Watu wawili wauawa katika shambulizi la Ukraine mjini Moscow

Chanzo cha picha, Reuters
Angalau watu wawili wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na Ukraine katika eneo la Moscow nchini Urusi usiku kucha, amesema Gavana wa Moscow Andrei Vorobyev.
Vorobyev amesema ndege zisizo na rubani 249 zilidunguliwa,akiongezea kuwa nyumba kadhaa za makazi ziliwaka moto.
Ghala moja katika eneo hilo pia lilishika moto. Katika mji mkuu Moscow, kiwanda cha kusafisha mafuta kiliharibiwa, huku vizuizi vya safari za ndege vikiwekwa katika viwanja viwili vya ndege.
Wakati huo huo, afisa wa Ukraine amesema watu wanane, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika mashambulizi ya Urusi katika maeneo ya Kyiv na Sumy siku ya hapo jana.
Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi yao hivi karibuni, yakilenga miundombinu ya kuzalisha nishati na usafirishaji, pamoja na vituo vikuu vya usafirishaji wa mizigo.
Soma pia:

