Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Man Utd na Liverpool vitani kwa Joao Gomes
Manchester United na Liverpool zimeanza mawasiliano ya kumwania Joao Gomes, Chelsea iko kwenye mazungumzo ya kumsajili Jonathan Rowe, huku klabu ya MLS ikipanga kufanya jaribio la kumsaka Mohamed Salah.
Manchester United na Liverpool zimeanza mawasiliano kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Wolverhampton Wanderers na timu ya taifa ya Brazil, Joao Gomes, mwenye umri wa miaka 25, baada ya mpango wake wa kujiunga na Atletico Madrid kushindikana. (Globo - in Portuguese)
Wakati huohuo, Chelsea iko kwenye mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Bologna, Jonathan Rowe, raia wa England mwenye umri wa miaka 23. Hatua hiyo inakuja huku ikielezwa kuwa winga wa Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye miaka 22, anatarajiwa kuondoka klabuni. (Il Resto del Carlino - in Italian)
Klabu ya Sporting Kansas City inayoshiriki MLS inapanga kufanya jaribio kubwa la kumsajili mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah (34), kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Liverpool. (Athletic)
Klabu kadhaa za England, zikiwemo Coventry City na West Ham United, zinafuatilia kwa karibu kiungo wa Bodo/Glimt, Patrick Berg (24), kufuatia kiwango chake kizuri cha uchezaji akiwa na timu ya taifa ya Norway kwenye Kombe la Dunia. (Teamtalk)
Everton inaonyesha nia ya kumsajili winga wa England wa Newcastle United, Jacob Murphy, 31, ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na klabu hiyo ya St James' Park. (Talksport)
Real Madrid imepanga kufanya kikao na nyota wake wa Brazil, Vinicius Jr, kwa lengo la kukamilisha mazungumzo ya kuongeza mkataba wake, kufuatia taarifa zilizodai kuwa klabu hiyo ilikuwa ikifikiria kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Paris Saint-Germain (PSG) imeanza kufanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Hispania na Barcelona, Ferran Torres, 26, iwapo winga Bradley Barcola ataondoka klabuni katika dirisha hili la usajili. (L'Equipe - in French)
Barcelona imeripotiwa kukamilisha makubaliano na Borussia Dortmund ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani, Karim Adeyemi (24). (Marca - in Spanish)
Nottingham Forest imewasiliana na Fiorentina kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa Brazil, Dodo (27). (Firenze Viola - in Italian)
Wakala wa kiungo mshambuliaji wa AS Roma, Matias Soule, 23, raia wa Argentina, anaendelea na mazungumzo na Sunderland pamoja na Fulham kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia moja ya klabu hizo katika dirisha hili la usajili. (Corriere dello Sport - in Italian)
Mchezaji wa zamani wa Hull City kwa mkopo Oscar Zambrano anatarajiwa kurejea katika klabu hiyo kutoka Maribor ya Slovenia. Mkatabe wake wa awali ulikatishwa baada ya kufungiwa kutokana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni. (Hull Daily Mail)
Fulham imefikia makubaliano ya kumsajili winga wa Celtic, Erskine Rennie,16, huku klabu hiyo ikitarajiwa kulipa takribani pauni 100,000 kama fidia kwa mchezaji huyo wa akademi ya Scotland. (Sky Sports)