Moja kwa moja, Mashambulizi yasitishwa: Trump aitaka Iran kufanya makubaliano haraka

Trump amesema uamuzi huo ulifikiwa kwa ushirikiano na Israel.

Muhtasari

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Mashambulizi yasitishwa: Trump aitaka Iran kufanya makubaliano haraka

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema amesitisha mpango wa kufanya mashambulizi dhidi ya Iran kwa sharti kwamba makubaliano yafikiwe "haraka" kati ya pande hizo mbili.

    Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Truth Social, Trump alisema aliamua "kufuta shambulio hilo, mradi tu iwezekane kufikiwa kwa MAKUBALIANO kwa haraka", ambayo yatajumuisha kufunguliwa mara moja kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz na kumalizika kwa kile alichokiita "tishio la nyuklia la Iran."

    Trump alisema uamuzi huo ulifikiwa kwa ushirikiano na Israel. Kauli hiyo imekuja wakati vyombo vya habari vya Marekani vikiripoti kuwa Marekani ilikuwa ikifikiria kufanya mashambulizi mapya na makali dhidi ya Iran mwishoni mwa wiki.

    Awali, Iran iliishutumu Marekani kwa kuongeza mvutano katika eneo hilo, ikionya kwamba taifa lolote la kikanda litakaloshirikiana na Marekani "litamezwa na vita" hivyo.

    Katika ujumbe wake, Trump alisema Marekani iko "tayari kabisa kwa hatua za kijeshi" dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akidai kuwa nguvu, uwezo wa kijeshi na vitisho vya Marekani vinafikia kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia.

    Hata hivyo, alisema aliamua kusitisha mashambulizi hayo baada ya kuombwa na Iran pamoja na baadhi ya mataifa ya Mashariki ya Kati kusubiri ili kutoa nafasi kwa mazungumzo ya kufikia makubaliano.

    Trump pia alidokeza kuwa hatua imepigwa katika mazungumzo hayo, akisema kuwa "misingi ya makubaliano tayari umefikiwa."

    "Hatua hii itajumuisha kufunguliwa mara moja, kikamilifu na bila masharti kwa Mlango wa Hormuz, pamoja na kumaliza tishio la nyuklia la Iran," Trump aliandika.

    Soma Zaidi:

  2. Hujambo. Karibu katika matangazo yetu ya mubashara ya tarehe 2/08/2026. Mimi ni Asha Juma.