Moja kwa moja, Lissu ataka kulipwa fidia kwa kesi yake ‘kucheleweshwa’

Lissu amedai kuwa upande wa Jamhuri umechelewesha shauri lake kwa makusudi ili kumweka kizuizini

Skip Video and continue reading
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Majaribio ya tiba ya Ebola yaanza nchini DRC

    Wahudumu wa afya

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la Afya Duniani limetangaza kuanza kwa majaribio ya dawa zinazoweza kutibu aina ya virusi vinavyosababisha mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisema Alhamisi kuwa mgonjwa wa kwanza tayari ameandikishwa kushiriki katika majaribio hayo nchini DR Congo.

    Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watu 1,400 wameambukizwa huku 438 wakithibitishwa kufariki kutokana na mlipuko huo.

    Kwa sasa hakuna chanjo au tiba iliyoidhinishwa dhidi ya aina ya virusi vya Bundibugyo, ambayo ni mojawapo ya aina za virusi vya Ebola na huambukiza kwa urahisi.

    Utafiti huu unafadhiliwa na WHO na unaratibiwa kwa ushirikiano kati ya Institut National de Recherche Biomédicale, Institute of Tropical Medicine na University of Oxford.

    Katika majaribio hayo, wagonjwa watapewa dawa mbili za kuzuia virusi (antiviral) ili kupima ufanisi wake.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya WHO mjini Geneva, Tedros alisema:

    "Hata bila tiba zilizoidhinishwa, baadhi ya watu wanapona ugonjwa huu. Hata hivyo, tunaweza kuokoa maisha mengi zaidi ikiwa tutakuwa na tiba salama na zenye ufanisi."

    Waziri wa Afya wa DR Congo, Samuel Roger Kamba, alisema kuanza kwa majaribio hayo ni hatua muhimu ya maendeleo, inayotoa matumaini mapya kwa wagonjwa, familia zao na jamii zilizoathirika.

    Unaweza kusoma;

  2. Shughuli za mazishi ya Ali Khamenei zaanza mapema kuliko ilivyotangazwa awali

    Mazishi ya Khamenei huko Mosalla

    Chanzo cha picha, IRNA

    Shirika la habari la IRNA limeripoti kwamba shughuli za mazishi ya Ali Khamenei zimeanza leo mapema kuliko ilivyokuwa imetangazwa awali.

    Kwa mujibu wa IRNA, ingawa hapo awali ilitangazwa kuwa shughuli za mazishi ya Ali Khamenei, aliyekuwa kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zingeanza Ijumaa jioni, shughuli za kutoa heshima kutoka kwa wageni wa kimataifa tayari zimeanza na zinaendelea.

    Mwili wa kiongozi huyo, ambaye IRNA inamtaja kama "kiongozi wa mapinduzi aliyefariki kishahidi," pamoja na miili ya baadhi ya wanafamilia wake, umewekwa mbele ya madhabahu katika Msikiti wa Mosalla wa Tehran.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mohammad Reza Aref, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mehrabad mjini Tehran na anawapokea maafisa na wajumbe wa kimataifa wanaowasili kuhudhuria shughuli hizo.

    IRNA pia imesema kuwa Mesbah al-Hoda Bagheri Kani, mkwe wa Ali Khamenei, atazikwa Ijumaa katika Uwanja wa Shahran na kijiji cha Kani, magharibi mwa Tehran, na baadaye huenda mwili wake ukapelekwa Mosalla.

    Hapo awali, Gavana wa Tehran pamoja na kamati ya maandalizi ya mazishi walikuwa wametangaza kwamba shughuli hizo zingeanza asubuhi ya Jumamosi, tarehe 4 Julai, kwa "hafla ya kuuaga mwili" katika Msikiti wa Imam Khomeini.

    Unaweza kusoma;

  3. Lissu ataka kulipwa fidia kwa kesi yake ‘kucheleweshwa’

    lissu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, ameomba Mahakama ya Rufani Dar es Salaam iamuru Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kumlipa fidia kutokana na usumbufu wa siku 139. Alidai ucheleweshaji huo ni mkakati wa makusudi wa kumuweka kizuizini.

    Lissu alitoa ombi hilo mbele ya jopo la majaji watatu akieleza kuwa mbinu hizo za kisheria zinazotumiwa na upande wa Jamhuri zinasababisha kesi iwe ya kusuasua na kumfanya aendelee kusalia gerezani .

    Alibainisha kuwa ucheleweshaji wa shauri hilo kwa makusudi ulianza mnamo Februari 24, 2026, na umefikia siku 139 hadi alipotoa ombi hilo .

    Alisema tayari ametimiza mwaka mmoja na miezi mitatu tangu akamatwe kwa tuhuma za uhaini, na akaitaka mahakama itupilie mbali maombi hayo ya DPP kwa kuwa hayana maslahi ya umma na badala yake aamriwe kulipa fidia.

  4. Iran yaonya dhidi ya shambulio lolote wakati wa mazishi ya Khamenei

    jeshi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Iran imesema kuwa ikiwa Marekani, Israel au washirika wao watachukua hatua yoyote wakati wa mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, Iran itatoa jibu kali na linalofaa.

    Kwa mujibu wa BBC Monitoring, Meja Jenerali Ali Abdullahi, kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya nchini Iran, ameonya Marekani, Israel na washirika wao kujiepusha na hatua zozote dhidi ya Iran kabla ya mazishi ya Ali Khamenei.

    Abdullahi, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa juu wa jeshi la Iran, alisema kuwa hafla ya mazishi itaonesha azma ya wananchi wa Iran ya "kulipiza kisasi" kwa kifo cha Ali Khamenei.

    Habari hiyo iliripotiwa tarehe 2 Julai na shirika la habari la Tasnim, linalohusishwa na Islamic Revolutionary Guard Corps kupitia akaunti yake ya Telegram.

    Alisema:

    "Tunamuonya adui mwenye nguvu wa Iran, hususan Marekani, utawala wa Israel na washirika wao katika eneo hili na kwingineko, waepuke kufanya jambo lolote linaloweza kusababisha kutokuelewana au makosa ya tathmini."

  5. Rais wa Cuba: Hatutafuti vita, lakini pia hatuviogopi

    Rais wa Cuba, Miguel Díaz-Canel

    Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock

    Rais wa Cuba, Miguel Díaz-Canel amesema katika mahojiano na Sky News kwamba anachukulia kwa uzito vitisho vya Donald Trump vya uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Cuba.

    Amesema yuko tayari kupigana "hadi tone la mwisho la damu" kwa ajili ya nchi yake na maadili ya jamii ya Cuba.

    Katika mahojiano ya kipekee na Sky News siku ya Alhamisi, Díaz-Canel alisema:

    "Hatutafuti vita, lakini pia hatuviogopi."

    Kauli za Díaz-Canel zinajibu vitisho vya mara kwa mara vya Donald Trump dhidi ya mji mkuu wa Cuba, Havana, pamoja na taarifa zinazoonesha kuongezeka kwa uwepo wa kijeshi wa Marekani karibu na mipaka ya bahari inayozunguka Cuba.

    Unaweza kusoma;

  6. Grossi: Wakaguzi wa IAEA bado hawawezi kurejea katika vituo vya nyuklia vya Iran

    Grossi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rafael Grossi amesema kwa shirika la habari la Urusi, RIA Novosti, kwamba wakaguzi wa IAEA bado hawajaweza kurejea katika vituo vya nyuklia vya Iran.

    "Tumewasilisha ombi la kufika huko, lakini hadi sasa hatujaweza kupata nafasi," alisema.

    Bw. Grossi alikuwa amesema awali kwamba makubaliano ya muda kati ya Iran na Marekani yangeruhusu wakaguzi wa IAEA kufikia vituo vya nyuklia vya Iran. Hata hivyo, Iran imesema kuwa suala hilo litajadiliwa katika makubaliano ya mwisho yanayoweza kufikiwa kati ya Iran na Marekani.

    Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema wiki iliyopita kwamba "Iran imekubali kikamilifu na bila masharti ukaguzi wa nyuklia katika kiwango cha juu zaidi na kwa muda mrefu sana ujao." Aliongeza kuwa, "Kama Iran isingekubali hilo, kusingekuwa na mazungumzo zaidi."

    Baadaye, Trump alisema kuwa hakuna haraka ya kuanza tena ziara za wakaguzi wa IAEA nchini Iran.

    Katika mahojiano ya televisheni, Mohammad Baqer Qalibaf alikataa makubaliano yoyote mapya kuhusu ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran.

    Alisema wakaguzi wataruhusiwa tu kufikia vituo kama vile Bushehr Nuclear Power Plant na Tehran Research Reactor, ambavyo tayari vilikuwa vimeidhinishwa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.

    Hata hivyo, hawataruhusiwa kufikia vituo vya urutubishaji cha Fordow Natanz na Isfahan, ambavyo vilishambuliwa katika mashambulizi ya anga ya Marekani mwaka uliopita.

    Suala la ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran, ambavyo vililengwa na mashambulizi ya kijeshi wakati wa vita, limekuwa chanzo cha mvutano kati ya Iran, IAEA na mataifa ya Magharibi.

    Wakati wa mashambulizi ya Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na baadaye Marekani kujiunga na vita na kushambulia vituo vikuu vya nyuklia vya Iran huko Isfahan, Natanz na Fordow karibu na Qom, Iran iliwazuia wakaguzi wa IAEA kurejea katika vituo hivyo.

    Hata hivyo, iliwaruhusu kukagua vituo ambavyo havikushambuliwa, kama vile Kituo cha Nyuklia cha Bushehr na Kinu cha Utafiti cha Tehran.

    Iran inasema hakuna kanuni zinazohusu ukaguzi wa vituo vya nyuklia ambavyo vimeshambuliwa kijeshi.

    Kwa upande mwingine, IAEA inasisitiza kuwa vituo hivyo havipaswi kutengwa na ukaguzi wa kawaida na kwamba Iran inapaswa kuwaruhusu wakaguzi kutembelea vituo hivyo.

    Unaweza kusoma;

  7. Iran yasema haijaalika mataifa yaliyounga mkono mashambulizi dhidi yake

    F

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amesema kuwa mataifa ya Ulaya yaliyochukua msimamo rasmi wa kuunga mkono mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran hayajaalikwa kuhudhuria mazishi ya Ayatollah Ali Khamenei.

    Hata hivyo, Baghaei amesema ujumbe kutoka baadhi ya mataifa ya Ulaya Mashariki utahudhuria shughuli hizo.

    Amesema karibu mataifa 100 yanatarajiwa kutuma ujumbe rasmi, watu mashuhuri au makundi mbalimbali kushiriki katika shughuli za mazishi hayo.

    Kwa mujibu wa Baghaei, angalau wakuu wanane wa nchi, wakiwemo marais na mawaziri wakuu, pamoja na maspika wa mabunge kutoka mataifa 12, wamewasili Iran.

    Aidha, mawaziri wa mambo ya nje, mawaziri wengine na wawakilishi maalumu kutoka mataifa mengi pia wanashiriki katika shughuli hizo.

    Unaweza kusoma;

  8. Tanzania yaweka utaratibu wa kufuatwa kabla ya maandamano

    Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Tanzania, Patrobas Katambi

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Tanzania, Patrobas Katambi

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania, Patrobas Katambi, amefafanua utaratibu wa kisheria unaosimamia maandamano na mikusanyiko ya hadhara, akisisitiza wajibu wa waandaaji kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi angalau saa 48 kabla ya kufanyika kwa shughuli hizo.

    Aidha, Katambi amesema utaratibu huo umeainishwa katika Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322, hususan vifungu vya 42, 43, 44, 45 na 46.

    Amesema kifungu cha 42 kinaipa Polisi mamlaka ya kusimamia na kuratibu mikusanyiko na maandamano yote yanayofanyika nchini, huku kifungu cha 43 kikielekeza kuwa mtu au waandaaji wanaokusudia kufanya mkusanyiko au maandamano katika maeneo ya umma wanapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa Mkuu wa Polisi angalau saa 48 kabla ya tukio husika.

    Kauli hiyo ya Katambi inakuja kufuatia mjadala ulioibuka kuhusu maagizo yake ya kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kusitisha utoaji wa vibali vya mikutano ya vyama vya siasa.

    Kwa sasa, serikali inaeleza kuwa uamuzi wa kusitisha mikutano ya kisiasa unatokana na sababu za kiusalama na juhudi za kuzuia vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza. Wakati huo huo, mitandaoni kumekuwa na miito ya kuitisha maandamano yanayotarajiwa kufanyika Julai 7, 2026.

    Oktoba 29, 2025, Tanzania ilishuhudia maandamano yaliyoambatana na vurugu na ghasia katika maeneo mbalimbali, ambapo watu 518 waliripotiwa kupoteza maisha huku maelfu wengine wakijeruhiwa, tukio lililoacha athari kubwa kwa usalama na shughuli za kijamii na kiuchumi nchini.

  9. Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wawasili Iran kuhudhuria mazishi ya Khamenei

    D

    Chanzo cha picha, ISNA

    Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Mohsen Naqvi, amewasili katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kuhudhuria mazishi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

    Naqvi alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Eskandar Momeni.

    Pakistan imekuwa ikipatanisha mazungumzo kati ya Iran na Marekani, na Naqvi amezuru Tehran mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya Taliban nchini Afghanistan, Amir Khan Muttaqi, pia amewasili Tehran kwa ajili ya shughuli hizo za mazishi. Jana alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi.

    Picha zilizotolewa saa chache zilizopita pia zilimuonyesha He Wei, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Wananchi la China, akiwasili Tehran kuhudhuria shughuli za leo. Mara baada ya kuwasili, alikutana na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf.

    Maafisa kutoka Turkmenistan, Armenia, eneo la Kurdistan nchini Iraq na mataifa mengine kadhaa pia wamewasili Tehran.

    Ujumbe kutoka Vikosi vya Uhamasishaji wa Umma vya Iraq umefika Iran ukiongozwa na Hadi Ameri, mbunge na mmoja wa makamanda wakuu wa kundi hilo.

    Iran inatarajia viongozi wa nchi, maspika wa mabunge na mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa kadhaa kuhudhuria mazishi hayo.

    Kwa mujibu wa Naibu Msemaji wa serikali ya Taliban, mbali na Waziri wa Mambo ya Nje, kiongozi wa Taliban Abdul Ghani Baradar Akhund pia atahudhuria mazishi hayo.

    Vyanzo vimeieleza BBC kuwa ubalozi mdogo wa Iran mjini Herat umetoa zaidi ya visa 2,000 vya bure kwa raia wa Afghanistan wanaotaka kuhudhuria shughuli hizo.

    Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, visa hivyo vya muda mfupi vimetolewa zaidi kwa wanaharakati wa kijamii na kitamaduni wa Afghanistan, wengi wao wakitarajiwa kuingia Iran kupitia Mkoa wa Herat.

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

  10. Majaribio ya dawa zinazoweza kutibu Ebola ya Bundibugyo yaanza

    F

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuanza kwa majaribio ya kitabibu ya dawa mbili zinazoweza kutibu aina ya virusi vya Ebola vya Bundibugyo, vinavyosababisha mlipuko hatari wa ugonjwa huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Mgonjwa wa kwanza tayari ameanza kushiriki katika majaribio hayo, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

    Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa zaidi ya visa 1,400 vya Ebola vimethibitishwa nchini DR Congo, huku watu 438 wakithibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.

    Hadi sasa, hakuna chanjo wala dawa iliyoidhinishwa kimataifa kwa ajili ya kutibu aina ya Ebola ya Bundibugyo, ambayo inajulikana kwa kuenea kwa haraka na kuwa na kiwango kikubwa cha vifo.

    Majaribio hayo yanaungwa mkono na WHO na yanatekelezwa na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Afya ya Umma ya Congo, Taasisi ya Ubelgiji ya Magonjwa ya Tropiki na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza.

    Akizungumza katika makao makuu ya WHO mjini Geneva, Dkt. Tedros alisema, "Leo tumeanzisha majaribio ya dawa mbili zinazoweza kutibu Ebola, na mgonjwa wa kwanza tayari ameanza kushiriki katika utafiti huo."

    Aliongeza, "Ingawa hakuna tiba iliyoidhinishwa kwa sasa, baadhi ya wagonjwa wamepona. Lakini kama tungekuwa na matibabu yaliyothibitishwa kuwa salama na yenye ufanisi, tungeokoa maisha ya watu wengi zaidi."

    Mlipuko wa Ebola nchini DR Congo na Uganda ulianza mwezi Mei, na WHO imeutangaza kuwa Dharura ya Afya ya Umma ya Kimataifa.

    Pia unaweza kusoma:

  11. Katika picha: Hali ilivyo katika mahakama ya Rufani kabla ya kesi kuanza

    Baadhi ya wananchi waliojitokeza kusikiliza kesi ya Lissu
    Maelezo ya picha, Baadhi ya wananchi waliojitokeza kusikiliza kesi ya Lissu
    w
    Maelezo ya picha, Waliofika mahakamani wakisubiri kesi kuanza
    Mwanasheria wa Serikali Nasorro Katuga (kushoto) akiteta na wanasheria wenzake
    Maelezo ya picha, Mwanasheria wa Serikali Nasorro Katuga (kushoto) akiteta na wanasheria wenzake
    Watendaji mbalimbali wa Mahakama
    Maelezo ya picha, Watendaji mbalimbali wa Mahakama
  12. Lissu afika Mahakama ya Rufani, marejeo ya kesi ya uhaini yasikilizwa leo

    g

    Chanzo cha picha, Mwananchi

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, tayari amefika katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam ambako mahakama hiyo inatarajiwa kusikiliza maombi ya marejeo yanayohusiana na kesi ya uhaini inayomkabili.

    Mahakama hiyo inasikiliza maombi ya marejeo Na. 7440840/2026 katika shauri la Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) dhidi ya Tundu Lissu.

    Maombi hayo yanasikilizwa na jopo la majaji watatu linaloundwa na Jaji Mwarija, Jaji Muruke na Jaji Khamis.

    Shauri la msingi la kesi ya uhaini lilisimama kwa takriban miezi minne ili kupisha usikilizaji wa rufaa ya Jamhuri iliyopinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupilia mbali ombi lake la kuwasilisha ushahidi wa nyongeza kupitia shahidi wake, ACP Amini Mahamba.

    Lissu alishtakiwa kwa kosa la uhaini mwezi Aprili 2025, miezi mitatu baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.

    Upande wa mashtaka unadai alitoa kauli zilizolenga kuhamasisha wananchi kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025.

    Mahakama ya Rufani inatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu maombi hayo baada ya kusikiliza hoja za pande zote.

  13. Jeneza la Khamenei lapelekwa katika msikiti wa Tehran

    f

    Chanzo cha picha, Isna

    Jeneza la Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, pamoja na miili ya baadhi ya wanafamilia wake waliouawa katika shambulio la pamoja la Israel na Marekani la Machi 29, limepelekwa katika msikiti mmoja mjini Tehran.

    Shirika la habari la ISNA limesema baadhi ya wageni wa kigeni waliowasili nchini Iran wametoa heshima zao kwa kuhudhuria ibada ya maombolezo mjini Tehran. Shughuli hizo zinatarajiwa kuendelea siku nzima.

    Miongoni mwa viongozi waliowasili Tehran kuhudhuria shughuli hizo ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Mohsin Naqvi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan chini ya utawala wa Taliban, Amir Khan Muttaqi.

    Imeelezwa pia kuwa maafisa kutoka Tajikistan, China na India wanatarajiwa kushiriki katika shughuli hizo.

    Baadhi ya wanafamilia wa Khamenei, akiwemo mkwe wake, mjukuu wake, mmoja wa mabinti zake na mke wa mwanawe Mojtaba Khamenei, waliuawa pamoja naye katika shambulio hilo.

    Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na mamlaka za Iran, shughuli za kuaga na mazishi ya Khamenei zitafanyika kwa hatua kadhaa katika siku mfululizo.

    Baada ya shughuli za maombolezo mjini Tehran na baadaye Qom, mazishi yake yanatarajiwa kufanyika mjini Mashhad Alhamisi ijayo. Kabla ya hapo, mwili wake pia unatarajiwa kupelekwa katika miji ya Najaf na Karbala nchini Iraq.

  14. Minyoo 38 yapatikana kwenye ubongo wa mwanamke baada ya kula nyama ya nguruwe India

    h

    Chanzo cha picha, Lowri Denman

    Laurie Denman aligundua kwa mara ya kwanza kuwa kuna jambo lisilo la kawaida mwilini mwake baada ya kuona minyoo mrefu wa takriban mita moja alipoenda chooni.

    "Ilikuwa ya kutisha sana. Ilifanana na utepe wenye mistari midogo midogo," alisema Laurie, mwenye umri wa miaka 42 kutoka Wales.

    Hilo lilikuwa ishara ya kwanza ya ugonjwa wa neurocysticercosis, hali iliyosababisha minyoo 38 kupatikana kwenye ubongo wake na kusababisha maumivu makali ya kichwa, degedege na matatizo ya kisaikolojia.

    Laurie ni miongoni mwa watu wachache nchini Uingereza waliowahi kugundulika kuwa na maambukizi hayo ya ubongo, yanayosababishwa na mabuu ya minyoo ya nguruwe.

    "Daktari aliniambia, tumeangalia picha za uchunguzi wako na tumegundua kuna minyoo 38 kwenye ubongo wako," alisema Laurie.

    "Mimi na mama yangu tulitazamana kwa mshangao, tukijiuliza ni kitu gani hiki."

    Mwanzoni, madaktari walidhani alikuwa na toxoplasmosis, maambukizi yanayoenezwa kupitia kugusana na kinyesi cha paka aliyeambukizwa.

    Hata hivyo, mama yake aliwauliza madaktari kama hali hiyo inaweza kuwa inahusiana na minyoo aliyokuwa ameipata mwaka mmoja uliopita.

    Baada ya uchunguzi zaidi, hatimaye aligundulika kuwa na ugonjwa wa neurocysticercosis.

    Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu wanaweza kupata maambukizi hayo kwa kula nyama ya nguruwe mbichi au isiyopikwa vizuri, kunywa maji yaliyochafuliwa na mayai ya minyoo, au kutokana na tabia duni za usafi.

    Ugonjwa huo ni nadra sana nchini Uingereza na visa vingi huonekana kwa watu waliotoka katika maeneo ambako ugonjwa huo ni wa kawaida.

    Daktari Healy, ambaye alikuwa akimhudumia Laurie, alisema kuwa hiyo ndiyo ilikuwa kisa cha kwanza cha aina hiyo kukiona katika maisha yake yote ya taaluma.

    Baada ya miaka kadhaa ya kupona, sasa anataka kutumia uzoefu wake kuhamasisha watu kuhusu ugonjwa huo.

  15. Moto wa nyika wazidi kusambaa kusini mwa Ufaransa, watu 3,000 wahamishwa

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Moto mkubwa wa nyika unaoendelea kusambaa kusini mwa Ufaransa umesababisha karibu watu 3,000 kuhamishwa kutoka makazi yao, huku mamlaka zikionya kuhusu kuanza mapema kwa msimu wa moto kufuatia wimbi la joto kali lililovunja rekodi.

    Kwa mujibu wa vituo vya habari nchini humo, watalii na wakazi wa maeneo ya Sainte Marie la Mer na Canet en Roussillon walilazimika kuondoka baada ya moto kuzuka katika eneo la kambi na kusambaa kwa kasi.

    Moto huo umeharibu nyumba kadhaa za muda kabla ya kufika eneo la bandari, ambapo moshi mzito wenye sumu ulitanda juu ya boti na majengo ya karibu.

    Kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo, moto mkubwa zaidi umeshuhudiwa katika maeneo ya Aude na Herault, ambapo zaidi ya ekari 900 za ardhi tayari zimeteketea.

    Takriban wazima moto 800 na magari 150 ya zimamoto wametumwa kupambana na moto huo, huku juhudi za kuudhibiti zikiendelea.

    Soma zaidi:

  16. Kombe la Dunia: Ureno yaibuka na ushindi wa kusisimua dhidi ya Croatia

    H

    Chanzo cha picha, Reuters

    Timu ya taifa ya Ureno imefuzu kwa hatua inayofuata ya Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Croatia katika mchezo uliomalizika kwa tamati ya kusisimua baada ya dakika 18 za nyongeza.

    Ivan Perisic aliipa Croatia bao la kuongoza, kabla ya kufunga tena dakika chache baadaye, lakini bao hilo likakataliwa kwa kuotea.

    Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, aliisawazishia timu yake kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 68 na kuufanya mchezo huo kuingia katika dakika za mwisho ukiwa wazi kwa pande zote.

    Gonçalo Ramos aliifungia Ureno bao la ushindi katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza.

    Hata hivyo, Croatia ilionekana kupata bao la kusawazisha katika sekunde za mwisho za mchezo. Mchezo ulisimamishwa kwa takriban dakika tano ili VAR ipitie tukio hilo, kabla ya kuthibitishwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea na bao hilo likakataliwa.

    Mashabiki wa Croatia, waliokuwa wakitarajia timu yao kusawazisha na kupeleka mchezo katika muda wa ziada, walishuhudia matumaini yao yakitoweka katika sekunde za mwisho, huku wakionyesha kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi.

    Sasa Cristiano Ronaldo ataiongoza tena Ureno katika pambano kubwa dhidi ya Hispania, mataifa mawili jirani yenye historia ndefu na ushindani wa jadi katika soka la kimataifa.

    Kabla ya mchezo huo, Hispania iliifunga Austria mabao 3 kwa 0 na kufuzu kwa hatua inayofuata kwa urahisi.

    Unaweza kusoma;

  17. Iran yasema mazishi ya Khamenei yataufanya ulimwengu usikie wito wa kulipiza kisasi

    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Spika wa Bunge la Iran na mpatanishi mkuu wa nchi hiyo, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa wito kwa Wairani kushiriki kwa wingi katika mazishi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, akisema ushiriki huo utakuwa sehemu ya kulipiza kisasi kwa kifo chake.

    Katika taarifa yake Alhamisi, Qalibaf alisema, "Ninawaomba wananchi wote wa Iran kuandika ukurasa wa kihistoria wa Iran ya Kiislamu kwa kushiriki katika mazishi ya Khamenei."

    Aliongeza kuwa, "Wito wa taifa wa kulipiza kisasi lazima usikike duniani kote."

    Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limesema litachukua hatua za kulipiza kisasi kwa kifo cha Kiongozi Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

    Katika taarifa iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza hilo, Mohammad Baqer Zolqadr, Iran imesema "kisasi kwa damu ya Ayatollah Ali Khamenei kitachukuliwa dhidi ya waliomuua."

    Khamenei aliuawa Februari 28 wakati wa siku ya kwanza ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

    Wakati huo huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ametangaza kuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, atashiriki katika shughuli za mazishi ya Khamenei zitakazoanza Jumamosi mjini Tehran.

    Kwa mujibu wa BBC Persian, shughuli za mazishi ya Khamenei zitafanyika kati ya Julai 4 na 8 katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad, huku mikutano ya maombolezo pia ikipangwa kufanyika katika miji ya Baghdad, Kazmin, Karbala na Najaf nchini Iraq.

    Unaweza kusoma;

  18. Hujambo natumai umzima na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 03/07/2026.