Moja kwa moja, Uingereza yatangaza msaada wa kijeshi dhidi ya Wahouthi kwa ombi la Saudi Arabia

Waziri Mkuu wa Uingereza, Andy Burnham, amesema Uingereza itatoa msaada wa kujihami wa kuongeza mafuta angani kwa Saudi Arabia, kufuatia mashambulizi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen dhidi ya Saudi Arabia.

Muhtasari

Uingereza yatangaza msaada wa kijeshi dhidi ya Wahouthi kwa ombi la Saudi Arabia

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Walinzi wa Mapinduzi Iran IRGC wadai kuimarisha uwezo wa kijeshi

    D

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Naibu kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, Mustafa Ezadi, amesema vikosi vya kijeshi vya Iran vinaendelea kuimarisha uwezo wao wa kijeshi.

    Kwa mujibu wa BBC Persian, vyombo vya habari vya Iran viliripoti kuwa Ezadi alikaribisha kuendelea kwa wafuasi wa serikali kujitokeza mitaani nyakati za usiku, akisema:

    “Iwapo uwepo wa wananchi utaendelea, njama nyingi za adui zitazuiwa.”

    Naibu kamanda huyo amesema Iran kwa sasa inaendelea kuimarisha uwezo wake katika maeneo ya makombora, ndege zisizo na rubani, makombora ya kusafiri, mifumo ya mtandao, vita vya kielektroniki na ulinzi wa anga.

  2. Uingereza yatangaza msaada wa kijeshi dhidi ya Wahouthi kwa ombi la Saudi Arabia

    e

    Chanzo cha picha, NURPHOTO/REUTERS

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Andy Burnham, amesema Uingereza itatoa msaada wa kujihami wa kuongeza mafuta angani kwa Saudi Arabia, kufuatia mashambulizi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen dhidi ya Saudi Arabia.

    Uingereza imesema msaada huo utaanza kutolewa katika siku chache zijazo na utahusisha ndege ya Uingereza aina ya Voyager, itakayoendesha shughuli zake kutoka kituo cha jeshi la anga cha RAF Akrotiri nchini Cyprus.

    Waziri Mkuu amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Saudi Arabia kuomba “msaada wa kijeshi”, ombi alilolidhinisha kwa ushauri wa Waziri wa Ulinzi Wes Strating na Waziri wa Mambo ya Nje Ed Miliband.

    Maafisa wa Uingereza wamesema msaada huo utatolewa kwa “muda mfupi” na awali unaweza kudumu kwa “wiki kadhaa”.

    Wahouthi wanapigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa na inayoungwa mkono na Saudi Arabia.

    Katika siku za hivi karibuni, Wahouthi wamesema wamefanya mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu dhidi ya mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, pamoja na miundombinu ya nishati katika pwani ya Bahari ya Shamu.

    Kwa mujibu wa maafisa wa Uingereza, msaada huo wa “kujilinda” unaweza pia kuhusisha kusaidia ndege za jeshi la anga la Saudi Arabia kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani zinazoelekezwa nchini humo.

    Saudi Arabia inakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na mashambulizi ya Wahouthi nchini Yemen, ambao wanaonekana kuwa na upatikanaji wa mara kwa mara wa ndege zisizo na rubani na makombora, huku wakilenga nchi hiyo jirani ya kaskazini.

    Yemen imekuwa katika vita vya vipindi tangu mwaka 2014. Kuongezeka kwa mapigano hivi karibuni kumezidisha hali hiyo, hasa kutokana na uungwaji mkono wa Wahouthi na Iran, wakati Iran yenyewe ikiwa katika mzozo wa vipindi na Marekani.

    Soma Zaidi:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 22/09/2026.