Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Marekani na Iran zatia saini makubaliano ya kusitisha vita

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa makubaliano hayo tayari yamesainiwa na Mlango-Bahari wa Hormuz unatarajiwa kufunguliwa kuanzia Ijumaa, ingawa bado kuna sintofahamu kuhusu vipengele na masharti kamili ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Kombe ya Dunia 2026: Iran na New Zealand zatoshana nguvu

    Mchuano kati ya Iran na New Zealand umekamilika kwa sare ya mabao 2-2.

    New zealand walikuwa wa kwanza kugusa nyavu dakika ya 7 kupitia kwa Elijah Just.

    Iran wakasawazisha dakika ya 32 kupitia kwa Ramin Rezaeian.

    New Zealand wakaongoza tena dakika ya 54 kwa bao la Elijah Just tena, kisha Iran wakasawazisha tena dakika ya 64 kupitia kwa Mhammad Mohebi.

    Sasa kuna ugumu wa kundi G kwani timu zote nne Iran New Zealand, Misri na Ubelgiji zote zina alama moja.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Watu wanane wafariki baada ya ndege aina ya B-52 kuanguka Marekani

    Watu wanane, wakiwemo wafanyakazi wawili wa Boeing, wameuawa baada ya ndege aina ya B-52 ya Jeshi la Anga la Marekani kuanguka mara tu baada ya kupaa kutoka Kituo cha Jeshi la Anga cha Edwards kusini mwa California.

    Tukio hilo lilitokea saa 11:20 kwa saa za eneo (19:20 GMT) siku ya Jumatatu wakati ndege hiyo ilikuwa katika misheni ya kawaida ya majaribio. Ajali hiyo ilisababisha moshi mkubwa mweusi angani ambao ungeweza kuonekana umbali wa maili nyingi.

    "Leo, Kituo cha Jeshi la Anga cha Edwards kilipata ajali mbaya, na tumewapoteza Wamarekani wanane mashuhuri," Kanali James Hayes alisema, akiwaelezea kama "kikosi mchanganyiko cha wanajeshi, wafanyakazi na wakandarasi wa serikali".

    Awali, Kambi hiyo ilisema kwamba dalili za awali zinaonyesha kuwa ajali hiyo "haingeweza kunusurika".

    Ndugu wa karibu wa wafanyakazi wanaarifiwa na watatajwa baada ya saa 24, Hayes alisema katika mkutano wa alasiri.

    Kituo hicho kimesitisha shughuli zake kwa muda.

    Alisema ndege aina ya B-52 ilikuwa yenye muundo wa kisasa wa rada na ilianguka mara tu baada ya kupaa na kuwaka moto.

    Baada ya kupitia video za awali, tukio hilo lilionekana kutokea "ajali isiyoweza kukingika," Hayes alisema.

    Pia unaweza kusoma:

    Soma zaidi:

  3. Marekani na Iran zatia saini makubaliano ya kusitisha vita

    Marekani na Iran zimetia saini makubaliano ya awali ya kusitisha vita vya Ghuba, katika juhudi za kumaliza mzozo uliotikisa eneo hilo na kuathiri soko la nishati duniani.

    Rais wa Marekani Donald Trump usiku wa kuamkia Jumanne kwa saa za Afrika Mashariki alisema kuwa makubaliano hayo tayari yamesainiwa, ingawa maelezo yake kamili bado hayajawekwa wazi na pande zote mbili zimesema mazungumzo zaidi yanahitajika kabla ya kufikiwa kwa mkataba wa kudumu wa amani.

    Makubaliano hayo yanatarajiwa kuongeza siku 60 zaidi za usitishaji vita uliotangazwa mwezi Aprili na pia kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao Iran imekuwa ikiuzuia tangu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Februari.

    Masuala nyeti, ikiwemo mustakabali wa mpango wa nyuklia wa Iran, yanatarajiwa kujadiliwa katika hatua inayofuata ya mazungumzo.

    "Makubaliano yamesainiwa kikamilifu," alisema Trump baada ya kuwasili nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri duniani wa G7.

    Pamoja na kusema yametiwa saini Trump akaongeza Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance anatarajiwa kuhudhuria hafla rasmi ya utiaji saini wa makubaliano hayo mjini Geneva, Uswisi, siku ya Ijumaa.

    Habari za makubaliano hayo zilisababisha bei za mafuta duniani kushuka hadi kiwango cha chini zaidi tangu Machi 10, baada ya matarajio ya kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha karibu asilimia 20 ya biashara ya mafuta duniani.

    Mkataba huo unachukuliwa kuwa hatua kubwa zaidi hadi sasa katika juhudi za kumaliza mzozo ambao umeua watu wasiopungua 7,000, wengi wao nchini Iran na Lebanon, huku pia ukiitikisa sekta ya nishati duniani.

    Soma zaidi:

  4. Hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja