutafuta usalama wakati
matetemeko ya ardhi yalipotokea.
Rais wa
mpito wa Venezeula Delcy Rodríguez ametangaza hali ya hatari.
Kuna
hofu ya majeruhi na uharibifu mkubwa lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa
kuhusiana na hilo kufikia sasa. Waokoaji wako mbioni kuwatafuta manusura ambao
huenda wamenaswa chini ya vifusi.