Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanasayansi watafanikiwa kuotesha meno mapya ya binadamu?
- Author, Sarah Sloat
- Nafasi, BBC
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Ingawa meno yana jukumu kubwa katika afya kuliko wengi wanavyofikiria, suluhisho la sasa kwa meno yanayong’oka au kuharibika ni la muda mfupi, na sio la kudumu.
Zamani haikuelweka kwamba "afya ya mdomo ni muhimu kwa afya mwili wako," anasema Pamela Yelick, profesa katika Shule ya Tiba ya Meno ya Tufts nchini Marekani.
Sasa, inaeleweka kwamba matatizo ya meno, kama vile bakteria katika fizi, yanaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na maambukizi ya mfumo wa kupumua.
Matatizo ya kupoteza jino, yanaathiri uwezo wa kula, kutafuna, na kutabasamu, na inaweza kudhuru ustawi wa kijamii na kihisia.
Madaktari wa meno wana zana nyingi za kusaidia kukabiliana na matatizo ya meno. Wanaweza kurekebisha mashimo kwa kuondoa sehemu iliyoharibika na kuliziba jino.
Lakini hili sio suluhisho la kudumu. Kwa mfano, kuna utofauti uimara wa baada ya jino kuzibwa, uzibaji unaweza kudumu kuanzia miaka mitano hadi 20.
Na marekebisho haya yanalenga zaidi "kurekebisha uharibifu, na sio kurejesha utendaji kazi wa jino kama mwanzo," anasema Anne George, profesa wa biolojia ya kinywa katika Chuo Kikuu cha Illinois, Chicago, nchini Marekani
Kwa nini meno hutoboka?
Meno yana tabaka nne kuu. Matundu hujitokeza wakati bakteria wanaokula sukari na kutoa asidi ambayo huyeyusha polepole safu ya kwanza ya jino. Na kila tabaka inayofuata ya meno ndio laini zaidi. Hadi tundu la jino.
George anatafiti protini zinazosaidia meno kukua, kung'arisha, na kujirekebisha. Pia alikuwa sehemu ya timu iliyounda moja ya jeni zinazosaidia kujenga meno, ili kuelewa zaidi kuhusu utendaji kazi wa ndani wa jinsi meno yanavyoundwa na kudumisha tishu zake.
Maarifa haya yanaweza kuleta matibabu mapya ambayo huchochea meno yaliyoharibika kurekebisha uharibifu wa mashimo, anasema George, ili kuondoa hitaji la daktari kuziba meno.
Kwa sasa ikiwa jino lina mashimo mengi na kuoza, matibabu bora na rahisi zaidi yanaweza kuwa kulitoa na kuweka jino jingine la bandia. Lakini meno ya bandia hayana mishipa inayokusaidia kuhisi unapotafuna, kwa hivyo inaweza kusababisha kutafuna sana na kupasua jino hilo.
Bakteria wanaweza kuingia katika jino bandia, na kusababisha hali ambayo inaweza kuathiri meno yaliyobaki yenye afya. Meno bandia huhitaji kubadilishwa baada ya takriban miaka 15 na yanaweza kugharimu maelfu ya dola.
Meno ya wanyama wengine
Meno yaliyokuzwa katika maabara yanaweza kuwa suluhisho la kudumu zaidi kuliko meno bandia, anasema Ana Angelova Volponi, mtaalamu wa meno katika Chuo cha King's London, nchini Uingereza.
Timu ya Volponi iligundua kuwa seli zilizochukuliwa kutoka katika tishu za fizi za binadamu, pamoja na seli zinazounda jino kutoka kwa panya, zinaweza kuzalisha "jino" lenye mizizi inayoendelea kukua.
Tofauti na wanyama wengine, wanadamu hawawezi kuendelea kuota meno baad ya kupata meno yao ya utu uzima. Lakini papa wana utesha meno. Pia uwezo huo anaa Kangaroo na tembo.
Nguruwe pia wana tabia ya kuotesha meno. Hata kama nguruwe atatolewa jino, kuna mashina kwenye taya yanayojiandaa kuunda jino lingine.
Kutoka maabara hadi kinywani
Licha ya mahitaji ya meno mapya, bado tuko mbali kwa miaka mingi kuwa na mtu wa kwanza mashimo yake ya meno kuoteshwa meno mengine, mbali na yale ya bandia.
Kabla ya "kuanza kuzungumzia" kuwachunguza wanadamu, majaribio kwa Wanyama yanapaswa kufanyika kwanza, anasema Ruohola-Baker.
Hilo litahitaji utafiti zaidi, muda, na pesa. Zaidi ya hayo, ili kuingiza meno yaliyokuzwa maabara kinywani mwa binadamu, watafiti wanahitaji kuunda mazingira bora ya ukuaji wa meno.
Wakati huo huo, masomo yaliyopatikana katika meno ya yanyozaliwa upya kwa wanyama yanaweza kusaidia juhudi pana za kuzalisha meno kwa binadamu na pia katika viungo na mifupa.
Juhudi za kutafiti meno katika maabara zinawafundisha wanasayansi jinsi tishu ngumu na laini zinavyofanya kazi pamoja.
Ingawa huenda isitokee hivi karibuni, Volponi ana imani suluhisho salama na endelevu la meno hatimaye litapatikana kwa binadamu.