Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Matetemeko mawili makubwa ya ardhi yakumba mji mkuu wa Venezuela

Tetemeko la kwanza lilikuwa la ukubwa wa 7.2 lilifuatiwa kwa karibu na linguine lenye ukubwa wa 7.5 na kuzua hali ya taharuki.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Italia yamkosoa Katibu Mkuu wa NATO baada ya Marekani kutumia kambi za Italia katika vita na Iran

    Italia ilikosoa matamshi ya Katibu Mkuu wa NATO kuhusiana na jeshi la Marekani kutumia kambi za kijeshi nchini Italia katika vita na Iran.

    Akijibu ukosoaji wa Donald Trump kwamba washirika wa NATO hawakuunga mkono Marekani vya kutosha, Mark Rutte aliiambia Fox News kwamba Ulaya imekuwa "jukwaa kwa Marekani kuonyesha na kutumia nguvu."

    "Ndege mia tano za Marekani ziliruka kutoka kambi za Marekani nchini Italia ili kusaidia Operesheni Epic Fury.

    Kwa hiyo msaada wetu ulikuwa mpana sana," alisema. Bw. Rutte pia alisema wakati wa vita, kati ya wanajeshi 4,000 na 5,000 walisafirishwa na ndege za Kimarekani kutoka kambi za Ulaya.

    Lakini Wizara ya Ulinzi ya Italia inasema katika taarifa kwamba matamshi hayo yaliwakilisha "picha ya kupotosha kabisa" kwa sababu hayatofautishi kati ya aina za ndege.

    Wizara hiyo ilisisitiza kuwa Italia iliidhinisha tu safari za ndege za "kiufundi, vifaa, na zisizo za kijeshi" za Marekani ndani ya mfumo wa makubaliano yaliyopo na Marekani, na "katika hali ambapo maombi yalifanywa nje ya mfumo huu, kama inavyojulikana, Italia haikutoa idhini."

    Serikali ya Italia imesisitiza kuwa haijaidhinisha matumizi ya maeneo yake na vituo vyake kwa misheni ya moja kwa moja ya kijeshi ya Marekani katika vita na Iran, na kwamba jukumu lake lilikuwa tu kwa msaada wa kiufundi na vifaa.

  2. Trump: Iran inapaswa kukubaliana na kila kitu ninachotaka

    Katika taarifa zake za hivi punde, Rais wa Marekani amesema kuwa, ameridhishwa na mchakato wa maelewano kati ya Iran na Marekani.

    "Nani angefikiria hili lingetokea? Huu ni wakati wa vita na Iran ina tabia nzuri sana. Wanakubali kila kitu ninachouliza na wanapaswa kufanya. Vinginevyo, tutarudi tu na kufanya kile kinachohitajika," Bw. Trump aliwaambia waandishi wa habari, akizungumzia bei ya mafuta inayokaribia $ 70 kwa pipa.

    Katika siku za hivi karibuni, kufuatia mkutano wa timu za mazungumzo za Marekani na Iran nchini Uswizi, ambao ulisuluhishwa na Pakistan, maafisa kutoka nchi zote mbili wametoa kauli kali na zinazokinzana.

    Soma zaidi:

  3. Marekani kuiuzia Uturuki injini za ndege za kivita zenye thamani ya mamilioni ya dola

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, utawala wa Rais wa Marekani Donald

    Trump unanuia kusonga mbele na mpango wa kuiuzia Türkiye makumi ya injini za ndege zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dola.

    Hatua hiyo, ambayo inafanywa licha ya upinzani kutoka kwa Congress, ni maendeleo makubwa kwa Ankara kabla ya mkutano wa kilele wa NATO mwezi ujao, vyanzo vinne vinavyofahamu suala hilo viliiambia Reuters.

    Injini hizi, zinazotengenezwa na General Electric, zitatumia Qa'an, ndege ya kwanza ya kivita ya Türkiye.

    Türkiye, kama mwanachama wa NATO, alianza mradi huu mkubwa mwaka wa 2016 ili kujitegemea zaidi ulinzi.

    Chanzo kimojawapo kilisema dili hilo litakuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 700 na linatarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.

    Soma pia:

  4. Kwa picha: Hofu na wasiwasi katika mitaa ya Caracas

    Picha zilizopigwa saa chache tbaada ya kutokea kwa tetemeko hilo zinaonyesha wakaazi wakiwa wamekusanyika kwenye mitaa ya mji mkuu wa Venezuela, baada ya nyumba zao kuporomoka na umeme kukatika.

    Wengine wanaonekana wakiwakumbatia ndugu na jamaa zao, huku maafisa wa waokoaji wakipekua vifusi kuwatafuta walionaswa.

    Mamlaka zinahofia tetemeko hilo limesababisha uharibifu mkubwa, lakini kiwango kamili cha uharibifu bado hakijajulikana.

  5. Matetemeko makubwa ya ardhi yakumba Venezuela na kuangusha majengo Caracas

    Mji mkuu wa Venezuela Caracas, umekumbwa na matetemeko mawili makubwa yaliyoachana kwa sekunde chache.

    Tetemeko la kwanza lilikuwa la ukubwa wa 7.2 lililotokea katika eneo la Montalbán, magharibi kidogo mwa Caracas, kulingana na shirika la ufuatiliaji wa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGC).

    Sekunde 39 baadaye, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.5 lilipiga takriban kilomita 10 ndani ya eneo hilo.

    Matetemeko hayo yametajwa kuwa moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ya Amerika Kusini katika karne moja.

    Majengo yaliporomoka na wakaazi kukimbilia barabarani kutafuta usalama wakati matetemeko ya ardhi yalipotokea.

    Rais wa mpito wa Venezeula Delcy Rodríguez ametangaza hali ya hatari.

    Kuna hofu ya majeruhi na uharibifu mkubwa lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusiana na hilo kufikia sasa. Waokoaji wako mbioni kuwatafuta manusura ambao huenda wamenaswa chini ya vifusi.

  6. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.