Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Wahouthi wadai kushambulia mji mkuu wa Saudi Arabia

Kundi la Wahouthi kutoka Yemen wamesema wameshambulia maeneo muhimu katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, kwa makombora na ndege zisizo na rubani.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Simba 10 wafariki katika mbuga ya wanyama Tanzania

    Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro(NCAA) yasema simba kumi wameuawa tarehe 18, mwezi huu wa Septemba, katika eneo la Ndutu, kata ya Endulen.

    Uchnguzi wa awali umebaini kuwa simba hao walifariki baada ya kulishwa sumu.

    Mamlaka za hifadhi hiyo zimeanzisha uchunguzi wa kitalaam na wa kina kubaini chanzo cha vifo hivyo na waliohusika.

    Soma pia:

  2. Watu wawili wauawa katika shambulizi la Ukraine mjini Moscow

    Angalau watu wawili wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na Ukraine katika eneo la Moscow nchini Urusi usiku kucha, amesema Gavana wa Moscow Andrei Vorobyev.

    Vorobyev amesema ndege zisizo na rubani 249 zilidunguliwa,akiongezea kuwa nyumba kadhaa za makazi ziliwaka moto.

    Ghala moja katika eneo hilo pia lilishika moto. Katika mji mkuu Moscow, kiwanda cha kusafisha mafuta kiliharibiwa, huku vizuizi vya safari za ndege vikiwekwa katika viwanja viwili vya ndege.

    Wakati huo huo, afisa wa Ukraine amesema watu wanane, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kyiv na Sumy siku ya hapo jana.

    Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi yao hivi karibuni, yakilenga miundombinu ya kuzalisha nishati na usafirishaji, pamoja na vituo vikuu vya usafirishaji wa mizigo.

    Soma pia:

  3. Wahouthi washambulia mji mkuu wa Saudi Arabia

    Wahouthi kutoka Yemen wamesema walishambulia maeneo “nyeti” katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, kwa makombora na ndege zisizo na rubani hapo jana, saa chache baada ya kuonekana kwa moto na moshi mkubwa karibu na uwanja mkuu wa ndege wa jiji hilo.

    Saudi Arabia ilikuwa imetoa tahadhari usiku kucha kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa hatari ya mashambulizi karibu na Riyadh, huku kukiwa na ongezeko la mashambulizi yanayotekelezwa na Wahouthi nchini humo.

    Ingawa Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Saudi Arabia tangu mwezi Julai, madai ya hapo jana yanaonekana kuwa shambulizi lao la kwanza dhidi ya Riyadh tangu kuanza kwa mashambulizi dhidi ya taifa hilo.

    Wahouthi hawakueleza kwa undani walicholenga mjini Riyadh, lakini walisema pia walishambulia kituo cha kampuni ya mafuta ya Saudi Aramco katika mji wa Yanbu, ulioko kwenye Bahari ya Shamu, ambao ni kituo muhimu cha usafirishaji wa mafuta cha Saudi Arabia.

    Wahouthi wamesema operesheni hiyo ilikuwa jibu kwa shambulizi lililotekelezwa katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

    Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na Wahouthi umesema mifumo yake ya ulinzi wa anga iliharibu kombora lililorushwa na kundi hilo la Yemen kuelekea Riyadh mapema hapo jana.

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja