Moja kwa moja, Hamas yakubali kuweka silaha chini Gaza; Trump kutangaza mpango wa Bodi ya Amani

Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuweka silaha chini kabisa katika Ukanda wa Gaza.

Muhtasari

Ruka Video uendelee
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Ghana yaunga mkono muhula wa miaka mitano kwa Rais

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Serikali ya Ghana imekubali pendekezo la kuongeza muda wa muhula wa urais kutoka miaka minne hadi miaka mitano, Waziri wa Sheria wa taifa hilo la Afrika Magharibi amesema siku ya Alhamisi.

    Rais John Dramani Mahama aliunda kamati mwaka jana kupitia upya Katiba ya mwaka 1992 na kutoa mapendekezo mbalimbali, ambayo baadhi yake yamekubaliwa na serikali.

    Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria, Dominic Ayine, alisema kuwa muhula wa Bunge pia utaongezwa ili uendane na muhula mpya wa rais wa miaka mitano.

    Aidha, serikali imeunga mkono pendekezo la kupunguza umri wa chini wa kugombea urais kutoka miaka 40 hadi miaka 35, hatua inayolenga kutoa nafasi kubwa zaidi kwa viongozi vijana kushiriki katika uongozi wa taifa.

    Serikali pia imekubali kimsingi pendekezo la kamati la kupunguza umri wa chini wa wagombea urais, ambao kwa sasa ni miaka 40. Hata hivyo, imefanyia marekebisho pendekezo hilo kwa kuweka umri huo kuwa miaka 35 badala ya miaka 30 kama ilivyopendekezwa awali na kamati.

    Hatua hiyo inalenga kupanua ushiriki wa vijana katika uongozi wa juu wa taifa huku ikiendelea kuhakikisha kuwa wagombea wa urais wanakuwa na kiwango cha kutosha cha uzoefu na ukomavu wa kisiasa.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Usafirishaji wa siri wa madini ya Urani kutoka Kongo

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watafiti nchini Marekani wanasema kiasi kikubwa cha madini ya urani kinachimbwa na kusafirishwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na mauzo ya madini ya kobalti, jambo linalozua wasiwasi kuhusu usalama na uangalizi wa shughuli hizo.

    Watafiti hao wameripoti katika jarida la Nature Communications kuwa wanakadiria hadi tani elfu tano za madini ya urani huenda ziliondoka DRC kati ya mwaka 2000 na 2024 na chini ya asilimia kumi kutangazwa au kuwekwa chini ya ulinzi wa kimataifa.

    Watafiti wanasema matokeo yao yanafichua pengo kubwa katika uangalizi wa nyuklia na mazingira, katika ufunguo wa ugavi wa mpito wa nishati duniani.

    Madini ya Cobalt kutoka Ukanda wa Shaba wa DRC ni muhimu kwa magari ya umeme, simu janja na mpito mpana wa nishati. Lakini watafiti kutoka Princeton na Chuo Kikuu cha Wisconsin wanasema Urani kiasili hufungamana na cobalt na inasafiri bila kutambuliwa katika mauzo ya nje.

    Wanasema baadhi ya nyenzo za mionzi pia zinaishia kwenye taka za mgodi, na kuziweka jamii katika hatari. Watafiti wanatoa wito wa ulinzi mkali wa kimataifa katika mnyororo wa usambazaji wa cobalt ili kuendana na mahitaji yanayoongezeka. BBC iliwasiliana na serikali ya DRC, lakini bado haijatoa majibu kuhusu utafiti huo

    DRC, ni mzalishaji mkubwa wa kobalti duniani.

    Mbali ya Kobalt nchi hiyo pia ina hazina kubwa zaidi duniani ya madini mengine ya thamani kubwa na yale muhimu, yakiongozwa kama vile, koltani, na dhahabu. Rasilimali hizi zilizoko chini ya ardhi, zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani trilioni 24, ndizo zinazochochea masoko ya teknolojia na nishati safi duniani.

    Lakini nchi hiyo imebakia katika hali ya umaskini kutokana na madini mengi kuchinmbwa kiholela bila udhibiti wa serikali na kiasi fulani kutoka na na maeneo yenye utajiri wa madini kukumbwa na vita vya muda mrefu au vinavyojirudiarudia.

    Pia unaweza kusoma:

  3. UEFA yatishia kususia Kombe la Dunia iwapo mipango ya FIFA itaidhinishwa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mpango wenye utata wa FIFA wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi umepata pigo kubwa. Mashirikisho 41 ya soka kutoka Amerika Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean yameukataa mpango huo, yakijiunga na upinzani wa pamoja wa mashirikisho yote ya Ulaya.

    Rais wa FIFA, Gianni Infantino, anasisitiza kuwa mpango huo ungeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili kwa mashirikisho ya soka ya kitaifa duniani kote.

    Mataifa yote 55 ya soka ya Ulaya yamekubaliana kususia Kombe la Dunia iwapo FIFA itatekeleza mpango huo. UEFA imesema timu zake zitashiriki katika mashindano ya FIFA tu iwapo mpango huo hautatekelezwa.

    Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa dharura wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA). Laura McAllister ni makamu wa rais wa Shirkisho la Soka Barani Ulaya.

    "Hatua ni wazi kabisa ni kitisho kwa mchezo wa soka kwa sababu pale tu utakapouza hisa kwa wawekezaji binafsi kwenye mpira ni wazi kabisa inatoa picha tofauti kabisa na msukumo wa tofauti kwa wale ambao ni ni wasimamizi wa Mchezo husika" alisema Laura.

    Uwezekano wa timu za Ulaya kujiondoa katika mashindano ya FIFA huenda ukawakatisha tamaa wawekezaji wa mradi huo wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi chini ya Rais wake Gian Infantino, kwa kuwa timu za Ulaya ndizo zinazotawala mchezo wa soka.

    Soma Zaidi:

  4. Kenya yawa timu ya kwanza kuyaaga mashindano ya WAFCON 2026

    .

    Chanzo cha picha, CAF

    Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake zinaendelea nchini Morocco.

    Kenya imekuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 mbele ya Senegal.

    Kenya imetolewa kwa kufungwa michezo yote miwili ya mwanzo kwani katika mchezo wa kwanza ilichezea kichapo cha 4-0 mbele ya wenyeji Morocco.

    .

    Chanzo cha picha, CECAFA

    Katika mchezo mwingine wa kundi A, Morocco wamewachapa Algeria 1-0 na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

    Leo ni michezo miwili ya kundi B ambapo Ivory Coast inakipiga na Afrika Kusini kabla ya Tanzania kushuka dimbani dhidi ya Burkina Faso.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Rais wa Kenya azungumzia mustakabali wa nchi baada ya mwaka 2030

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Kenya, William Ruto, amesema atazindua rasmi mashauriano ya kitaifa tarehe 12 Agosti 2026 ili kujadili mustakabali wa nchi baada ya mwaka 2030.

    Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni siku ya Alhamisi, Rais alisema kuwa mjadala huo, aliouelezea kuwa tafakuri muhimu zaidi tangu kupitishwa kwa Katiba ya mwaka 2010, utahusisha serikali, vyama vya siasa, serikali za kaunti, wafanyabiashara na hasa vijana.

    Alisema Kenya inaweza kuwa nchi yenye ustawi mkubwa, mapato ya juu na ushindani wa kimataifa ndani ya kizazi kimoja, iwapo itaendelea kudumisha utulivu na umoja wa kitaifa.

    Rais Ruto aliahidi kuwaunganisha Wakenya wote, akisema kuwa mkataba wa maendeleo wa taifa “lazima uundwe na Wakenya wenyewe kupitia mazungumzo ya wazi na ushirikishi wa kitaifa.”

    “Haya si mazungumzo ya kuandaa waraka mwingine wa serikali. Ni kuhusu kujenga mwafaka mpya wa kitaifa,” alisema rais.

    Rais alikiri kuwa maono ya taifa baada ya mwaka 2030 yaani (Vision 2030), ambayo yalilenga kuifanya Kenya kuwa taifa la kipato cha juu cha kati ifikapo mwaka 2030, hadi sasa hayajafanikiwa kufikia malengo yake.

    Hata hivyo, alisisitiza kuwa serikali yake imefanikiwa kurejesha utulivu wa uchumi mkuu, kupunguza mfumuko wa bei pamoja na gharama za ukopaji, na kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.

    Hotuba ya Rais Ruto, ambayo ilijikita zaidi katika maendeleo ya muda mrefu, haikutoa uzito mkubwa kwa changamoto za sasa kama vile deni la taifa, gharama kubwa ya maisha, ukosefu wa ajira kwa vijana, na ukatili wa polisi.

    Kenya itafanya uchaguzi mkuu mwezi Agosti 2027, na rais analenga kugombea muhula wake wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kama rais wa nchi.

  6. Hamas yakubali kuweka silaha chini Gaza; Trump kutangaza mpango wa Bodi ya Amani

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha katika Ukanda wa Gaza huku akiongeza kuwa taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.

    Trump atangaza mpango wa Bodi ya Amani

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Bodi ya Amani imefikia makubaliano ya kuhakikisha Hamas na makundi mengine yenye silaha katika Ukanda wa Gaza yanaweka silaha chini kabisa.

    Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha huko Gaza, na kwamba taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.

    Kwa upande wake, Israel bado haijatoa maoni au kauli rasmi kuhusu tangazo hilo.

    Trump amesema kuwa Israel itaondoka katika Ukanda wa Gaza kadri zoezi la kuachana na silaha litakapokamilika, na akayataja makubaliano hayo kuwa "hatua muhimu kuelekea Gaza hatimaye kutawaliwa na serikali mpya ya Kipalestina."

    Awamu ya pili ya mpango wa usitishaji mapigano huko Gaza ulioratibiwa na Marekani inajumuisha kundi la Hamas kuachana kabisa na serikali.

    Awamu hiyo ya pili pia inahusisha ujenzi upya wa Ukanda wa Gaza, ambao umeathiriwa vibaya na vita vya muda mrefu.

    Soma Zaidi:

  7. Hujambo msomaji wetu. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 31/07/2026