Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Arsenal wampatia kipau mbele Morgan Rogers
Arsenal wamemweka kiungo mwenye umri wa miaka 23, Morgan Rogers, kama lengo lao kuu na wanataka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kutoka Aston Villa (The Athletic).
Liverpool wameulizia uwezekano wa kumsajili kiungo mwenye umri wa miaka 17 kutoka Mexico, Gilberto Mora, akitokea klabu ya Club Tijuana (El Universal).
Everton wanataka kumsajili beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25, Djed Spence, kutoka Tottenham (The Athletic).
Tottenham wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pauni milioni 85 ili kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 19, Junior Kroupi, kutoka Bournemouth (TalkSport).
Inter Miami wanataka kumsajili kipa wa Cape Verde mwenye umri wa miaka 40, Vozinha, baada ya kuachwa na klabu ya daraja la pili nchini Ureno, Chaves (Marca).
Chelsea wanajiandaa kumpa mkataba mpya kiungo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18, Jesse Derry, ili kuzuia nia ya Bayern Munich kumsajili (Football Insider).
Ipswich Town, ambao wamepanda daraja hivi karibuni, wanataka kukamilisha usajili wa rekodi ya klabu kwa kumchukua mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 21, Emersonn, kutoka Toulouse (Give Me Sport).
Paris St-Germain wameanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, Maghnes Akliouche, kutoka AS Monaco (RMC Sport).