Trump atishia Iran usitishaji mapigano "umefutiliwa mbali"; Iran yaonya kuwa "watajibu bila uwoga"
Trump alipokuwa akiuita uongozi wa Iran kuwa "wakihuni" na "unaougua", Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema: "Hatulipizi matusi kwa matusi, bali kwa vitendo."
Muhtasari
- Marekani hatimaye "itachukua" nyenzo za nyuklia za Iran - Trump
- Iran yaishutumu Marekani kwa kukiuka Hati ya Makubaliano
- Pakistan, mpatanishi wa Marekani na Iran ataka pande zote kujizuia
- Kurejea kwa mapigano kikamilifu kutakuwa na "madhara makubwa" - UN
- "Hatulipizi matusi kwa matusi, bali kwa vitendo" – Iran
- Vyombo vya habari vya Iran vyajibu kauli ya Trump
- Trump atishia kuzingira tena maji ya Iran baharini
- Tutaishambulia Iran tena leo usiku - Trump
- Maelfu ya watu wajumuika mjini Najaf, nchini Iraq kumuaga Khamenei
- Makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran yafutiliwa mbali - Trump
- Shirika la UN linawataka wahudumu wa meli kusitisha safari katika Mlango Bahari wa Hormuz
- Rais wa Iran aikashifu Marekani kwa kuingilia sheria za Kombe la Dunia
- Qatar yaishutumu Iran kwa "ukiukaji wa wazi" wa sheria za kimataifa
- Video: Tazama Marekani ilivyoishambulia Iran
- Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, asaini sheria inayoongeza muda wa urais wake
- Washirika wa NATO watangaza pauni bilioni 37 kwa mradi mpya wa makombora
- Samatta astaafu kuchezea timu ya taifa ya Tanzania
- Jeshi la Iran limesema limeshambulia maeneo 85 ya kijeshi ya Marekani nchini Kuwait na Bahrain
- Wafanyakazi wa bandari wanavyohofu kupoteza kazi kutokana na matumizi ya AI
- Misri yakerwa na 'dhuluma' na kudai Messi alipendelewa
- Marekani yaanzisha mashambulizi dhidi ya Iran baada ya meli za mafuta kushambuliwa katika Mlango wa Hormuz
Moja kwa moja
Na Lizzy Masinga & Asha Juma
Marekani hatimaye "itachukua" nyenzo za nyuklia za Iran - Trump

Chanzo cha picha, EPA
Trump ameulizwa na vyombo vya habari kuhusu kauli yake ya mwezi uliopita kwamba watu wa Iran walikuwa wema na wenye nia njema kushirikiana nao — ikilinganishwa nay eye leo kuwaita viongozi wa Iran "wahuni".
Alijibu kwa kusema kuwa "amewafahamu", akiongeza kuwa viongozi wa nchi hiyo hawawafanyii wananchi wao jambo jema "kwa kuzingatia matendo yao katika wiki moja au mbili zilizopita."
Trump kisha alisema haamini kuwa mzozo mkubwa utaanza tena, akiongeza kuwa: "Chochote kitakachotokea kitaisha haraka sana."
Rais huyo alirudia kauli zake za awali kwamba Marekani "inaweza" kuishambulia Iran usiku huu.
Aliongeza kuwa mtu yeyote atakayekaribia nyenzo za nyuklia za Iran zilizohifadhiwa chini ya ardhi "atalipuliwa", na kwamba Marekani hatimaye "itazichukua."
Trump: Sidhani kama vita vitaanza tena na Iran

Chanzo cha picha, Win McNamee/Getty Images
Trump ameulizwa katika mkutano na wanahabari ikiwa anaonekana kama vita vinaweza kuanza tena.
"Sidhani kama vita vitaanza tena," alijibu.
"Nadhani hali itamalizika haraka sana. Washambulie meli kadhaa, na sisi tuwashambulia kwa nguvu zaidi."
Ameongeza kuwa awali aliulizwa kama alikuwa anapanga kuishambulia Iran tena, na akasema: "Nilisema tunaweza kufanya hivyo, ndiyo, tunaweza."
"Lakini wanaposhambulia, nasi tunashambulia," alisema. "Tunatumia lugha yao na tunazungumza lugha yao."
Iran yaishutumu Marekani kwa kukiuka Hati ya Makubaliano

Chanzo cha picha, EPA
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa taarifa ikishutumu Marekani kwa kukiuka Hati ya Maelewano (MoU) — makubaliano kati ya Iran na Marekani ya kushirikiana kumaliza mzozo huo.
Wizara hiyo imetaja kile ilichokiita "mashambulizi haramu ya mara kwa mara dhidi ya Iran, pamoja na uamuzi wa Waziri ya Fedha wa Marekani jana usiku wa kufuta leseni ya uuzaji wa mafuta ya Iran" kuwa ni miongoni mwa ukiukaji huo.
Imeonya kuwa Marekani inawajibika kwa "athari mbaya" zinazosababishwa na kuongezeka kwa mvutano huu.
Soma Zaidi:
Pakistan, mpatanishi wa Marekani na Iran ataka pande zote kujizuia

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akiwa na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif wakati wa mazungumzo ya Islamabad mwezi Aprili. Pakistan imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Nchi hiyo ilikuwa miongoni mwa wapatanishi wakuu waliofanikisha kutiwa saini kwa Hati ya Maelewano (MoU) kati ya Marekani na Iran mwezi uliopita, baada ya kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika mnamo mwezi Aprili.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema, "mgogoro mpya sio kwa maslahi ya upande wowote", na akatoa wito kwa "pande zote kujizuia" na kutekeleza ahadi zao katika Hati ya Maelewano (MoU).
Taarifa hiyo inasema: "Hakuna njia mbadala ya kuendelea kushirikiana, zaidi ya kufanya mazungumzo, na kutumia diplomasia."
Soma Zaidi:
Kurejea kwa mapigano kikamilifu kutakuwa na "madhara makubwa" - UN

Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kwa Iran na Marekani kurejea kwenye meza ya mazungumzo
Antonio Guterres amesema katika taarifa kwamba kurejea kwa mapigano kikamilifu kati ya nchi hizo mbili kutakuwa na "madhara makubwa" kwa watu wa eneo hilo, amani na usalama wa kimataifa, pamoja na uchumi wa dunia.
Pia ametoa wito kwa pande zote kuchukua hatua za haraka za kupunguza mvutano.
Soma Zaidi:
Habari za hivi punde, "Hatulipizi matusi kwa matusi, bali kwa vitendo" – Iran

Chanzo cha picha, EPA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X kuwa,
"Kuliita taifa la Iran, ambalo ni la kistaarabu na jasiri, kwa lugha ya kudhalilisha hakupunguzi ukuu wake."
"Wairani wanajulikana kwa ustaarabu, utamaduni, na maadili yao thabiti."
"Hatulipizi matusi kwa matusi, bali kwa vitendo; bila uwoga na kwa ujasiri mkubwa."
Wanajeshi wanane wa Iran wauawa katika mashambulizi ya Marekani - jeshi la Iran
Wanajeshi wanane wa Iran wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Marekani usiku kucha, kwa mujibu wa taarifa inayodaiwa kutolewa na jeshi la Iran.
Taarifa hiyo, ambayo imesambazwa na vyombo kadhaa vya habari vya Iran, imesema wanajeshi hao walikuwa wanahudumu katika jeshi la anga na jeshi la wanamaji.
Aidha, imeeleza kuwa wanajeshi hao walikuwa wamepangiwa kufanya kazi katika miji ya Bandar Abbas na Bushehr.
Vyombo vya habari vya Iran vyajibu kauli ya Trump

Chanzo cha picha, Reuters
Press TV, kituo cha habari cha Kiingereza kinachomilikiwa na shirika la utangazaji la serikali ya Iran (IRIB), kimenukuu chanzo cha usalama kikisema kuwa Iran itafunga Mlango-Bahari wa Hormuz kwa shughuli zote za usafiri wa majini iwapo nchi hiyo itashambuliwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chanzo hicho pia kimesema Iran italenga takriban maeneo mawili kwa kila eneo moja linalolengwa la Iran, kikiongeza kuwa: "Iran haitofautishi kati ya Marekani na washirika wake katika eneo hilo."
Wakati huo huo, shirika la habari la Tasnim, linalohusishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC), limesema kuwa "kufutiliwa mbali" kwa makubaliano ya usitishaji mapigano ya Islamabad "kumetangazwa rasmi" na Trump.
Chombo hicho cha habari kiliongeza kuwa Iran sasa ina "mamlaka yaliyo wazi zaidi" ya kukabiliana na Marekani, Israel na washirika wao katika eneo hilo na duniani.
Awali, mshauri mwandamizi wa Kiongozi Mkuu wa Iran alionya kuwa hali itakuwa "mbaya" katika eneo la Mashariki ya Kati kufuatia matamshi ya Trump.
Soma Zaidi:
Trump atishia kuzingira tena maji ya Iran baharini

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Donald Trump amesema Marekani inazingatia kurejesha mzingiro wa majini kwenye bandari za Iran, hatua ambayo ilisitishwa kama sehemu ya makubaliano ya awali ya kumaliza vita tarehe 17 Juni.
"Tunaweza kuurejesha mzingiro huo," Trump alisema. "Utawahusu Iran pekee; nchi nyingine zinaweza kuendelea kufanya shughuli zao kama kawaida."
Trump pia alisema Iran inaweza kujaribu kutega mabomu ya baharini ikiwa itapata fursa, lakini akaongeza kuwa Marekani ina meli maalumu za kuondoa mabomu hayo baharini.
Aidha, alisema kuwa nchi wanachama wa NATO zimejitolea, wakati wa mkutano wa kilele uliofanyika leo, kutuma meli za kuondoa mabomu ya baharini katika eneo hilo.
Soma Zaidi:
Tutaishambulia Iran tena leo usiku - Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Donald Trump Rais wa Marekani Donald Trump alipoulizwa na wanahabari akihudhuria mkutano wa Nato, kuhusu Iran alijibu kuwa
"Tuliwashambulia sana jana usiku," na kuongezea kuwa "tutawashambulia tena kwa nguvu kubwa usiku wa leo"
Trump ameonya kuwa mashambulizi ya sasa yanaweza kulenga miundombinu muhimu nchini humo ikiwemo madaraja na kampuni za kutoa chumvi kwa maji ya matumizi.
Rais huyo pia amesema Marekani inaweza kuchukua udhibiti wa Kisiwa cha Kharg ambacho ni kituo kikubwa cha kusafirisha mafuta kilichopo kwenye pwani ya Iran na kusema kuwa hakuna kitu ambacho Tehran inaweza kufanya kuzuia hilo.
Rais huyo alisisitiza kuwa "huenda kukawa na shambulio kubwa" usiku wa leo nchini Iran.
Awali Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, alikuwa ametoa onyo la shambulio kufanyika maeneo ya ndani sana nchini Iran.
Soma pia:
Maelfu ya watu wajumuika mjini Najaf, nchini Iraq kumuaga Khamenei

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Msafara wa mazishi ya Ali Khamenei Umati mkubwa wa waombolezaji ulikusanyika hii leo kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei katika mji wa Najaf nchini Iraq.
Jeneza la kiongozi huyo wa zamani wa Iran liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf jana jioni huku Waziri Mkuu wa Iraq Ali Zaidi pamoja na maafisa kadhaa wakuu wa serikali na viongozi wa kidini wakihudhuria hafla rasmi ya kupokea jeneza hilo.
Iraq ilitangaza leo Jumatano kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa.
Ibada ya mazishi mjini Najaf ilianza saa kumi na mbili asubuhi saa za eneo hilo.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na Mustafa Khamenei, mmoja wa wana wa kiongozi huyo wa Iran, pia walihudhuria hafla hiyo.
Mazishi ya mwisho ya Khamenei yatafanyika hapo kesho eneo analotoka la Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.
Msafara wa mazishi mjini Najaf umefanyika wakati mvutano kati ya Marekani na Iran unazidi kutokota kuhusu mlango bahari wa Hormuz.
Awali, Marekani ilikuwa imetangaza kuwa ilikuwa imeipa Iran wiki moja kufanya shughuli hiyo ya mazishi.
Soma Pia:
Trump: Makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran yamefutiliwa mbali

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Donald Trump Rais wa Marekani Donald Trump akiwa pembeni mwa mkutano wa NATO mjini Ankara, amesema kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano kati yao na Iran yamefutiliwa mbali, na kuongezea kuwa mazungumzo na Iran ni “kupoteza muda.”
Trump, alipoulizwa na waandishi wa habari kama makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran yamekwisha, alijibu, “Nadhani yamekwisha.”
Trump ameyasema hayo baada ya Iran na Marekani kushambuliana, huku pande zote mbili zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
Soma pia:
Shirika la UN linawataka wahudumu wa meli kusitisha safari katika Mlango Bahari wa Hormuz

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha za meli Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO), linalosimamia usafirishaji wa kimataifa wa njia za bahari, amelaani mashambulizi dhidi ya meli zinazopitia Mlango Bahari wa Hormuz, kwa muda wa siku mbili zilizopita.
IMO imewataka nahodha wa meli kutotumia njia hiyo ya bahari.
“Mashambulizi haya yamewaweka tena mabaharia wasio na hatia katika hatari kubwa,” amesema Katibu Mkuu wa IMO, Arsenio Dominguez.
Safari za meli, zikiwemo meli za kubeba mafuta zilikuwa zimeongezeka baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran.
Aidha kampuni ya meli ya Bahri imethibitisha kuwa moja ya meli zake, Wedyan, ilishambuliwa wakati ikipita katika Mlango bahari wa Hormuz siku ya Jumanne.
Kampuni ya Bahri imesema shehena ya meli hiyo iko salama pamoja na wafanyikazi wake.
Awali, BBC Verify ilithibitisha kuwa Wedyan ilikuwa miongoni mwa meli tatu zilizolengwa katika shambulio hilo.
Pia unaweza kusoma:
Rais wa Iran aikashifu Marekani kwa kuingilia sheria za Kombe la Dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Iran,Masoud Pezeshkian Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameikosoa serikali ya Marekani kama mwenyeji wa Kombe la Dunia, akiishutumu kwa “kupindisha sheria, kuwanyanyasa washindani wenza, kuwawekea vikwazo na udanganyifu.”
Hii inajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema aliomba FIFA irejelee upya adhabu ya kusimamishwa kwa mechi moja kwa mchezaji wa soka wa Marekani Folarin Balogun, ambapo baadaye FIFA ilimruhusu kucheza katika mechi inayofuata.
Ushiriki wa Iran katika Kombe la Dunia ulikumbwa na vikwazo kutokana na matatizo ya visa na masuala ya usafiri.
Soma Zaidi:
Qatar yaishutumu Iran kwa "ukiukaji wa wazi" wa sheria za kimataifa

Chanzo cha picha, Reuters
Qatar imelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya Bahrain na Kuwait, ikiyataja kuwa hayana uhalali.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema mashambulizi hayo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na wa mamlaka ya Bahrain na Kuwait.
Qatar pia imesisitiza umuhimu wa mazungumzo na diplomasia, kupunguza mvutano, na kuendeleza yaliyofikiwa kupitia makubaliano ya maelewano.
Iran imesema inalenga maeneo ya kijeshi ya Marekani yaliyoko Bahrain na Kuwait, kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi yake yaliyofanyika usiku.
Video: Tazama Marekani ilivyoishambulia Iran
Maelezo ya video, Mashambulizi ya Marekani yalenga boti za kijeshi za Iran. Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa asaini sheria inayoongeza muda wa urais wake

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesaini kuwa sheria muswada unaoongeza muda wake wa kuhudumu madarakani kwa miaka miwili zaidi, hadi mwaka 2030, msemaji wa serikali Nick Mangwana amesema Jumanne.
Mwezi uliopita, mabunge yote mawili ya Zimbabwe yaliidhinisha muswada huo.
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Mangwana alisema: "Imesainiwa, imethibitishwa na sasa ni sheria," akiambatanisha nakala ya sheria hiyo.
Sheria hiyo pia ina kipengele kinachoruhusu rais kuchaguliwa na Bunge badala ya kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi kupitia kura.
Dalili kwamba Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 83, alitaka kuendelea kubaki madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili mwaka 2028 zilianza kujitokeza takribani miaka miwili iliyopita.
Wafuasi wake walianza kuimba kaulimbiu katika mikutano ya chama tawala ZANU–PF wakimtaka apewe muda zaidi ili akamilishe ajenda yake ya maendeleo.
Mwaka uliopita, chama cha ZANU–PF kilipitisha azimio la kufanya marekebisho ya katiba ili kuongeza muda wa mihula ya urais. Pendekezo hilo lilipata idhini ya Baraza la Mawaziri mwezi Februari.
Unaweza kusoma;
Washirika wa NATO watangaza pauni bilioni 37 kwa mradi mpya wa makombora

Chanzo cha picha, EPA
Mataifa kumi na mawili, yakiwemo Uingereza, yanatarajiwa kutumia zaidi ya pauni bilioni 37 sawa na dola bilioni 50 za Marekani katika kipindi cha miaka 10 ijayo kutengeneza kombora jipya la masafa marefu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa Ulaya.
Mradi huo unaojulikana kama Deep Precision Strike umetangazwa rasmi na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza na unatarajiwa kujadiliwa baadaye Jumatano katika mkutano wa NATO unaofanyika mjini Ankara, Uturuki.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer, anahudhuria mkutano huo ambao unatarajiwa kuwa wa mwisho kwake akiwa waziri mkuu.
Anatarajiwa kukosolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa kushindwa kuweka mpango wa kufikia lengo la kutumia asilimia 3.5 ya Pato la Taifa (GDP) kwa matumizi ya ulinzi ifikapo mwaka 2035, ambalo lilikubaliwa na karibu wanachama wote wa NATO mwaka uliopita.
Hata hivyo, Jumatano Sir Keir ataongoza mkutano wa viongozi wapatao 12 kujadili mpango huo mpya wa utengenezaji wa kombora.
Kombora la Deep Precision Strike linaelezwa kuwa miongoni mwa silaha za kisasa zaidi za NATO, likiwa na uwezo wa kushambulia malengo yaliyo umbali wa karibu kilomita 300 kwa usahihi mkubwa, huku uwezo wake ukitarajiwa kuongezwa hadi kufikia kilomita 2,000.
Sir Keir alisema mpango huo unaoongozwa na Uingereza "utasaidia kuwaunganisha washirika wa Ulaya na kuimarisha usalama wa NATO kwa miaka mingi ijayo."
Hata hivyo, kama ilivyo kwa miradi mingine mingi ya kijeshi inayopangwa, kombora la Deep Precision Strike halitarajiwi kuwa tayari kutumika hadi katika miaka ya 2030.
Mnamo Juni, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, alitangaza mapitio ya miezi sita kuhusu uwepo wa majeshi ya Marekani barani Ulaya.
Samatta astaafu kucheza timu ya taifa ya Tanzania

Chanzo cha picha, Getty Images
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ametangaza kustaafu rasmi kuichezea timu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 15, miaka 10 kati ya hiyo akiwa nahodha.
Kupitia chapisho lake katika ukurasa wa Istagram, Samatta amewashukuru wote alioshirikiana nao wakiwemo wachezaji na mamlaka za soka za nchi na serikali katika nyakati za furaha na huzuni.
''Ulikuwa wakati mzuri na wa kipekee katika maisha yangu kuwa mchezaji wa timu ya taifa kwa takribani miaka 15, ninajisikia fahari kusema ninashukuru kwa nafasi hii'' Aliandika Samatta.
Amesema kuwa miaka 10 ya kuwaongoza wenzake akiwa nahodha imekuwa alama kubwa katika maisha yake ikiwemo kufunzu fainali za AFCON mara tatu na kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuweka historia ya kuingia 16 bora kwa mara ya kwanza.
''Nina imani huu ni wakati wa vipaji vipya kupewa nafasi ya kutufikisha katika hatua za juu zaidi.''
''Nikijivunia Utanzania wangu, ninaahidi kuendelea kutoa mchango wangu kwa timu ya taifa katika maeneo mengine yaliyo ndani ya uwezo wangu na uzoefu wangu.'' Aliandika


















