Je, ni timu mbili zinazopigania ubingwa Ligi kuu ya England?

Chanzo cha picha, Getty Images
Michezo minne ni kipindi kifupi mno kuzungumzia nani yumo au hayumo kwenye kinyang'anyiro cha ubingwa... sivyo?
Hata hivyo, Arsenal na Manchester City ambazo zimekuwa timu mbili bora katika misimu mitatu kati ya minne iliyopita zinaonekana kuwa katika kiwango cha juu zaidi kuliko nyingine zote kufikia sasa.
Je, huu tayari ni ushindani wa timu mbili pekee?
Zikiwa na makocha wapya (au walioanza hivi karibuni), timu za Manchester United, Chelsea, Liverpool na Tottenham zote zilikuwa zikitarajia matokeo bora zaidi msimu huu.
Lakini kufikia sasa, viwango vyao vya kuanza msimu vimekuwa vya kusuasua hadi kufikia hatua ya kuwa vibaya mno.
Timu mbili za juu zimefanya vizuri kiasi gani?
Arsenal na Manchester City ndizo timu mbili pekee zenye pointi 12 kutoka katika michezo minne.
Tayari zinaongoza kwa pointi nne dhidi ya Hull City iliyo katika nafasi ya tatu ambayo licha ya kuanza vyema sana, huenda isijione kuwa katika kinyang'anyiro cha ubingwa na pointi tano mbele ya timu nyingine zote.
Arsenal ndio mabingwa watetezi na walitabiriwa kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kabla ya msimu kuanza.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Chini ya kocha Mikel Arteta, walihitimisha ukame wa mataji wa miaka 22 msimu uliopita kwa mtindo wa uchezaji ambao mara nyingi ulionekana kuwa wa kuhitaji nguvu na uvumilivu mkubwa (attritional style).
Walianza msimu huu kwa ushindi wa kuvutia wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Community Shield.
Na wameendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Coventry, Aston Villa, Chelsea na Sunderland pamoja na Napoli katika Ligi ya Mabingwa.
Ikijumuisha msimu uliopita, sasa wana rekodi ya kushinda mechi tisa mfululizo kwenye na mara ya mwisho kupoteza mchezo katika mashindano yoyote ndani ya dakika 90 ilikuwa dhidi ya City mnamo tarehe 19 April.
Tofauti na Arsenal, City hawana mwendelezo uleule msimu huu kutokana na kocha Pep Guardiola kuondoka baada ya kushinda mataji sita, ikiwemo mataji matatu makubwa kwa mpigo (Treble), katika kipindi cha miaka 10.
Enzo Maresca, ambaye aliwahi kuwa msaidizi wake, amechukua mikoba hiyo na kuwaongoza kupata ushindi katika mechi nne kati ya nne kwenye ligi baada ya kupoteza mchezo dhidi ya 'Gunners' jijini Cardiff.
Wamezifunga Bournemouth, Crystal Palace, Coventry pamoja na Porto katika Ligi ya Mabingwa ya kupata ushindi wa utata wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili.
Erling Haaland alifunga bao hilo pekee, huku chombo kinachosimamia waamuzi wa Ligi Kuu baadaye kikikiri kufanya makosa kwani bao hilo lilipaswa kukataliwa kwa madai ya kuotea (offside).
Licha ya kuanza msimu kwa rekodi ya ushindi wa asilimia 100, takwimu za kina kuhusu mwenendo wa Arsenal na City hazionyeshi utawala kamili.
Brighton (mabao 13) na Chelsea (mabao 10) zimefunga mabao mengi zaidi kuliko mabao nane ambayo kila moja ya timu hizo mbili zinazoongoza imefunga.
Kwa upande wa mashuti, Arsenal na City zinashika nafasi ya 10 na 11, na kwa kugusa mpira ndani ya eneo la hatari la wapinzani, zinashika nafasi ya sita na ya tano mtawalia.
Arsenal imefungwa bao moja pekee na City imefungwa mabao mawili rekodi mbili bora zaidi kwenye ligi hiyo.
Vipi kuhusu timu nyingine?
Timu tatu zilizofuata katika orodha ya wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa mujibu wa makampuni mengi ya kubashiri kwa mpangilio zilikuwa Chelsea, Liverpool na Manchester United, huku Tottenham ikiwa nyuma zaidi.
Chelsea na Liverpool zote ziliachana na makocha wao na kuajiri Xabi Alonso na Andoni Iraola mtawalia wakati wa majira ya joto.
United na Spurs zote zilibadilisha makocha mapema mwaka wa 2026, huku Michael Carrick na Roberto de Zerbi wakiongoza maandalizi ya kabla ya msimu kwa mara ya kwanza.
Msimu uliopita, Chelsea ilimaliza katika nafasi ya 10, Liverpool (kama mabingwa watetezi) ilishika nafasi ya tano, na Spurs ilimaliza ya 17 huku United ikimaliza ya tatu baada ya kuboresha kiwango chake chini ya Carrick.
Hivyo, kwa timu zote nne, kulikuwa na matumaini makubwa kwamba huu ungekuwa msimu bora zaidi.
Chelsea inashika nafasi ya tano, ikiwa imepoteza mchezo mmoja pekee hadi sasa na kufunga mabao 10... lakini imefungwa mabao tisa rekodi ya nne mbaya katika ligi hiyo.
Wamefungwa mabao mawili au zaidi katika kila moja ya mechi zao nne za kwanza za msimu wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2015-16.
Liverpool inashika nafasi ya saba, ikiwa haijapoteza mchezo wowote baada ya mechi nne lakini tatu kati ya hizo zimeisha kwa sare.
Hii ni mara ya tatu tu katika misimu 63 iliyopita ambapo wameshindwa kushinda mechi yoyote kati ya mbili za kwanza za ligi walizocheza nyumbani.
United inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi nne rekodi inayolingana na mwanzo wao mbaya zaidi wa msimu wa Ligi Kuu tangu 1992-93... na pia inalingana na msimu uliopita.
Wamepiga mashuti mengi zaidi kuliko timu nyingine yoyote kweny, ligi mashuti 84 na wameruhusu mashuti machache zaidi (41) dhidi yao.
Licha ya hayo, wameruhusu idadi ya mabao sawa na waliyofunga , mabao saba.
Spurs isingejiona kuwa katika kinyang'anyiro cha ubingwa baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 mara mbili mfululizo, lakini ingelitarajia kuanza vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa... ambapo inashika nafasi ya 17.
Na mbaya zaidi, hii ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo kushindwa kufunga bao lolote katika mechi zao nne za kwanza za ligi.
Historia inatuambia nini?
Kabla ya msimu huu, timu 80 katika ligi kuu ya Uingereza zilishinda mechi zao nne za kwanza za ligi hiyo.
Kati ya hizo, ni timu 24 pekee zilizofanikiwa kutwaa ubingwa, jambo linalothibitisha kuwa kutawala ligi mwanzoni hakumaanishi moja kwa moja kuwa timu itaweza kudumisha kasi hiyo hadi mwisho.
Katika enzi ya Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League), ni timu tisa kati ya 28 zilizoshinda mechi nne mfululizo mwanzoni mwa msimu ambazo hatimaye zilitwaa ubingwa; ya hivi karibuni ikiwa ni Manchester City katika msimu wa 2023-24.
Kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapa chini, ni misimu sita pekee ya awali ya Ligi Kuu ambapo timu mbili au zaidi zilishinda mechi zao zote nne za kwanza.
Na habari mbaya kwa timu zinazofukuzia ubingwa ni kwamba ni klabu mbili pekee zilizowahi kutwaa taji la Ligi Kuu baada ya kuwa nyuma kwa pointi tano au zaidi kufuatia mechi nne.
Manchester United ilifanikisha hilo mara tano chini ya Sir Alex Ferguson (1992-93, 1996-97, 1998-99, 2007-08 na 2008-09), huku Manchester City ya Pep Guardiola ikifanikiwa kufanya hivyo katika msimu wa 2020-21.
















